MO Dewji: Tuzo ya goli bora la CAF 2022 limeleta heshima ya kipekee kwa Simba SC na Tanzania

MO Dewji: Tuzo ya goli bora la CAF 2022 limeleta heshima ya kipekee kwa Simba SC na Tanzania

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mohammed Dewji MO, ameleza furaha yake huku akimpongeza Nyota Pape Ousmane Sakho baada ya kushinda Tuzo ya goli bora la CAF 2022 mjini wa Rabat nchini Morocco

"Wanasimba na Watanzania tunajivunia mafanikio yako Pape Ousmane Sakho.

Hongera kwa kushinda Tuzo ya goli bora la CAF 2022 na asante kwa kuleta heshima ya kipekee kwa Simba SC na Tanzania.

Tuzo hii imezidi kuonyesha namna gani Simba SC ni Timu Kubwa na ina wachezaji wenye viwango". Dewji MO.
 
Ni heshima ya kipekee kwa Simba na Tanzania
20220722_080337.jpg
 
Hongera sana kwake.

Alistahili, magoli ya hivyo ni machache sana
Acrobatic ni goli matata sana huwa huwezi kushindanisha mabao mengine.

Zouhair El Moutaraji

Gabadinho Mhango

Ni mabao mazuri sana, wameyafunga hawa kwa mbali na ujuzi sana, lakini Acrobatic Pape Ousmane Sakho ilikuwa haina mpinzani yaani.
 
Mi mwenyewe ninefurahi sana...
Msimu huu tukaze zaidi
Ila
Kagere
Mugalu
Mhilu
Hapana aiseee

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Usajili unaendelea mkuu, Mhilu kuna tetesi tayari amerejea kwa mkopo kunako timu yake Kagera Sugar

Kagere na Mugalu lolote linaweza kutokea licha ya kwenda kwenye PRE-SEASON
 
Ngoja tuone Mayele nae huenda akatetema kwa kuweka goli matata kama hilo la Sakho
 
Unaweza kufunga mabao mengi ukapewa Ng'ombe demigod

Lakini unaweza kufunga bao moja tu ukapewa Tuzo, ukaheshimisha klabu na nchi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Pettymagambo View attachment 2299599
Mheshimu Mayele boss maana alifunga magoli mawili ya staili hiyo na moja likawa goli Bora NBC premier league. Sakho apongezwe kwa kushinda tuzo kubwa Africa lakini haina maana ya kumdharau Mayele.
 
Back
Top Bottom