Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mkoani Tanga, Timotheo Mnzava, amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi wa Kituo cha Afya Magoma wanaodaiwa kuwalipisha wajawazito shilingi 200,000 kwa ajili ya upasuaji wakati wa kujifungua, kinyume na maelekezo ya Serikali.
Agizo hilo limetolewa kufuatia malalamiko ya wananchi wa Kata ya Magoma, wakati wa ziara ya Mbunge huyo Januari 5, 2025, alipozuru kituo hicho kwa ajili ya kukabidhi gari la wagonjwa (ambulance) lililotolewa na Serikali.
Katika ziara hiyo, wananchi walilalamikia vitendo vya baadhi ya watumishi wa kituo hicho, ambao pia wanadaiwa kuwatoza wagonjwa shilingi 10,000 wanapoanza kliniki.
Tumepokea taarifa kuwa kuna watu wanalipa hadi shilingi 200,000 kufanyiwa upasuaji, maelekezo ya Serikali ni kwamba wanaostahili kuhudumiwa bure, wahudumiwe bila malipo, wanaostahili kulipa, walipe kulingana na maelekezo ya Serikali," alisema Mnzava.