Mnyonyaji mkubwa wa walimu ni cwt

nchasi

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Posts
564
Reaction score
185
Ndugu walimu wote tanzania!
Hongereni kwa kazi ya ujenzi wa taifa hususani katika kukuza vijana kitaaluma na maadili bora.
Aidha niwape pongezi kwa uvumilivu wenu maana mmechagua kazi yenye changamoto nyingi sana mfano mazingira duni, maslahi kidogo yaliyoambatana na makato lukuki nk.
Ndugu walimu kwa idadi yenu yaani walimu wa shule za msingi na sekondari mnafikia takribani 301,960 na ni nguvu kazi kubwa na ya kujivunia kwa taifa lenye uchu wa maendeleo.
Lakini pamoja na weledi mlionao mmeshindwa kubaini mnyonyaji wenu namba moja ni cwt ambao bila huruma wanawapunguzia hicho kidogo mpatacho bila makubaliano na hakuna msaada wowote kutoka kwao angalieni mafanikio waliyonayo viongizi wenu wanaowanyonya bila huruma.
Angalia hesabu rahisi jinsi wanavyojipatia mapato murua kutoka kwenu kila mwezi.
301,960 × 10,000 = 3,019,600,000 kwa maneno ni bilioni tatu milioni kumi na tisa na laki sita {hayo ni makadirio ya wastani maana mishahara yenu inatofautiana } kwa mwaka mmoja zidisha hicho kiwango mara 12.
Nawashauri ndugu walimu hicho chama kinawanyonya kweli amkeni, chukueni hatua za haraka ikiwezekana toeni tamko makato yasitishwe mara moja maana mmegeuzwa vitegauchumi vya mapato ya cwt. Amkeni walimu kila shule mjitetee mbele ya huyu mkoloni asiye na huruma kwa kipato chenu duni halafu haoni huruma tafteni wanasheria ili cwt iwalipe kwa uonevu na ifilisiwe mrudishiwe magawiwo yenu mliyokatwa bila makubaliano.
Nawasilisha
 
Hivi kwa mwalimu kujiunga na cwt, ni hiari au lazima?
 
Kwa walivyo sikio la kufa, sidhani kama watakusikia na kukuelewa.
 
yaani mtoa mada umeniamshia machungu yalikuwa yamepoa,
wanachukua hela nyingi sana inakaribia na ya bima ya afya ambayo inakutibu wewe na wategemezi wa 4 halafu eti ni ya kuendesha chama. ?? unakuta hujawahi jaza form zao lakini wanakukata.

huu ni wizi kwani kujiunga katika chama chochote ni mkataba ambao mteja anajaza mwenyewe , wanapata wapi hizi taarifa nakuanza kumkata mtu kama mwanachama??
 
Tatizo walimu tupo disorganized na ndani ya walimu hao hao kuna wengine wananufaika na cwt hawapo tayari chama kife.
 
Tupigie hesabu na TUICO, kifupi vyama vyote vya wafanyakazi ni genge la wezi, mimi nashukuru toka nianze kazi sijawahi kuchangia au kuwa mwanachama wa vyama hivi vya kilaghai, na kwa nafasi niliyinayo kwa sasa siruhusiwi kuwa mwanachama wa hivyo vyama,
 
kaka umenena ila sasa hiki chama huna jinsi ya kujitoa maana hawa wako sambamba na mwajiri wetu
 
Kujiunga na chama chochote kile ni lazima uisome katiba yao na uielewe, Tatizo letu hatupendi kusoma na ndio maana tunapigwa kizembe, TUICO wanakata 2% ya basic pay sasa waulize wanaifanyia nini hiyo 2%? Mimi nashukuru huyu mnyonyaji hakuwahi kuionja hela yangu zaidi ya kunipa vitisho nikifukuzwa kazi hawatanitetea
 


hoja nzuri sana,,cha msingi tujiulize ni wapi pa kuanzia ili kufikisha malalamiko yetu? mana wananikera sana hawa hamaa na bado sijaona mchango wao kwa mustakabali na maslahi ya walimu.
 
Maneno matupu hayavunji mfupa, kila siku hamuishi kuisema cwt, mbona hakuna hatua yoyote mnayochukua?
 
Mkuu unamda gani tangu uanze kazi hii!? Mbona jambo hili lishafafanuliwa sn tu! Nakushaur kama wewe mwalim, kupitia m/kiti wa cwt tawi lako mwiteni katib wa cwt wilaya ajekuwaelimisha zaidi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…