Mo Dewji ameonyesha sura yake halisi,wanasimba tutarajie u-Dictator Mo akishakabidhiwa Hisa

Mo Dewji ameonyesha sura yake halisi,wanasimba tutarajie u-Dictator Mo akishakabidhiwa Hisa

Tumeshuhudia juzi tu mfanyabiashara Mohammed Dewji akipitishwa kama mwekezaji atakayepatiwa Hisa 49% za klabu hivyo kuwa mwanachama mwenye hisa nyingi.


Lakini kabla hata hajakabidhiwa timu rasmi tayari tumeshuhudia na kuona sura Halisi ya Mo

1.Kauli aliyotoa Jana Mo kupitia ukurasa wake wa Twitter imeonyesha chembe chembe za u-Dictator ,hapo bado hajaanza kazi rasmi je akianza si ataonea wafanyakazi wa klabu ,


2.Wafanyakazi wa klabu ya simba watakuwa na uoga na furaha kuwaondoka sababu bosi mkuu akikasirika basi ataweza kuwaadabisha na kuwadhalilisha kupitia mitandao ya kijamii

3.Mwalimu Omog kateleza mechi moja lakini mwanahisa huyu kaamua kumtolea povu kupitia Twitter na haikupita masaa 3 viongozi walioshika hatamu simba wakajawa na hofu na kuamua kumtimua mwalimu

Hapa Dewji hajakabidhiwa rasmi Hisa na kuanza kufanya kazi tayari tumeshaona sura yake je akikabidhiwa Hisa si itakuwa hapatoshi hapa mitaa ya msimbazi
Badilikeni sasa hivi timu itaongozwa kwa mujibu wa business plan sio bla bla za vijiweni.
 
Ni hivi , Mo baada ya " kuuziwa " Simba anataka kuweka watu wake kuanzia makocha , wachezaji pamoja na viongozi .
 
Hujui uchungu wa hela wewe, nunua na wewe hisa hata Maji maji Fc halaf uwe unawachekea makocha na wafanyakazi
 
Yaani tim ya simba ikifungwa kocha anafukuzwa, daa kazi kweli kweli!
 
Hiyo inaitwa B2B hakuna masihara. If you can work resign and let others take control seat.
 
Back
Top Bottom