Mada nyingi zimeshatolewa hapa jukwaani zikielezea hatari za utumiaji wa kupindukia wa vinywaji vya kusisimua, kwa lugha ya kigeni “Energy Drinks” hususan kwa vijana.
Leo ningependa tujadili athari kubwa inayosababishwa na chupa zilizotumika za kinywaji hiki kutokana na kuzagaa ovyo kwenye majalala, lakini zaidi hasa kwenye mifereji na mitaro iliyoko pemebezoni mwa barabara zetu katika miji iliyo mingi hapa nchini. Chupa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa sana si uchafuzi tu wa mazingira bali pia uzibaji mifereji ya kupitishia maji machafu.
Hii ina maana kinywaji hiki ni “double hazard” kutokana na athari yake kwa afya na mazingira.
Ushauri wangu ni kwa wizara mbili zinazohusika na afya na mazingira kujielekeza kwenye hatua za kukabiliana na athari nilizozitaja.