SI KWELI Mo Dewji asifia jezi za Yanga za msimu wa 2024/25

SI KWELI Mo Dewji asifia jezi za Yanga za msimu wa 2024/25

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kwa mara yakwanza Raisi wa heshima wa Simba Mo Dewji akubali yaishe kwenye suala la ku print Jezi Kali hapa Africa.

Kwenye post yake huko mjini Twitter Mo amepost "hakika mtani (Yanga) kwenye suala la jezi una dunia yako"

Je suala hili unalichukuliaje?

IMG_20240729_175121_906.jpg
 
Tunachokijua
Julai 12, 2024, Klabu ya Yanga ilizindua jezi rasmi zitakazotumika kwenye ligi kuu ya NBC msimu wa 2024/25. Uzinduzi wa jezi hizi uliambatana na mambo mengi ikiwemo kufanyika kwa kipindi maalum kwenye televisheni ya Azam.

Baada ya kufanyika kwa uzinduzi huu, baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii zilianza kuchapisha taarifa zinazodai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu ya Simba aliwapongeza Yanga kwa uzinduzi wa jezi nzuri (hapa).

"Hakika mtani kwenye jezi una dunia yako, respect kwako" Mo Dewji.

Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo imetengenezwa, Mohammed Dewji hajaipongeza Yanga kama inavyodaiwa. Badala yake, Julai 25, 2024 kwenye mtandao wa X, bilionea huyo alichapisha ujumbe unaosema "Najiandaa kuvaa jezi mpya ya Simba, Wangapi mmeikubali(hapa)

Julai 28, 2024, ukurasa wa Mtandao wa X wa Mohammed Dewji (@Moodewji) haukuchapisha taarifa yoyote kama inavyoonekana kwenye ujumbe huo.

Aidha, utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwenye mitandao yote ya kijamii haujaleta majibu yanayoashiria au kuonesha kuwa Mo Dewji aliweka ujumbe huo.
Kwa mara yakwanza raisi wa heshima wa Simba mo dewji akubali yaishe kwenye suala la ku print Jezi Kali hapa Africa.....

Kwenye post yake huko mjini Twitter mo amepost " hakika mtani (Yanga) kwenye suala la jezi una dunia Yako"

Je suala hili unalichukuliaje??????View attachment 3054684
Yanga mahayawani. Baada ya Batiki zao Kubuma, wanatafuta marketing strategy ya kuzitoa.

Mnafoji mpaka na Tweets za tajiri ili mpate milestone. Acheni kujitekenya mbwa ninyi.

MO hajaandika kitu kama hicho.
 
Yanga mahayawani. Baada ya Batiki zao Kubuma, wanatafuta marketing strategy ya kuzitoa.

Mnafoji mpaka na Tweets za tajiri ili mpate milestone. Acheni kujitekenya mbwa ninyi.

MO hajaandika kitu kama hicho.
Nenda mjini Twitter...mud kachafuka
 
Back
Top Bottom