Mo Dewji kutenga Bil. 25 kusaidia wabunifu wa AI na Fintech

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,143
Reaction score
1,729
Bilionea Mohammed ‘Mo’ Dewji , ametangaza kuwa yuko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu wenye thamani ya TZS bilioni 25 ili kuchochea mageuzi ya kiteknolojia nchini Tanzania na barani Afrika.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye X Jumatano hii, Dewji ameandika:

“Niko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu (Startup Fund) wenye thamani ya shilingi bilioni 25 kusaidia wana teknolojia, akili bandia (AI), fintech, na wabunifu wa kiteknolojia hapa Tanzania na Afrika. Tutatoa michango na uwekezaji kusaidia vijana wabunifu wenye mawazo ya kubadilisha dunia.
Andaieni mawazo yenu — muda umefika.”

Mfuko huo unatarajiwa kutoa ruzuku, uwekezaji na msaada kwa vijana wabunifu, na hivyo kuimarisha ukuaji wa uchumi wa kidijitali unaochipuka nchini.

Dewji, ambaye ni tajiri namba moja Tanzania na Mwenyekiti Mtendaji wa MeTL Group, ameibadilisha kampuni hiyo kutoka biashara ya dola milioni 30 hadi kuwa kampuni kubwa ya zaidi ya dola bilioni 2.2 inayofanya kazi katika nchi 11.

Akiwa mfadhili na mwanzilishi wa Mo Dewji Foundation, amekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika elimu, afya na upatikanaji wa maji, sambamba na kuwa kinara wa kukuza ubunifu na teknolojia barani Afrika.

Tangazo la mfuko huu linakuja wakati ambao uwekezaji wa kimataifa kwenye AI umeongezeka kwa kasi, ukifikia zaidi ya dola bilioni 200 mwaka 2025, huku matumizi ya AI duniani yakitarajiwa kufikia takribani dola trilioni 1.5.

Barani Afrika, ufadhili wa startup umefikia dola bilioni 2.8 hadi Agosti 2025, na Tanzania ikiendelea kupanua mazingira ya ubunifu kupitia ongezeko la watumiaji wa mtandao, mifumo ya malipo ya kidijitali, na vituo vya ubunifu.

Mfuko huu wa Dewji unatarajiwa kuziba pengo muhimu la mtaji kwa waanzilishi wa AI, fintech na teknolojia nyingine, na kuipa Tanzania nafasi ya uvumbuzi Afrika.
1765425657162.jpg
 
Hivi zile bilioni za nyuma ziko wapi.
Huyu Mo kama anakopea benk nahisi kuendesha maisha yake siku akifa tutawekwa chini ya ulinzi na kampuni ya Majembe auction kila aliyevaa jezi ya simba
 
Bilionea Mohammed ‘Mo’ Dewji , ametangaza kuwa yuko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu wenye thamani ya TZS bilioni 25 ili kuchochea mageuzi ya kiteknolojia nchini Tanzania na barani Afrika.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye X Jumatano hii, Dewji ameandika:

“Niko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu (Startup Fund) wenye thamani ya shilingi bilioni 25 kusaidia wana teknolojia, akili bandia (AI), fintech, na wabunifu wa kiteknolojia hapa Tanzania na Afrika. Tutatoa michango na uwekezaji kusaidia vijana wabunifu wenye mawazo ya kubadilisha dunia.
Andaieni mawazo yenu — muda umefika.”

Mfuko huo unatarajiwa kutoa ruzuku, uwekezaji na msaada kwa vijana wabunifu, na hivyo kuimarisha ukuaji wa uchumi wa kidijitali unaochipuka nchini.

Dewji, ambaye ni tajiri namba moja Tanzania na Mwenyekiti Mtendaji wa MeTL Group, ameibadilisha kampuni hiyo kutoka biashara ya dola milioni 30 hadi kuwa kampuni kubwa ya zaidi ya dola bilioni 2.2 inayofanya kazi katika nchi 11.

Akiwa mfadhili na mwanzilishi wa Mo Dewji Foundation, amekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika elimu, afya na upatikanaji wa maji, sambamba na kuwa kinara wa kukuza ubunifu na teknolojia barani Afrika.

Tangazo la mfuko huu linakuja wakati ambao uwekezaji wa kimataifa kwenye AI umeongezeka kwa kasi, ukifikia zaidi ya dola bilioni 200 mwaka 2025, huku matumizi ya AI duniani yakitarajiwa kufikia takribani dola trilioni 1.5.

Barani Afrika, ufadhili wa startup umefikia dola bilioni 2.8 hadi Agosti 2025, na Tanzania ikiendelea kupanua mazingira ya ubunifu kupitia ongezeko la watumiaji wa mtandao, mifumo ya malipo ya kidijitali, na vituo vya ubunifu.

Mfuko huu wa Dewji unatarajiwa kuziba pengo muhimu la mtaji kwa waanzilishi wa AI, fintech na teknolojia nyingine, na kuipa Tanzania nafasi ya uvumbuzi Afrika.
View attachment 3514137

Huyu ni tapeli, kawatapeli Simba na Bilioni 20 hadi leo wana Simba hawana hamu
 
Huo ni Uongaoo Banaaaa! Uongoooo hapana!!

Anataka Bizness ideaz apite nazo....Hapo inabidi ukiandika ukasajili kabisa COSOTA ili akiiba tu unadeal nae perpendicular
kabla ya kufanya pitch ya idea yako unakuwa ushaimiliki kisheria. Kuna watu walianzisha pitch deck, baada ya wiki uunakuta idea yako uliyoiwasilisha iko mtaani ishaanza kuingizwa sokoni
 
Yeah ,hawa matajiri wana mipunga mingi na wanatumia watu kupata bizness ideas na huwa wanaanzisha vitu kama hivyo wapate idea bure ,sasa kuwakomesha ni kwenda kuisajili kabisa uwe na hakimiliki(Copyright) kabisa then ndiyo unampelekea! Wajifunze kwenye Mogogoro wa Azam Media na mwenye idea ya VITASA OG.
 
Bilionea Mohammed ‘Mo’ Dewji , ametangaza kuwa yuko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu wenye thamani ya TZS bilioni 25 ili kuchochea mageuzi ya kiteknolojia nchini Tanzania na barani Afrika.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye X Jumatano hii, Dewji ameandika:

“Niko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu (Startup Fund) wenye thamani ya shilingi bilioni 25 kusaidia wana teknolojia, akili bandia (AI), fintech, na wabunifu wa kiteknolojia hapa Tanzania na Afrika. Tutatoa michango na uwekezaji kusaidia vijana wabunifu wenye mawazo ya kubadilisha dunia.
Andaieni mawazo yenu — muda umefika.”

Mfuko huo unatarajiwa kutoa ruzuku, uwekezaji na msaada kwa vijana wabunifu, na hivyo kuimarisha ukuaji wa uchumi wa kidijitali unaochipuka nchini.

Dewji, ambaye ni tajiri namba moja Tanzania na Mwenyekiti Mtendaji wa MeTL Group, ameibadilisha kampuni hiyo kutoka biashara ya dola milioni 30 hadi kuwa kampuni kubwa ya zaidi ya dola bilioni 2.2 inayofanya kazi katika nchi 11.

Akiwa mfadhili na mwanzilishi wa Mo Dewji Foundation, amekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika elimu, afya na upatikanaji wa maji, sambamba na kuwa kinara wa kukuza ubunifu na teknolojia barani Afrika.

Tangazo la mfuko huu linakuja wakati ambao uwekezaji wa kimataifa kwenye AI umeongezeka kwa kasi, ukifikia zaidi ya dola bilioni 200 mwaka 2025, huku matumizi ya AI duniani yakitarajiwa kufikia takribani dola trilioni 1.5.

Barani Afrika, ufadhili wa startup umefikia dola bilioni 2.8 hadi Agosti 2025, na Tanzania ikiendelea kupanua mazingira ya ubunifu kupitia ongezeko la watumiaji wa mtandao, mifumo ya malipo ya kidijitali, na vituo vya ubunifu.

Mfuko huu wa Dewji unatarajiwa kuziba pengo muhimu la mtaji kwa waanzilishi wa AI, fintech na teknolojia nyingine, na kuipa Tanzania nafasi ya uvumbuzi Afrika.
View attachment 3514137
Sisi watanzania ni wajinga sana huyu alivyokuwa mbunge singida hakutatua shida yeyote. Kifupi huyu anatambua Tanzania sio kwao amekuja kuchuma tu. Huyu ni mgujirati muislamu. Angekuwa India caste system isingemruhusu kutengeneza hata milion moja kwa mwaka. Tajiri namba moja Tanzania scholarships zake ni kusomesha watanzania UDSM. Are we serious ? Na mashamba yote ya katani anamiliki yeye. We have a long way to go as a country.
 
Naunga mkono juhudi za MO Dewji katika kufikiria kuwekeza ndani ya nchi yake ambayo juzi imetimiza umri wa miaka 64 ya uhuru.

Kama ni binadamu basi ni yule ambae afaidi matunda ya kazi zake baada ya kustaafu kazi au bado yuko azidi kuhangaikia mlo wa siku agalau mlo mmoja.

Mo aanze na Singida mkoa alikozaliwa aubadilishe uwe mkoa Satelite uwe na mambo yote anoyawaza.

Akiwa mfadhili na mwanzilishi wa Mo Dewji Foundation, awe mstari wa mbele kuwekeza katika elimu, afya na upatikanaji wa maji, sambamba na kuwa kinara wa kukuza ubunifu na teknolojia nchini Tanzania kwa kuanza na mkoa wa Singida.

Mkoa wa Singida ukiwa mkoa bora kwa masuala yote elimu, afya, Teknolojia, utachukuliwa kuwa ni pilot project na serikali itautumia kama kigezo cha kuendeleza mikoa mingine iloyo na maisha duni.

Akifanya hivyo ataeleweka uzuri sana.
 
Huo ni Uongaoo Banaaaa! Uongoooo hapana!!

Anataka Bizness ideaz apite nazo....Hapo inabidi ukiandika ukasajili kabisa COSOTA ili akiiba tu unadeal nae perpendicular
Hamna cha bure lazima umgawie umiliki(ownership stake) kidogo ili awekeze kwako. Ipo wazi.

Lakini usipoenda kwake utaenda kwa wengine tu. Startups zinafanikiwa kwa kukua haraka. Ubunifu sio tija, tija ni utendaji wa kasi. Ulichobuni leo usipokifanyia kazi mwingine atakifanyia kesho.

Kwanza mpaka ubuni kitu kipya sana kinachoweza kupewa patent ni ngumu. Kuna vigezo vyake. Wabunifu wengi hubuni matumizi mapya ya teknolojia iliyopo(soft tech) na siyo kubuni teknolojia mpya kabisa(hard tech).
 
Sisi watanzania ni wajinga sana huyu alivyokuwa mbunge singida hakutatua shida yeyote. Kifupi huyu anatambua Tanzania sio kwao amekuja kuchuma tu. Huyu ni mgujirati muislamu. Angekuwa India caste system isingemruhusu kutengeneza hata milion moja kwa mwaka. Tajiri namba moja Tanzania scholarships zake ni kusomesha watanzania UDSM. Are we serious ? Na mashamba yote ya katani anamiliki yeye. We have a long way to go as a country.
Kwani kazi ya Mbunge ni kupeleka Barabara , maji, bungeni kwake ?
 
Back
Top Bottom