Mchezo huu wa soka mimi nashindwa kabisa kuelewa kwa sababu hata Ulaya vilabu vinaendeshwa kwa mikopo tuu na inaonekana kupata faida ni kazi sana.
Sasa hata hapa vilabu vya Yanga na Simba vinatumia fedha nyingi sana lakini hakuna mrejesho wa hizo fedha na ndio maana piga ua lazima wawe na wafadhili.
Muda ule dikteta Magufuli alipomsondeka ndani Manji ona Yanga ilivyodorora hadi wakawa wanatembeza bakuli.
Vilabu kupata faida hasa katika nchi shithole kama hizi za kiafrika ni ngumu sana na ndio maana vilabu vingi vya kiafrika kama Canon Yaounde, Union Douala, Tonerre Kalala (Cameroon); Hafia Conakry (Guinea); Africa Sport, Stella Abidjan, Asec Mimosa (Ivory Coast); Hearts of Oak, Asante Kotoko, Obuasi Goldfield (Ghana); Djoliba Athletic Bamako (Mali); Enugu Rangers, Icc Shooting Stars, Enyimba, Stationery Stores (Nigeria); AS Bilima, TP Mazembe, His Majesty Sanga Balende (Congo DR); Cara Renaissance de Aglon (Congo Rep); Mufulira Wonderers, Nkana Red Devils, Kabwe Warriors, Green Buffaloes (Zambia); Gor Mahia, AFC Leopards (Kenya); KCC, Sports Club Villa, Express (Uganda); Agaza Lome (Togo); Pan Africa (Tanzania) nk, nk vimekufa na vingine vimebaki majina tu, vilabu ambavyo enzi hizo vilikuwa ni ๐ฅ wa kuotea mbali.