The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kikwazo kikuu cha kupatikana kwa katiba mpya hapa nchini Tanzania ni mnyukano wa wanasiasa. Wapinzani wanaitaka katiba mpya kama chombo cha kuwasaidia kuitoa ccm madarakani. Ikiwa mantiki iko hivyo hata wewe ungekua CCM usingekubali.
Kwa upande wa ccm wanaona hii katiba inawasaidia kuitawala nchi bila shida wala tatizo, zaidi ya Hilo wanaona kitisho cha kuruhusu katiba mpya ni kupoteza hiyo fursa.
Kwa upande wa wananchi wengi wao hawana uelewa wowote kuhusu mambo ya katiba hivyo, wanategemea kulishwa na wanasiasa.
Kwa mantiki hiyo huu msuguano utaendelea hadi atokee mtu wa pembeni atie shinikizo ili ccm ikubali kama ilivyokubali mfumo wa vyama vingi.