"Tukianza kutafuta asiye na dhambi ili tujadiri naye kuhusu kesho yetu hatutampata,hivyo tuna kila lazima ya kuacha chuki na visasi na kuwaamini viongozi wetu"
"Siwezi kuwa chawa wa Mama (Rais Samia) na wala sio wa chawa wa mama, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, utawala wa Mama japo alikuwa ni makamu wa Hayati Rais Magufuli wana tofauti kubwa sana ni kama mbingu na mchanga, mtu yoyote mkweli ataliona hilo"
"Nina imani sana na Rais Samia na Serikali yake ya chama chake,hadi sasa naona kuna nia na dhamira njema"
Freeman Mbowe - Mwenyekiti CHADEMA #ClubHouse
Mbowe kayasema haya wapi mkuu. Ni muhimu kukamilisha nukuu yako ili tuwe na uhakika nayo bila ya mashaka yoyote.
Hata kama yamesemwa na Mbowe, bado hajaeleza ni katika mambo gani hasa kuna tofauti kati ya yule 'kichaa' na huyu 'Maza Mizinguo'.
Kama mlinganisho ni katika maeneo ya "UKICHAA", hakika hapo hakuna ushindani kati ya huyu na yule. Hili liko wazi kabisa.
Lakini uongozi wa nchi hauishii kwenye 'ukichaa' pekee. Kuna mambo mengi mengine ambayo yanahitajika kutazamwa na kuyapima katika utendaji wa watu wanaolinganishwa.
Nitaungana na Mbowe katika kusifu juhudi za Maza Mizinguo katika eneo la kujali utu wa wengine; lakini kwa sasa sifa zangu zitaishia hapo.
Sikubaliani na Maza kwenye mambo yake ya "ufunguzi wa nchi" kiholela bila kuwa na mikakati ya kudhibiti uchafu unaoendana na wahusika wanaopewa uhuru usio kikomo kuendesha na kuvuna mali za waTanzania.
Mbowe hajazungumzia chochote kuhusu "sera" za Maza. Hakuna kinachotofautisha sera za CHADEMA na CCM ya Maza Mizinguo?
Hili halihusu "Kutafuta asiye na dhambi", na wala kutofautiana katika sera hakuhusu "chuki wala visasi". Sasa Mbowe aseme, akipinga sera za CCM itaonekana ana chuki na kutafuta visasi?
Akidai Katiba Mpya, ataonekana hana shukrani na aliyotendewa na Maza Mizinguo, hata kama ilikuwa ni haki yake kutendewa hivyo?
Mwisho, kama Mbowe anaona kuwa Maza anafaa, basi amuhimize asifanye kampeni za kujiuza hata kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi 2025. Mtu anayeonekana kwa wananchi anafanya vizuri hahitaji kujiuza namna anayofanya sasa hivi. Hii ni kasoro kubwa kwake.