Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Rais wa klabu, Mohammed Dewji ametajwa na jarida la Face2Face Africa lenye makao makuu yake jijini New York, Marekani kuwa mmoja kati ya mabilionea wawili ambao wamesaidia kukuza biashara ya mpira wa miguu barani Afrika.
Kutajwa kwa Mo kumetokana uwekezaji na mafanikio ambayo Simba imeyapata tangu alipoanza kufanya uwekezaji katika klabu hii kubwa zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana ni pamoja na kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara nne mfululizo na kucheza mara tano hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF jambo ambalo limeiwezesha klabu kushika nafasi ya saba kwa ubora wa vilabu. Lakini pia Mo amekuwa akitoa pesa za usajili na gharama zingine pindi zinapohitajika.