Mo Dewji Fei Toto anakusubiri

Mo Dewji Fei Toto anakusubiri

Edson Carrington

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2022
Posts
216
Reaction score
636
Salam JF,

" Siwezi sema nina furaha sana nikiwa hapa, ndoto zangu siku moja niwe moja kati ya wachezaji wakubwa Afrika, na naamini hili nitalifanikisha nikiwa timu na bora yenye kushiriki michuano mbalimbali Afrika mara kwa mara, na hii pekee ndio njia ya kuwezesha kipaji changu kuonekana kwa urahisi zaidi Afrika."

Hayo ni maneno ya fundi wa mpira feisal salum almaarufu kama fei toto, akielezea hisia zake za soka toka ajiunge na Azam. Huku akisisitiza kuwa hana furaha kwa kukosa nafasi ya kushiriki michuano mablimbali barani Afrika.

Hii inadhihirisha kuwa Feisal salum anauhitaji wa kuchezea klabu yenye mafanikio ndani na nje ya nchi kwa kushiriki michuano ya Afrika.

Hii imekuwa kama salamu ambayo kijana huyu ameituma Msimbazi, kwani ni vilabu viwili tu ambavyo vinavyoshiriki mara kwa mara michuano hii kwani ni Simba na Yanga, lakini kwa upande wa Yanga haitawezekana juu ya matatizo yaliyotokea.

Hii ni kama salamu kwa Mo Dewji kukiona kipaji hiki kwani ni moja kati ya vipaji adimu zaidi Tanzania. Simba inatakiwa kukaa chini na kijana huyu na kuzungumza nae.

Naiona Combination kali sana kati ya Feisal Salumu na Mcongoman Fabrice Luamba Ngoma.

Kila la kheri Feisal mdogo wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona nilisikia mkataba wa Azam na Yanga katika dili la kumuuza kipengele kimoja wapo Azam haitaruhusiwa kumuuza Simba.
 
Wachezaji wakitoka yanga Viwango Vyao vinakufa RASMI.

Miaka ya Karibuni.
1. Bangala.
2.Feisal.
3. Mayele.
4. Saido.
 
Wachezaji wakitoka yanga Viwango Vyao vinakufa RASMI.

Miaka ya Karibuni.
1. Bangala.
2.Feisal.
3. Mayele.
4. Saido.
Ukimtoa bangala ambaye kiwango chake kilikufa tangu akiwa Yanga hao wengine lini viwango vyao vimekufa? Saidoo Katoka Yanga kashinda tuzo ya mfungaji Bora na Hadi Leo n yegemeo huko ukoloni... Mayele anapata nafasi Hadi timu ya Taifa... Fei n top scorer wa Azam Hadi sasa
 
Ukimtoa bangala ambaye kiwango chake kilikufa tangu akiwa Yanga hao wengine lini viwango vyao vimekufa? Saidoo Katoka Yanga kashinda tuzo ya mfungaji Bora na Hadi Leo n yegemeo huko ukoloni... Mayele anapata nafasi Hadi timu ya Taifa... Fei n top scorer wa Azam Hadi sasa
🙏 Facts vs opinions
 
Back
Top Bottom