True story nina rafiki wawili kwa wakati tofauti tofauti wamejaribu kuingia kwenye Telecommunication market ya Tanzania na mpaka sasa kesi zao ziko mahakamani.
Mmoja alifanya partnership ya 30% + 5% kwa kigogo na 65% ya non Tanzanian investor ambao walikuwa na Know How zote necessary kurun biz under very low cost and effective management structure. Walifanikiwa kila mahala kwenye kupata leseni lakini mgogoro ukawa kwamba issue yao ika vuja kwenye voda, then wakapewa channel au frequency ambazo wasingeweza kufanya chochote. Waka file lawsuit mahakamani, na mpaka leo kesi ipo hai.
Wengine walitoka Seattle, hawa niliongea nao mwenyewe 2008 walikuwa wanataka business developer in African market. A small company ambayo ina run kama Cricket, boost au simple mobile. They don't own mitambo wala nini, walipofika bongo wakutana na kikwazo kwamba wao ni kampuni fake. Ukweli kampuni hiyo ni popular Seattle, basi wakakwamia hapo.
Tanzania bado Vodacom inatawala sana nani aingie kwenye market na nani asiingie.