Mo Dewji: Nimetoa 1.5b za usajili lakini haziendani na wachezaji waliosajiliwa

Mo Dewji: Nimetoa 1.5b za usajili lakini haziendani na wachezaji waliosajiliwa

Kudadadeki,

Yaani Mo ka' Mama wa Kambo! Yaani anakupa ugali na masemango juu...

-Hapa ukitumwa hutaki lakini ukisia ugali tayari ndo wa kwanza...

-Yaani we mtoto mroho kweli, hata kutafuna chakula hutafuni, unasukumia tu ka' mzigo wa mavi kwenye choo cha shimo

-Lione linavyokombeleza mboga utadhani amenenunua shangazi yako

-Yaani unakula kama unafukuzwa. aaaaaargh!!

-Hata kunywa maji hutaki kwa sababu unaogopa utashiba haraka

-We mtoto mitonge yote hiyo, ikikukwama shingono nani unataka umsumbue?

-Liangalie linavyomwagika mijasho wakati wa kula utadhani mbeba zege

Dah! Blaza unazingua bhana!! CEO si alikuwa Da' Barbara lakini?! Ina maana ilikuwa hesabu yote wanayompelekea yeye anapitisha tu wakati tuliambiwa da' Barbara ni Kiboko ya Wapigaji pale Ukoloni Street?!
Kama upo makini utaona hii sio mara ya kwanza Mo kutoa kauli kama hii

Huko nyuma aliwahi kusema hivi hivi na Uto wengi walichukulia kama fursa ya wao kuonesha chuki zao.

But soon or later Hersi alikuja kuyarudia maneno yale yale na hakukuwa na kunguni yeyote kutoka Uto aliyepinga kauli hiyo.

Fact ni moja ambayo ameisema na sijaona mtu yeyote akijisumbua kuangaika nayo. Sijaona yeyote ambaye ameifikiria kauli ya Mo aliyoitoa kama mfano kuwa hakuna mwekezaji ambaye aliwahi kudumu kwa kipindi cha miaka 6 kama alivyofanya yeye

Na wengi wamejikuta wakifirisika, mfano mzuri angalieni Vodacom walivyojitoa tu kwenye ligi yetu sababu ilikuwa nini?

Chukua sababu yao halafu thaminisha na kile walichokuwa wanakitoa kama kina relate.

Vodacom walikuwa wanatoa 80M lakini walishindwa kuendelea kwasababu ya pesa ambayo walikuwa wanaitoa na kile wanachokipata kilikuwa hakina uwiano mzuri
 
Mchezo huu wa soka mimi nashindwa kabisa kuelewa kwa sababu hata Ulaya vilabu vinaendeshwa kwa mikopo tuu na inaonekana kupata faida ni kazi sana.

Sasa hata hapa vilabu vya Yanga na Simba vinatumia fedha nyingi sana lakini hakuna mrejesho wa hizo fedha na ndio maana piga ua lazima wawe na wafadhili.

Muda ule dikteta Magufuli alipomsondeka ndani Manji ona Yanga ilivyodorora hadi wakawa wanatembeza bakuli.

Vilabu kupata faida hasa katika nchi shithole kama hizi za kiafrika ni ngumu sana na ndio maana vilabu vingi vya kiafrika kama Canon Yaounde, Union Douala, Tonerre Kalala (Cameroon); Hafia Conakry (Guinea); Africa Sport, Stella Abidjan, Asec Mimosa (Ivory Coast); Hearts of Oak, Asante Kotoko, Obuasi Goldfield (Ghana); Djoliba Athletic Bamako (Mali); Enugu Rangers, Icc Shooting Stars, Enyimba, Stationery Stores (Nigeria); AS Bilima, TP Mazembe, His Majesty Sanga Balende (Congo DR); Cara Renaissance de Aglon (Congo Rep); Mufulira Wonderers, Nkana Red Devils, Kabwe Warriors, Green Buffaloes (Zambia); Gor Mahia, AFC Leopards (Kenya); KCC, Sports Club Villa, Express (Uganda); Agaza Lome (Togo); Pan Africa (Tanzania) nk, nk vimekufa na vingine vimebaki majina tu, vilabu ambavyo enzi hizo vilikuwa ni 🔥 wa kuotea mbali.
 
Mo anapaswa aweke sawa kauli yake.:-
1. Hiyo 1.5B ni usajili tu wa hao wachezaji wapya au ni pamoja na mishahara yao.
2. Kama ni usajil wa wachezaji wapya pamoja na mishahara yao itakuwa imetumika vizuri.
3. Kama ni usajili tu bila kujumuisha misahara ya hao wachezaji wapya basi kuna upigaji mkubwa sana pale Simba.
4. 1.5B kwa usajili tu bila mishahara hapa Afrika kama Simba ingekuwa na mkurugenzi mzuri wa ufundi au timu nzuri ya "scouting" ingepata wachezaji wakali watatu mpaka wanne ambao wangekuwa uti wa mgongo kwenye timu yao ukichanganya na wengine waliopo basi Simba ingetisha sana Afrika zaidi ya inavyotisha sasa.
 
Sass hapo kamsimanga Nani uto?

Mbona kamjibu mwandishi kutokana na swali alilouliza. Alafu mambo ya Simba utopolo Ndiyo huwa mnateseka sijui hiki kisokolokwinyo lini kitawaisha!!
Vice versa is turuu
 
Kama katoa 1.5b Kwa ajili ya usajili, ilikuwaje tulishindwa kumsajili manzoki Kwa 300mil? Yaani hapo kwenye 1.5b ukitoa iyo 300m si bado unabakiza 1.2b?
Thamani nzima ya manzoki ilitakiwa iwe Ml 900, ndipo Simba ilipochemka hapo
Vipers Club wakitaka $200,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Ml 250,
Manzoki nae kusaini mkataba alikuwa anavuta $ 200,000 Simba waliona Viper wanahitaji pesa nyingi ya kuvunja mkataba.
 
Kwa iipofika Simba na usajiri wa Tsh B.1.5 ni pesa ndogo ya kawaida sana haswa pale utakapotaka kusajiri wachezaji zaidi ya watano wa kigeni,
 
Back
Top Bottom