Pia inashangaza et shabiki wa mkia kumjadili Yanga eti anakosea kumpa timu manji haaah kufweni mikia nyie
Simba waliamini kuwa wakiwa na MO kama 51% owner wataizidi kete Yanga ya wanachama. Walipoona Manji kakodishiwa kwa 10 years roho zimewauma sana kwani dili lao halitakuwa na impact yoyote kwa timu ya wananchi.
Nionanvyo mimi Yanga iko safe zaidi kwani mali za klabu zinabaki mikononi mwa klabu, kinachokodishwa ni timu na logo pekee, katika kipindi hiki Klabu inaweza kuanzisha timu nyingine hata kwa jina la Young Africans SC Jr na kuipandisha hadi ligi kuu na endapo kutakuwa na mtu mwingine anaihitaji atakodishiwa pia na klabu itaendelea kuanzisha timu nyingine siku hadi siku huku tukiendelea kunyanyua kwapa kwa ushindi wa timu zetu.
Kwa upande wa Simba, MO akichukua hisa 51% then 49% zitamilikiwa na individuals, MO na wenzake wana uhuru wa kuuza hisa zao kwa mtu yeyote mwenye pesa hata kama ni
Makoye Matale wa Yanga. Mali zote za Simba ziko included kwenye hizo hisa hivyo kampuni ikifilisika hatutakuwa na Simba tena labda ianzishwe upya. Endapo kuna hasara itatokea, basi hasara hiyo itakuwa shared among shareholders kwa kiwango cha hisa zao.
Kwa upande wa Yanga, baada ya miaka 10 timu na logo zinarudi mikononi mwa klabu na safari itaendelea. Katika kipindi hiki cha miaka 10 Klabu ya Yanga ifanye utambuzi wa mashabiki wake wote nchi nzima kwa utaratibu watakaouweka. Lengo la kuwatambua ni kuwarasmisha na kuwafanya kuwa wanachama. Endapo idadi ya mashabiki ikifikia 10,000,000 tu kati ya 50,000,000 ya Watanzania wote na kila mmoja akachangia TZS 5,000 tu kwa mwaka, Klabu itakuwa na uwezo wa kujipatia TZS 50bn/= kwa mwaka sawa na TZS 500bn/= kwa miaka 10 ambazo zinaweza kufanya mambo makubwa ndani ya klabu bila hata ya kumtegemea mtu yeyote.
MO na Manji wote ni wale wale tu tofauti hapa ni kila mmoja na approach yake. Kwa hali ilivyo kwa sasa uendeshaji wa vilabu kwa mfumo uliorithiwa tangu zamani umefikia kikomo. Tupende tusipende hawa jamaa ni lazima tuwakabidhi hivi vilabu, tujipange upya.