SoC02 Mnyonyeshe Mtoto

Stories of Change - 2022 Competition

Lucky65

New Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
1
Reaction score
3
Tafiti za kiafya zinaonyesha kuwa mtoto anahitaji sana maziwa ya mama kwani maziwa hayo yana faida nyingi sana kwa watoto katika maendeleo yao ya ukuajia wa mwili na akili.

Maziwa ya mama yana virutubisho kama vile pprotini, mafuta, wanga, vitamini n.k ambavyo mtoto anavihitaji sana ili akue.

Washauri wa kiafya wanashauri mtoto anyonyeshwe bila kulishwa kitu kingine chochote walau ndani ya miezi sita ya kwanza tangu kuzaliwa kwake na aendelee kunyonyeshwa mpaka atapofikia umri wa miaka miwili.

Ni nini faida za kumnyonyesha mtoto
Maziwa ya mama yana protini za aina mbili kuu ambazo ni whey 60% na casein 40% ambazo zina huo mchanganyo asilia ambao mtoto anao uwezo wa kuumeng'enya vizuri. Aidha kuna aina nyingine za protini zinazopatikana kwenye maziwa ya mama tu ambazo zina faida kubwa hususani kwenye kuuwezesha mwili kupambana na vimelea vinavyoweza kusababisha maradhi nazo ni:

i. Lectoferin hizi huzuia ukuaji wa vimelea kwenye mfumo wa chakula ambavyo hutegemea madini chuma katika kukua kwake hivyo kuongeza usalama wa afya ya mfumo wa chakula wa mtoto.

ii. Secretory IgA, IgG, na IgM ambazo husaidia kuepusha uvamizi wa vimelea aina ya E.Coli pamoja na kuzuia mtoto kupata athari za mzio (Allergies)

iii. Lysozyme hii husaidia kupambana na vimelea vya E.Coli pamoja na Salmonella
iv. Bifidus factor hii husaidia kuchochea ukuaji wa lactobasilus ambaye ni bakteria anayezuia kukua kwa bakteria hatarishi kwenye mwili wa mtoto.
Pia maziwa ya mama yana mafuta ambayo husaidia kukua kwa ubongo na kuwezesha mwili kuweza kufyonza vitamini muhimu kwa mtoto na pia husaidia kwenye retina ya macho na mfumo mzima wa Neva

Changamoto kubwa imeonekana kwa wamama na mabinti wa siku hizi hawapendi kunyonyesha watoto sababu ni kwamba wanadai watapoteza mwonekano wao wenye mvuto na hii imechagizwa pakubwa na maendeleo ya utandawazi ambapo wengi kwa sasa wanafanya Bottlefeeding kwa watoto wao.

Tutazame madhara ya kumnywesha mtoto maziwa badala ya kumnyonyesha

Achilia mbali gharama utakazoingia wakati unaandaa yale maziwa ilihali maziwa ya kunyonyesha ni bure kabisa gharama ya fedha si kitu lakini tazama na ufikirie madhara anayoweza kupata mtoto na wewe pia usipomnyonyesha mtoto wako
Kwa kufanya bottlefeeding mtoto anaweza pata utapia mlo kwani maziwa yanayoandaliwa ni vigumu sana kuwa na ufanisi wa asilimia 100 kwenye ule mchanganyo ambao mtoto anaweza kumeng'enya yaani 60 kwa 40.

Lakini pia zile protini zinazosaidia kujenga kinga ya mwili zinapatikana kwenye maziwa ya mama tuu na haziwezi kuzalishwa viwandani hivyo mtoto asiponyonya anaweza kuwa na afya duni.

Lakini pia maziwa ya kuandaliwa yanakua hayapo kwenye kiwango stahiki cha joto kama maziwa ya mama na yanakua na hatari kubwa ya kubeba vimelea (contaminated) wakati yanaandaliwa mpaka mtoto atapokuja kunywa. Aidha maziwa ya kuandaliwa tofauti na maziwa ya mama yanaweza sababisha mzio (Allergies effect) kwa mtoto.

Hiyo ni kwa upande wa mtoti lakini pia kuana athari anazoweza pata mama kama asiponyonyesha kama vile anakua katika hatari ya kupata kansa ya matiti na kansa ya mfumo wa uzazi.

Tafiti zinaonyesha kunyonyesha mtoto kunamsaidia mama aliyetoka kujifungua kupona haraka na kuurudisha mfumo wa uzazi katika hali yake ya kawaida.

Ikumbukwe sababu pekee ya kumfanya mama asimnyonyeshe mtoto wake ni kama anasumbuliwa na maradhi ambayo yanaweza kuambukiza au yanayomfanya ashindwe kunyonyesha kwa kusanabisha udhaifu wa misuli.

Kuna wamama huwa wanasumbuliwa na tatizo la kukosa maziwa hivyo wanashindwa kunyonyesha watoto wao suluhisho la tatizo hili ni kama ifuatavyo
Mama anapokosa maziwa yafaa ale vyakula kama vile Ndizi, Nyama, Uji wa pilipili mtama , Mbegu za maboga, Dagaa, Samaki, Maini, Maharage, Maziwa na Maji vyakula hivi vina virutubisho kama vile madini chuma, zinc, selenium, calcium, vitamini, protini na omega 3 ambavyo huchochea kuongezeka kwa maziwa kwenye mwili wa mama
Maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto hakikisha unamnyonyesha ni wajibu wako na ni haki yake isipokua tuh kwa mazingira ya maradhi.
"Ewe binti usiache kumnyonyesha mtoto kwa madai ya kutaka kubaki na mwonekano wako huo kwani ukiwa na mtoto mwenye afya njema utakuwa na mvuto zaidi" #MnyonyesheMtoto

Tujenge vizazi bora vyenye utimamu mkubwa wa mwili na akili.

Makala hii imeandaliwa nami
Bahati Mrutu (Lucky)
 
Upvote 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…