Mo Dewji aanzisha petition ya kumuomba Rais Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa

Mo Dewji aanzisha petition ya kumuomba Rais Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa

Huu unafiki mkubwa..
Alikuepo hai wakati serikali inatafuta jina..
Iliwahi pendekezwa jina la Mkapa ..watu
Wakajibu Kwa kashfa sana..

Sasa keshakufa ndo muanze kumpa jina
Hata hatajua kumbe mlimpa heshima hiyo..
Huu ni unafiki mkubwa
Kuna majitu huku hadi yanatia kinyaa kwa kujipendekeza
 
Unajulikana kama Mkapa Stadium, hii petition ya nini? Ange-appriciate kama hizi hizi juhudi na sifa njema angezipata akiwa hai.
 
Kweli bwana huyu bwana hakuwa mbinafsi kama mwenzake aliyepeleka international airport machakani
 
Kuna vitu huwa vinapendeza vifanyike watu wakiwa hai. Hakuna jambo linalofurahisha kama kuona watu wanatambua juhudi au mchango wako na kuonesha appreciation wakati bado unaishi.

Wakati huo uwanja unataka kupewa jina, Mkapa aligoma usipewe jina lake. Kimsingi huyo Mkapa pamoja na mazuri na mapungufu yake, alikuwa hapendi sifa za vitu vya nchi kupewa jina lake. Nakumbuka yeye ndio rais aliyegoma picha yake kuwa kwenye noti/sarafu za nchi hii, na pia aligoma jina la Muheshimiwa na kupenda kuitwa zaidi ndugu. Ila zama hizi za kusifia watu, naona mambo hayo yanataka kurudi kwa kasi.
 
Huu unafiki mkubwa..
Alikuepo hai wakati serikali inatafuta jina..
Iliwahi pendekezwa jina la Mkapa ..watu
Wakajibu Kwa kashfa sana..

Sasa keshakufa ndo muanze kumpa jina
Hata hatajua kumbe mlimpa heshima hiyo..
Huu ni unafiki mkubwa
tulifanya makosa na tunatubu na hatutaki tena tukosee tunataka uitwe UWANJA WA MKAPA tosha
 
Kwani si ndiyo kunaitwa kwa Mkapa tokea zamani. Tena watu waliita kwa mchina,serikali ikawaambia unaitwa Mkapa.
Wanayeita kwa Mkapa hawana tofauti na wanaopaita kwa Mchina kwa kuwa majina haya yote ni ya kienyeji na sio yapo Kisheria(majina rasmi) jina rasmi la ule uwanja ni Uwanja wa Taifa.
Aliyetoa jina la kwa Mkapa ni Maoni binafsi ya Dr. Mwakyembe.
 
tulifanya makosa na tunatubu na hatutaki tena tukosee tunataka uitwe UWANJA WA MKAPA tosha

Yeye aligoma akiwa hai maana alijua fika ni kodi za wananchi, huku rais akiwa si mlipa kodi. Wekeni basi na picha ya Magufuli kwenye noti, maana Mkapa ndio rais wa kwanza kugoma kuweka picha yake kwenye fedha za nchi, ili muwe hamjakosea. Watu tunajitahidi kutoka kwenye kusifia watu, twende kwenye sifa za kitaasisi, nyie mnaturudisha kwenye sifa za watu. Hizi ndio tabia zitafanya viongozi wakae madarakani kwa lazima, ili majina yao yatapakae kwenye miradi ya umma. Shubamiit. Siku ikitokea uchafu wao ikataka kuitwa majina yao msikasirike.
 
Wanayeita kwa Mkapa hawana tofauti na wanaopaita kwa Mchina kwa kuwa majina haya yote ni ya kienyeji na sio yapo Kisheria(majina rasmi) jina rasmi la ule uwanja ni Uwanja wa Taifa.
Aliyetoa jina la kwa Mkapa ni Maoni binafsi ya Dr. Mwakyembe.
Bora hata Mwakyembe alitoa hayo maoni Ben akiwa hai. Na kipindi hicho Mo wala hakutokea kusema na kuunga mkono hoja. Leo Ben kafa,Mo eti anatoa petition 😱
 
Yeye aligoma akiwa hai maana alijua fika ni kodi za wananchi, huku rais akiwa si mlipa kodi. Wekeni basi na picha ya Magufuli kwenye noti, maana Mkapa ndio rais wa kwanza kugoma kuweka picha yake kwenye fedha za nchi, ili muwe hamjakosea. Watu tunajitahidi kutoka kwenye kusifia watu, twende kwenye sifa za kitaasisi, nyie mnaturudisha kwenye sifa za watu. Hizi ndio tabia zitafanya viongozi wakae madarakani kwa lazima, ili majina yao yatapakae kwenye miradi ya umma. Shubamiit. Siku ikitokea uchafu wao ikataka kuitwa majina yao msikasirike.
unachanganya hasira na na kutokuelewa mambo, au binadamu mwanadamu mtu ni vitu vinavyokuchanganya sana??
 
Kwani Taifa na Mkapa which is the best- Aliyejenga kaita uwanja wa Taifa leo mbadili ili kuonyesha Taifa ni Ndogo kuliko Mkapa?

Kumuenzi vizuri mzee Mkapa tujenge kitu kingine tuliite jina lake na pia Yale mapendekezo yaliyomo kwenye kitabu chake ikiwepo tume huru ya uchaguzi tufanyie kazi kuanzia uchaguzi huu wa october
 
unachanganya hasira na na kutokuelewa mambo, au binadamu mwanadamu mtu ni vitu vinavyokuchanganya sana??

Kuna hasira gani hapo zaidi ya facts? Akiwa hai aligoma huo uwanja kupewa jina lake. Unapokuja na hoja mfu ya kuwa mlikosea, unamaanisha ndio huna hasira ama?
 
Naunga mkono hoja

Asante Mzee Mkapa

Mifumo yote inayofanya kazi sasa ni kazi zake

ANASTAHILI
 
Naunga mkono hoja.

Ule ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa ambao rais Benjamin Mkapa aliufanya kwa manufaa ya Taifa
Kuna ushujaa gani katika uamuzi huo? Ulikuwa uamuzi mzuri na wa busara, lakini sidhani kama ulikuwa wa kishujaa. Ungekuwa wa kishujaa kama yeye au nchi ingeweza kuathirika kwa namna mmoja kutokana na uamuzi huo au ulikuwa unapingwa na wenye mamlaka wengine lakini akaendelea tu. Haikuwa hivyo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom