OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Nimesikitishwa na mijadala mitandaoni ya kumshutumu Waziri Mwakyembe kwamba ameanzisha utaratibu mpya wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa. Ndugu zangu, si kweli. Utaratibu huu upo tangu 2017 kisheria na sisi Simba tulikubali.
Waziri Mwakyembe alituruhusu SIMBA tuendelee na mwekezaji mmoja. Ndugu WanaSimba Mimi nipo na niko na nyinyi, siendi popote. Na sasa tumeishazungumza na Serekali na mazungumzo ni mazuri. Nawasihi WanaSimba wote twendeni tukaishangilie Timu ya Taifa na tukutane Simba Day tarehe 6. Tulianza vizuri na Serikali na tutamaliza vizuri na Serikali.