Mo dewji hivi unawaonaje mashabiki wa simba?

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
Kila Siku Mo Dewji husema anapata hasara katika Uwekezaji wake binafsi huwa simuelewi cha Msingi ni kuwa mashabiki wa Simba huwa wanamuelewa anapiwaambia hivyo.

Nina imani kwa sasa kila moenda Soka Afrika na Kwingineko anaifahamu Simba na anaifuatilia. Kwa Club kubwa kama Simba Ukipata fursa ya Kuweka Chochote kwenye Jersey yao cha kibiashara utakuwa umeitambulisha bidhaa hiyo au Kampuni lako si Tanzania tu bali hata nje ya mipaka ya Africa. Kitendo kama hicho kinaweza kukupa faida mara kubwa sana.

Angalieni Jersey Ya Simba ina matangazo ya Bidhaa za Mo kila upande inakuwaje anapata Hasara?

Wakati Umefika Sasa Mo aache kuwalagai mashabiki wa Simba kuwa kinachomfanya aifadhili Simba ni Mapenzi yake kwa Club. Aache pia kujifabya anatoa fedha zake kwa Hisani badala ya Win Win Situation.

Brand ya Simba ni kubwa sana na inajitisheleza kuiendesha Club tena Kitajiri kabisa. Anachotaka kutuambia Mo kwa Lugha nyingine ni kwamba Brand ya Simba haimpi Faida kutangaza nayo.

Kama hapati Faida akae pembeni watafutwe watu wanaoweza kuitumia Brand ya Simba kutengeneza Faida yeye kama ana mapenzi tu aendelee kuisapoti Simba akiwa pembeni.

Kama anapata Hasara sio kosa la Simba bali ni kosa la watu wake wa Masoko wanashindwa kuitumia Simba vizuri. Kwa ukubwa Wa Simba wameshavuka level za kuwa Ombaomba brand yao inatosha kabisa….

Yeye anadai mpaka sasa kashatumia Bilioni 50 nje ya Utaratibu na makubaliano. Mimi ni Yanga ila Simba wanapaswa kukaa na Mo wamwambie kuhusu hizi kauli zake zinaififisha brand ya Club na kama amechoka watafute wadhamini wengine.
 
Ngoja vijana wake waje. Wapo humu tayari kumtetea, na kumpigania kwa aina yoyote ile ya mashambulizi dhidi yake.
 
Ndio maana analeta wachezaji wa HOVYO KABISA....

Sawadogo.
Mohamed Ottara.
Okrah.
Banda.
Dejan
Kanute

Mo MJINGA sana
 
Kama anapata hasara aache kutangaza bidhaa zake...
Kama M-bet wanatoa bilioni 3 Kwa mwaka ...yeye na bidhaa zake wanalipia kiasi gani matangazo??

Anadanganya wajinga
 
Simba is Falling Down! Rangi za kufeli Simba ni nyingi, ila Siri ni moja Simba inafeli sababu ya kuzidiwa akili na Rais wa Yanga, Eng Hersi jeshi la mtu mmoja ndo muuaji wa Simba, Dili za wachezaji hatumi mtu, Dili za kocha hatumi mtu anafanya mwenyewe na Kwa Siri! Yanga Ina pesa za kumsajili hata Ronaldo utopoloni hakuna ubahili kama wa kanjibai Mo!

Ona rangi za Simba baada ya kufeli

1. Matola tuachie timu we ndo mchawi wetu , kaachia timu na ugali ila uozo Bado upo pale timu bovu tu
2, Barabara CEO gani demu ndo chanzo tunafeli ondoka kaondoka Simba kukwepa matusi ila Ngoma mbichi tu
3. Kocha Gomez hujui Kufundisha ondoka kaondoka zake ila makombe Bado tu
4 Haji Bugatti is smart kaona Simba kazeeka Hana maajabu hawindi Tena huyo katimkia Utopoloni kwenye raha
5.Diamond Platnumz kaona Simba Kawa Paka huyo katimkia Utopoloni
6 mara stori ni kuwa Simba imejaa wachezaji wazee Onyango, Boko, Kapombe haya Lete vijana Phiri, Banda, Kyombo, Baleke, Sakho Ngoma ila ngoma Bado mbichi
7. Msemaji Ahmed Hana bahati mara Mwenyekiti jina kubwa ila hujawahi kuifunga Yanga unapewa hela na kutuhujumu!
8. Mo Sasa kajaa lawama kibao kwa Kila mtu kumbe tayari Amejua jumba bovu limemuangukia, mashabiki maandazi wa Mauno Fc mayowe yamezidi timu halina hata kombe la mbuzi au kuku , Mo Deeji nae anajitetea sasa ngoma nzito mara ooooh napata hasara mabilioni, si uondoke kama CEO Barabara , mara ooh Simba ilifungwa nikalia hivi Simba Wana mpira Gani kumfunga mwarabu? , Mara oooh hela za usajili zimeliwa na mapanya yako yamejaa Simba ndo tumepata magarasa tu kina Putin na Babu Onyango.

My take: Simba ni watani zetu na kwasasa hamjui boli dawa yeni mtafuteni Eng Hersi awafunde , acheni makasirikio na lawama
 
Simba wenyewe ni Mbumbumbu unafikiri Wana la kufanya?
 
Nyie njaa zinawasumbua.

MO anatusaidia sana.
 
Metl hawajawahi sema wanapata hasara kutangaza Simba. ( Hawa wanamkataba na Simba na wanalipia yale Matangazo) tsh ngapi fuatilia wewe sasa, sio kila kitu utafuniwe.
Ukisikiliza mapato na matumizi, utaona MO kaongezea Billion kadhaa kwenye budget.
Hizi ndizo anazilalamikia, hii ni hasara kweli.

Eti matangazo, nani yupo tayari MO alipie matangazo pekee bila kuongeza chochote?
Wengi wenu mnaongozwa na Chuki, asa sielewi inakusaidia nn kumchukia mtu asiye kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…