Mo anacheza na akili za wajinga wasiojitambua?

Mo anacheza na akili za wajinga wasiojitambua?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Je, kuna umuhimu wa kuuliza mashabiki wapige kura iwapo Simba inahitaji kocha tena kwenye mtandao?

Je, ana uhakika gani waliopiga kura ni wana Simba?Unadhani leo akatokea mjinga mmoja pale utopolo tuseme rais wa timu atangaze kura kuuliza iwapo yanga inahitaji kocha mpya unadhani asilimia ngapi ya mashabiki wa yanga watapiga kukubali ama kukataa?Je huoni watakaopiga kura ya kumkataa ni mashabiki wa Simba? Na unaweza kushangaa kuwa asilimia zaidi ya 60% wakamkataa Nabi lakini wote hao wakawa mashabiki wa Simba?

Mimi nilivyoona sikupiga kura kwani ni upuuzi na siwezi kufanya hivyo kwa kuwa najua tatizo la Simba sio kocha bali ni wachezaji.

Timu inahitaji wachezaji wakubwa na huo ni ukweli ulio wazi,lakini wewe unajaribu kukwepa kusajili badala yake unataka kutuletea makocha wako wapumbavu wa kizungu waanze upya na timu jambo ambalo ndilo hatari sana kwa sasa.

Kama kuna shabiki wa Simba anadhani tatizo tulilo nalo Simba ni mwalimu,na anadhani akileta mwalimu mzungu basi Kibu atakuwa Mbape basi nitaamini magonjwa ya akili sasa yamefikia kiwango cha juu mno hapa nchini.

Mo kama timu imemshinda awaachie wengine aache janja ya nyani kula hindi bichi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mo ache janja janja asajili wachezaji wazuri kwenye ili dirisha dogo
 
Je, kuna umuhimu wa kuuliza mashabiki wapige kura iwapo Simba inahitaji kocha tena kwenye mtandao...
Don't take everything serious kwenye social network mambo mengine ni ya kufurahisha kijiwe tu mbona hata Elon musk juzi tu aliuliza watumiaji wa Twitter kama wanapenda aendelee kuwa CEO wa Twitter ila wengi walisema hapana kwenye social media vitu vingine ni utani tu.
 
Mwache tajiri afanye yake, wewe mla makongoro hata jezi ya simba orijino huna.
 
Mo alichofanya ni kutumia mojawapo ya mbinu ya Management ili kujua mtazamo wa watu kihusu Kocha Mgunda. Wewe kwa akili yako ndogo ya kiutopolo ukaona anataka kuleta kocha mzungu.

Pili unajichanganya na kuonesha chuki ya wazi kwa Mo. Yeye amehoji kwenye ukurasa wake binafsi ambao sio official kwa masuala ya timu.

Kuonesha chuki yako ilivyokupofusha unazungumzia suala la usajili wa wachezaji wazuri na wakati haikuwa mada ya Mo kuhusu usajili. Pia hakuna sehemu aliyosema timu haitasajili wachezaji wazuri.
 
Kazi yenu kulalamika tu
Wakati hamna pesa mnayotoa hapo Simba
Ni hatari Sana Mo kuwasikiliza wapumbavu wanaojiita mashabiki

Mnataka wachezaji wenye quality wakati nyie hamchangii chochote hapo Simba!
We ndiye mpumbavu sana.Mo xtra na vingine kama hivyo unakunywa wewe demu wake tu?
Au unadhani jezi za Simba mnavaa wake za Mo pekee?
Unashindwaje kujua mchango wa shabiki mmoja mmoja?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mgunda ni kocha wa muda na hata yeye Mgunda analijua hilo. Suala la Mo kuendesha kura ya maoni ni haki yake hata wewe unaweza anzisha uzi hapa JF.
 
Mo alichofanya ni kutumia mojawapo ya mbinu ya Management ili kujua mtazamo wa watu kihusu Kocha Mgunda. Wewe kwa akili yako ndogo ya kiutopolo ukaona anataka kuleta kocha mzungu.

Pili unajichanganya na kuonesha chuki ya wazi kwa Mo. Yeye amehoji kwenye ukurasa wake binafsi ambao sio official kwa masuala ya timu.

Kuonesha chuki yako ilivyokupofusha unazungumzia suala la usajili wa wachezaji wazuri na wakati haikuwa mada ya Mo kuhusu usajili. Pia hakuna sehemu aliyosema timu haitasajili wachezaji wazuri.
Mbinu gani na unauliza watu wa yanga wakuamulie nini cha kufanya?
Unatumia kigezo gani kujua aliyepiga kura ni mwanasimba?
Ninyi ndio wasomi mliojaa kamasi kichwani kwa sababu ya kukariri na kupata degree za chupi kisha mnakuja hapa na kujiona mnajua sana

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom