Mo anajenga klabu, Manji anatafuta sifa na manufaa

Mo anajenga klabu, Manji anatafuta sifa na manufaa

Mambo ya kawaida kwa nchi gani.. acha kupotosha
Sio kila kitu lzm uige nitajie muungano wa Tanzania km Kuna sehem duniani Kuna muungano km huu lkn mpk leo tunaendelea na muungano wetu acha kukariri.
 
Yanga wasipokuwa makini hawatapata hata ndururu kwenye 'mkodisho ', itakuwa kama wawekezaji wa kwenye sekta ya madini, wanatangaza hasara kila mwaka ili kukwepa kodi lkn wawekezaji wanauza makampuni hayo kwa pesa ndefu.

Vv
 
Sio kila kitu lzm uige nitajie muungano wa Tanzania km Kuna sehem duniani Kuna muungano km huu lkn mpk leo tunaendelea na muungano wetu acha kukariri.
Dah.. siumesema nchi zingine ni kawaida, nikakuomba nitajie sasa kosa liko wapi.
 
Unabisha ili mradi ubishe au unabisha ukijua unacho bishania? siku shangai ni wewe tena ligi na ianze.
Ubishi uko wapi mkuu.. weka DATA kuwa nchi fulani na timu fulani ilikodishwa ili tufunge ukurasa
 
Kumekuwepo na mitizamo tofauti kuhusu matajiri Mo na Manji kujiingiza katika masuala ya soka. Tangu zamani Mo amekuwa akiisaidia Simba kwa hali na mali kwa manufaa na maendeleo ya klabu. Mo ameazimia kununua 51% ya hisa za klabu ya Simba kwa thamani ya Tsh bilioni 20. Aidha, nguli huyo wa kibiashara amemwaga noti zenye thamani ya Tsh 100 milioni ndani ya klabu ya Simba kwa ajili ya kusaidia usajili wa wachezaji vitasa. Hii yote ni kwa ajili ya manufaa na maendeleo ya klabu ya Simba SC.

Baada ya Manji kumsikia Mo alivyoazimia kuisuka Simba, roho ikamuuma. Eti sasa anataka kuikodi klabu ya Yanga kwa muda wa miaka 10 ili aitumie nafasi hiyo kupiga hela kwa manufaa yake binafsi kwa mgongo wa “ufadhili”. Anaona unyonyaji alioinyonya Yanga bado haujatosha, sasa ameamua kabisa kukodi klabu ili apige fedha vizuri.

Kwa lugha nyingine unaweza kusema kwamba Manji ni opportunist. Anatumia trick ya kupambana na Mo kwenye soka la watani wa jadi kwa manufaa yake binafi na familia yake. Eti mtu anakodi klabu kwa miaka 10 na wanachama wanamkubalia! Ama kweli hizi njaa za wanachama wa Yanga ni shida.

Manji amekuwa akiifaidi Yanga kisiasa kwa muda usiopungua miaka 20! Baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni ndani ya chama chake (CCM) katika uchaguzi wa mwaka 2000 kwa sababu ya kugawa rushwa kwa wajumbe, Manji aliamua kununua uenyekiti wa Yanga ili ajijenge kisiasa. Umaarufu wake wa kisiasa ulishuka sana tangu alipojihusisha katika ugawaji wa rushwa katika kura za maoni, Jimbo la Temeke. Alipoingia uongozini ndani ya klabu ya Yanga, umarufu wake umepanda hadi ameshinda udiwani wa Kata ya Mbagala. Kuibuka kwake kuikodi klabu ya Yanga ni ushahidi tosha kwamba sasa anausaka ubunge katika uchaguzi mkuu ujao. Jamani tuwe makini sana na huyu K@njib@i…hana nia njema hata kidogo.
tunamkubali hivyo hivyo mdau.
 

Attachments

  • 1470758470140.jpg
    1470758470140.jpg
    6.3 KB · Views: 21
Wewe ipua.
Mbona unakimbia kivuli chako.. ulidai kuwa kukodisha timu kwa waliotutangulia ni jambo la kawaida.. tukakuomba data bado hujatoa, sasa kwanini unasema niipue mimi ilhali ww ulisema mambo ya kawaida

Rejea comment yako ya mwanzo
 
Mbona unakimbia kivuli chako.. ulidai kuwa kukodisha timu kwa waliotutangulia ni jambo la kawaida.. tukakuomba data bado hujatoa, sasa kwanini unasema niipue mimi ilhali ww ulisema mambo ya kawaida

Rejea comment yako ya mwanzo
Ni kawaida sana tu na nina rejea kusema hivyo kama ni Data endelea kusubiri,Wengine ni waelewa nakuona wewe ndio unaye omba usivute wingi? Sasa siumeona vime chemka ndio ipua sasa.
 
Back
Top Bottom