MO Dewji afafanua uwekezaji Klabu ya Simba na kuwahakikishia yupo Simba SC haendi popote!

Pale yeye kanunua zote 49% kwa 20 billion ili ule mchakato tuendelee sasa hao wawili wakija watauziwa kwa bei ya soko,Mo amechungulia mbali ndio maana amezishika 49% kwa pamoja kwanza,halafu vitabu vya mahesabu vikiwekwa sawa atapiga pesa ndefu sana.

Unafikiri faida atapata tshs ngapi ishu ikienda DSE? Ata tukimchukia Mo kumbuka kuna msemo MWENYE NACHO UONGEZEWA na tunachomfanyia Mo ni kama kumpiga CHURA teke ni kumuongezea mwendo. Mo ni mfanyabiashara mkubwa unafikiri kanuni au mizengwe akujua kana kwamba aingie kichwa kichwa atoe 20 billion tu. Huyu ndio Angel investor MO na siyo mwenzetu kabisa mkuu.
 
Mo hajanunua hizo hisa. Business mean a lot to buy and sell either on credit or cash but lazima iwe buy and sell.. yy amebid na sio kununua ndio maana hajaweka hela. We unadhani mgogoro huu kiini chake ni nini?
NASISITIZA MO HATOPEWA TIMU AIMILIKI. MANJI ALIKATALIWA KUIKODI ACHILIA MBALI KUINUNUA.
Huwa napata shida sana na mind za watz wengi hasa masuala yanayohitaji brain nzuri. Kwann hatujipi muda wa kutafakari vitu kwa kina? Kama simba mnataka iwe kampuni pelekeni DSE pale ili watu wanunue hizo hisa. Mchakato wa kuifanya kampuni haimfanyi MO na familia yake kuokota dodo chini ya mbuyu. AJITATHIMINI KISHA AFUNGUE MACHO msako anaosakwa tayari umempata na hapo ndio mwanzo wa stress za kibiashara.
The best advice kwa MO ni kuanzisha timu yake ambapo itamchukua angalau miaka 15 kuwa na fan base ya uhakika kidogo. TOFAUTI NA HILO NIKUHAKIKISHIE MO HAWEZI NA HATOWEZA KUIMILIKI SIMBA SPORTS CLUB.
 
Ulikuwa unafaidika na mfumo uliopita?Kwa mapovu haya sio bure ulikuwa na interest!
Wanachama wa Simba wameamua na hakuna kurudi nyuma.Yanga wangefika hatua hii pia hakuna ambaye angeweza kuwazuia ikiwa wanachama majority wanataka mfumo wanaoupenda kuendeleza timu zao.Mfano hai TFF na BMT walijaribu kuwaburuza Yanga kwenye suala la uchaguzi lakini wanachama waliposimama kidete,uchaguzi ulifanyika kwa matakwa ya wanachama walio wengi.Conspiracy theories hazina nafasi kila kitu kipo wazi.Majungu ya vikao vya kahawa hapa sio mahali pake na kujidai kwamba unajua kuliko wanaojua.
 
Kumbe sheria ya wawekezaji watatu ipo toka 2017..Sasa Mwakyembe kwa Nini aliruhusu MO kuendelea na mchakato..nakumbuka matajiri watatu walijitokeza mzee Bakhresa na bilionea wa Uarabuni..wakatoswa Mo akafanya figisu ..kuweni makini kwa Nini MO anaitaka Timu peke yake??Magori sio mtu mzuri refer NSSF
 
Majungu ya kahawa. ETI bilionea wa Arabuni?Hana jina?Bakhresa ana timu yake. Ingekuwa ni ujinga ku bid kwenye timu nyingine.Haikutokea..Sheria zisingemruhusu.Jukwaa hili ni jukwaa la heshima msiligeuze kikao cha wanywa kahawa wasio na kazi.
 
Hahaha sio kwa tambo hizi mtani.

Ama sababu commando kipensi in the house
 
Hahahaaa. Kama nawaona ambavyo mlikuwa mnaombea asirudi.

Kuna sehemu Dada yangu Shunie kanitag na kunitag kwa raha tu alizokuwa nazo kisa uzi unasema Zahera harudi Jangwani. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Aisee huyu jamaa naamini Ndio Moo dewji wenu! Naamini mmesha mlipa malimbikizo na posho zake zote.
 
banda ka biashara kwa maana pana sio hiyo uliyoiweka hapo, nayeye atakuuliza kweli mo anashindwa kuanzisha timu kama azam akawasajiri kina kagere?
Hivi we kwa akili yako ndogo unahisi mo anakosa milioni 700 kununua eneo LA kujanga eneo LA biashara kariakoo??
 
Sio as Vital tena

Sio kwa ku okoteleza uko
Mnataka muendelea kujipigia gori 7 saba kama kawaida yenu
CAF hao ndio changamoto Mtani kwa kutoa ratiba zao bila mpangilio kwani ndio mwanzo wa kila kitu kuvurugika.

Si nimesikia hata nyie Simba Day mumeirudisha nyuma. Au si kweli?
 
CAF hao ndio changamoto Mtani kwa kutoa ratiba zao bila mpangilio kwani ndio mwanzo wa kila kitu kuvurugika.

Si nimesikia hata nyie Simba Day mumeirudisha nyuma. Au si kweli?
Poleni sana. Nilihisi labda gharama.

Nasikia mabingwa wa Tanzania tunaanza ligi na kiporo; kwa sababu ya kima jukumu ya Kitaifa kama ilivo ada.
 
Mbona mshindo anajulikana biashara zake na wala usitake kumuhusisha na mambo ya TISS sisi ni watu wazima hatudanganywi kitoto hivyo.
.
Na Jerry Muro napafahamu hadi kwake hana ubia wala tenda ya kufanya kazi na TISS embu tuache utoto tujadili mambo serious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…