Mo au yeyote anaetaka kuonesha mechi za ligi kuu, afanye yafuatayo:
Atafute timu iliyopo ligi daraja la 1 au la 2, aingie nayo mkataba wa miaka 10 na anunue haki zote za matangazo ya timu hiyo, na mkataba umtake kuonesha mechi zote za timu hiyo (hasa za nyumbani - home) katika ligi yoyote itayoshiriki. Pia anunua haki zote za matangazo za timu hiyo.
Akishakuwa na mkataba na hiyo timu, apambane aipandishe daraja iingie ligi kuu. Hapo sasa ndio kutapokuwa na mgogoro wa kisheria kati yake na AZAM na TFF. Wao kina TFF watasema wana mkataba na Azam na ndie pekee mwenye haki ya kuonesha ligi kuu, yeye atawaambia ana mkataba na timu hiyo unaomtaka kuonesha mechi zote za timu, asipoonesha anakuwa anavunja mkataba wao. Ikumbukwe timu hii haibanwi chochote na mkataba wa TFF na Azam sababu haikuwa katika ligi kuu pindi TFF wanapoingia mkataba na Azam.
Mgogoro huu wa kisheria, utawafanya Azam na huyo mwingine kukaa mezani kujadiliana na hatimae haki za kurusha matangazo zinaweza kugawanywa.