MO Dewji Afanya Mapinduzi! Udhamini wa Vilabu 10 Kwenye NBC Premier League Wazua Gumzo

MO Dewji Afanya Mapinduzi! Udhamini wa Vilabu 10 Kwenye NBC Premier League Wazua Gumzo

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
53,537
Reaction score
133,017
Katika soka la Tanzania, pesa imekuwa silaha kubwa katika kujenga na kuendeleza vilabu vya ligi kuu. Katika misimu miwili iliyopita, GSM, mdhamini wa Yanga SC, alidhamini vilabu zaidi ya saba, akionyesha nguvu yake katika soko la udhamini wa soka.

Lakini sasa, Mohamed Dewji ameibuka na mpango wa kudhamini vilabu 10 kwa kiwango cha mamilioni ya shilingi, hatua inayotikisa ulingo wa soka la ndani!

Kwa makadirio, MO Dewji atawekeza kati ya milioni 300 hadi milioni 500 kwa kila klabu, akitumia udhamini huo kutangaza moja ya bidhaa katika kampuni yake.

Hii siyo tu msaada wa kifedha kwa vilabu, bali ni mabadiliko makubwa yanayoweza kupangua mfumo wa udhamini wa soka nchini.

Swali linabaki: Je, hatua hii itaongeza ushindani mzuri na kuinua soka letu, au itaharibu mfumo wa ligi kwa kuondoa uwiano wa ushindani?

Kwa upande mmoja, udhamini huu unaweza kuwa chachu ya maendeleo, kwani klabu zitapata rasilimali za kuimarisha vikosi vyao, kuajiri wachezaji bora, na kuboresha miundombinu yao. Ushindani unaweza kuongezeka kwa kuwa vilabu vingi vitakuwa na uwezo wa kifedha kushindana kwa haki.

Lakini kwa upande mwingine, uwingi wa pesa kutoka kwa mdhamini mmoja unaweza kuharibu mfumo mzima kwa kutengeneza upendeleo au kuleta utegemezi mkubwa wa vilabu kwa mfadhili mmoja.

Je, GSM ataongeza dau lake ili kudhibiti soko la udhamini, au MO Dewji atakuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwenye mustakabali wa soka letu?

Huu ni wakati wa wadau wa soka kujadili—hatua hii ni neema au changamoto kwa mustakabali wa soka la Tanzania? 🔥⚽
Screenshot_20250504-160149.png
 
Hii ni habari inayotikisa soka la Tanzania! Mzee wa mabadiliko, Mohamed Dewji bilionea namba moja Tanzania.

Ameweka rekodi mpya kwa kudhamini vilabu 10 kwenye msimu ujao wa NBC Premier League. Hatua hii ni zaidi ya udhamini—ni mustakabali mpya wa soka la ndani! 🔥⚽

Inadaiwa hayo yamejiri kufuatia kikao kilichofanyika leo chini ya bodi ya wakurugenzi kikiongozwa na MO Dewj mwenyewe.View attachment 3324443
Sisi ndiyo Simba SC AKA;
JamiiForums1683832807.jpeg

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Malalamiko (Lia lia) SC.
4. Makelele SC.
5. Mipang'ang'a SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyang'au SC.
8. Manyaunyau (Mapaka) SC.
9. Mazumbukuku SC.
10. Mikia SC.
11. Mwakarobo SC.
12. Ngada SC.
13. Zuwena SC.
14. Kufa Kiume SC.
15. Kikanuni SC.
16. Panya Roads SC.
17. Bebwa Bebwa (Mbeleko) SC.
18. Bahasha SC
19. 5imba SC.
20. Ubaya Ubwege SC.
21. Manguruwe SC.
22. Objective Football SC.
23. Mazombi SC.
24. Kolowizard SC.
25. Visingizio(Visababu)SC.
26. Wekundu wa Msimbazi SC.
27. Mbuzi SC.
 
Ko unataka kuniambia M0 kamzidi hela bakresa? Unasema mo tajiri namba moja kwa kigezo kipi?
 
Simba walikuwa wanasema mtu mmoja/kampuni moja kudhamini timu nyingi haifai na inasababisha kupanga matokeo.

Vipi kuhusu hili la MO kudhamini timu kumi?
 
Acheni kumzushia Kanji, Hana pesa ya mchezo

Hata zile bilioni 5 za supercup na mkataba wa bilioni 40 wa M-Bet tulitegemea atasajili vyuma vya bei ghali ila kilichotokea 😂

Muhindi hana pesa ya kugawa gawa hayo mambo ni ya waarabu.
 
Tukubaliane sasa kudhamini zaidi ya timu moja ni sawa au sio sawa?
 
Acha adhamini ila tukikutana kuwalamba mkono ni lazima labda mkimbie tena
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;View attachment 3324446
1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Malalamiko (Lia lia) SC.
4. Makelele SC.
5. Mipang'ang'a SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyang'au SC.
8. Manyaunyau (Mapaka) SC.
9. Mazumbukuku SC.
10. Mikia SC.
11. Mwakarobo SC.
12. Ngada SC.
13. Zuwena SC.
14. Kufa Kiume SC.
15. Kikanuni SC.
16. Panya Roads SC.
17. Bebwa Bebwa (Mbeleko) SC.
18. Bahasha SC
19. 5imba SC.
20. Ubaya Ubwege SC.
21. Manguruwe SC.
22. Objective Football SC.
23. Mazombi SC.
24. Kolowizard SC.
25. Visingizio(Visababu)SC.
26. Wekundu wa Msimbazi SC.
Mbuzl Sc.
 
Shukrani kunikumbusha Mkuu, nilisahau badala Makolokolo wangeleta wachezaji uwanjani walileta mbuzi 🤣
 
Atasaidia sana maana Kuna timu hata basi la kusafiria wanakosa aisee na hakuna kitu kigumu kama timu kukosa pesa ni balaa sana
 
Simba walikuwa wanasema mtu mmoja/kampuni moja kudhamini timu nyingi haifai na inasababisha kupanga matokeo.

Vipi kuhusu hili la MO kudhamini timu kumi?
Walikuwa wanatamani lakini wakaishia kula kwa macho
 
Unafiki ni kitu kibaya sana; kama kitu unakiamini hakipo sawa unatakiwa kikisimamia regardless of time to change it. Sasa baadae ukikitenda unaonekana kumbe ulikuwa mnafiki na mwongo.
 
Back
Top Bottom