MO amenunua gari inayoaminika kuwa na mfumo mkubwa wa ulinzi wa kidigitali

MO amenunua gari inayoaminika kuwa na mfumo mkubwa wa ulinzi wa kidigitali

Ingekua linakwepa mabom hapo sw
Ingekua haiwez kuguswa, kuharbiwa mifumo ya kamera na hata kufunguliwa au kupasuliwa milango bila ridhaa ya mmiliki

....ayo yote yangewezekana nami ningeitafuta hii kampuni[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

babawawili
 
Baada ya kile kinachooneka kuwa ni kuimarisha ulinzi na kutuma salaam kwa watekaji, MO amenunua gari inayoaminika kuwa na mfumo mkubwa wa ulinzi wa kidigjtari.
View attachment 975439
Muda mfupi baada ya MO kuposti picha hiyo (Tesla Model 3), mtandao unaoaminika kule Nigeria wa Pulse, uliandika kuwa MO amenunua gari hilo kwa dola za Marekani 35,000 (Sh80 Milioni). Hata hivyo, mtandao wa Tesla wenyewe unaandika kuwa Model 3 inauzwa dola 46,000 (Sh106 Milioni).

Makadirio ya kununua Tesla Model 3, kulisafirisha mpaka nchini, kodi na kuwatela wataalamu wa kumfungia mfumo wa kuchaji gari lake nyumbani kwake, inaweza kufikia kati ya Sh250 milioni. Watekaji wote salamu zenu kutoka kwa MO. Ni salamu za kufungia mwaka 2018.

Tesla Model 3 ni gari linalozalishwa na Kampuni ya Tesla Inc ambayo yenyewe imejikita kutengeneza magari yasiyotumia mafuta. Magari ya Tesla yanatumia gesi na umeme tu.

Tesla M3 halina injini kabisa. Gari lote ni umeme. Halina muungurumo. Linatembea kimyakimya, kama huelekezi macho lilipo, litapita nyuma yako pasipo wewe kujua kama kuna gari limekupita.

Lina camera za dashboard, yaani dashcam. Zenyewe huchukua matukio yote mbele, nyuma na pembeni kuzunguka gari. Ni kamera za mzunguko wa nyuzi 360 na huchukua video zenye ubora wa hali ya juu, yaani HD.

Sifa nyingine ni Tesla Model 3 ni gari kamili la kidigitali. Halina ufunguo, linatumia rimoti yenye umbo la gari lenyewe. Ukishaingia kwenye gari, kwenye dashboard kuna kitu mfano wa tablet. Hiyo ndiyo unaitumia kuendesha gari.

Ukiamua hata hiyo rimoti yake si muhimu sana. Unaweza kuweka App ya gari kwenye simu, kisha utaitumia simu yako kuendesha gari, kufungua milango, kufunga na kulidhibiti.

Tesla Model 3 lina mfumo wa autopilot ya kiwango cha juu kama ndege. Autopilot huwezesha ndege kujiongoza yenyewe ikiwa angani kwa kutambua sehemu hatari kupita na kuchagua uelekeo salama.

Kwa Tesla Model 3 kuwa na autopilot, inalifanya gari hilo kujiendesha lenyewe. Lina kamera za kutosha zenye kuona mbali (autopilot cameras), hivyo hata dereva akilikimbiza, lenyewe hutambua hali halisi ya barabara mbele ya safari, kwa hiyo hupigia kengele ya alarm. Dereva asipotii, gari lenyewe hufunga breki. Gari lina automatic break.
Gari haliwezi kugonga. Unaweza kuliendesha hata ukiwa umelala, maana likikaribia kugonga gari lingine au kitu chochote, linaona na kufunga breki lenyewe (umeambiwa lina automatic break). Ni gari ambalo limepiga hatua kubwa kufikia kiwango cha kuwa gari lenye kujiendesha bila dereva.

Musk alisema, Tesla Model 3 haliwezi kuibiwa kabisa. Kwani katika dashboard limefungwa kitu kinaitwa Smart Summon. Kwa hiyo popote pale litakapokuwa, mmiliki wa gari kwa kutumia rimoti au simu yake yenye App ya Tesla Model 3, ataweza kuliita gari, hata likiwa nchi nyingine. Kumbuka linaweza kutembea bila dereva.

Kwa mantiki hiyo, kama MO angekuwa anatumia Tesla Model 3 kipindi kile alipovamiwa na watekaji Hoteli ya Colosseum, October 11, 2018;, maana yake sasa hivi gari hilo lingerekodi matukio yote, na pengine watekaji wangejulikana kwa picha zao siku ya kwanza.

Huu ni ujumbe murua kabisa kwa wale watekaji, dawa yao ndio imepatika.

Ref. Jeuri ya Mo Dewji atuma salamu kwa watekaji
Ah haata anunue ndege awe anasafiri juu na chini, watekaji watamsubiria hata akiwa ameingia toilet anatekwa na camera hazioneshi hata km alikwepo..kuteka mtu ni hesabu nyingi sio utaenda tu umwombe kumteka
 
Afunge mziki mzito alafu apite mitaani vioo chini ikisikika ile ngoma ya Mr Nice "kikulacho kiko kinguoni mwako"
 
Gari ya namna hiyo ni kujiongezea stress tu, kwa maelezo yako - ukilinganisha na barabara za hapa bongo litakuwa linaziama kila sehemu madimbwi. Tatu wasiojulikana wanajua jinsi ya kufanya hadi wampate bila hizo camera kujua. Anaweza akawa kwenye busness meeting wakamuingilia na kumkamata. Cha msingi awe makini tu.
 
Kwa huuu unyani wetu tusahau kitu inaitwa maendeleo.(unyani nimekopa kwa marehemu mtikila r.I.p).
HAKIKA, MAGARI KAMA HAYO YATATUNGIWA SHERIA SPECIAL KABISA.

Hii ndio TANZAGIZA.

- Sheria ya mitandao inatungwa with JF in mind.

- Sheria ya takwimu special for ZITTO.

- Sheria ya vyama vya siasa special for UPINZANI.

- Sheria ya TLS special for TUNDU LISSU.
 
woiiiii iyo picha aliipost instagram account yake ,alafu tesla model 3 haipo hata top 100 ya secured car ....nikadhani utaongelea security customized za gari ila umeongea hamna engine ,halitoi sauti na camera ambayo hata simu ya elfu 25 Inayo camera ..... itazuia nini labda
Uandishi full roho mbaya!
 
Hivi karibuni nitaingiza mtambo wangu Audi A8. Hio Tesla ya Mo ni cha mtoto. Wana jf mniombee nikubaliwe kuiingiza nchini na kuisajili salama.
Acha kiburi uombewe
 
Dogo ametumisi ngoja tumvizie siku simba inacheza
 
Usicheze na difenda la watu wasiojulikana wewe, tesla itapiga vipicha lkn wadau watamnyofoa tu kama watamtaka
 
Wahuni wanateka ndege sembuse hiyo gari??? Tena safari hii wakimfuata kama ndiyo kanunua hiyo gari kuwatisha wataondoka nae na hiyo gari last time walimwachia ile Range now wakija watasepa na hiyo Musk
 
Watu wasiojulikana hawafanywi lolote,rejea tukio la kutekwa na kuumizwa vibaya aliyekuwa kiongozi wa madaktari Dr Ulimboka,Aliyemteka Dr ulimboka anajulikana na Kubenea aliweka wazi mawasiliano ya mtekaji hadi dakika za mwisho na Dr ulimboka alimtambua na alimtaja ni nani lakini hajafanywa kitu,kwahiyo hiyo Tesla M3 hata ikirecord hadi sura za wasiojulikana hawatafanywa kitu chochote!!
 
Back
Top Bottom