nchasi
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 564
- 185
Ndugu walimu wote tanzania!
Hongereni kwa kazi ya ujenzi wa taifa hususani katika kukuza vijana kitaaluma na maadili bora.
Aidha niwape pongezi kwa uvumilivu wenu maana mmechagua kazi yenye changamoto nyingi sana mfano mazingira duni, maslahi kidogo yaliyoambatana na makato lukuki nk.
Ndugu walimu kwa idadi yenu yaani walimu wa shule za msingi na sekondari mnafikia takribani 301,960 na ni nguvu kazi kubwa na ya kujivunia kwa taifa lenye uchu wa maendeleo.
Lakini pamoja na weledi mlionao mmeshindwa kubaini mnyonyaji wenu namba moja ni cwt ambao bila huruma wanawapunguzia hicho kidogo mpatacho bila makubaliano na hakuna msaada wowote kutoka kwao angalieni mafanikio waliyonayo viongizi wenu wanaowanyonya bila huruma.
Angalia hesabu rahisi jinsi wanavyojipatia mapato murua kutoka kwenu kila mwezi.
301,960 × 10,000 = 3,019,600,000 kwa maneno ni bilioni tatu milioni kumi na tisa na laki sita {hayo ni makadirio ya wastani maana mishahara yenu inatofautiana } kwa mwaka mmoja zidisha hicho kiwango mara 12.
Nawashauri ndugu walimu hicho chama kinawanyonya kweli amkeni, chukueni hatua za haraka ikiwezekana toeni tamko makato yasitishwe mara moja maana mmegeuzwa vitegauchumi vya mapato ya cwt. Amkeni walimu kila shule mjitetee mbele ya huyu mkoloni asiye na huruma kwa kipato chenu duni halafu haoni huruma tafteni wanasheria ili cwt iwalipe kwa uonevu na ifilisiwe mrudishiwe magawiwo yenu mliyokatwa bila makubaliano.
Nawasilisha