nyakahanga
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 240
- 65
Heshima wakuu.
Ni matumaini yangu kuwa hapa ndani kuna watu wanaohusika na vitengo ama taasisi nilizozitaja katika Subject ya post hii.
Mnamo tarehe 14/9/2014, tovuti ya NACTE ilitoa majina yasiyopungua 4000 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ngazi ya stashahada ya juu ya ualimu (kwa masomo ya sayansi na hisabati) katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa taarifa za uhakika ni kwamba majina hayo yanajumuisha waombaji walioomba moja kwa moja kupitia chuo kikuu cha Dodoma na wale waliotuma maombi yao kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi (MoEVT).
Mkanganyiko uliojitokeza ni kwamba, katika tangazo la wizara ya elimu juu ya mafunzo haya la tarehe lilibainisha kuwa waombaji wote watakaochaguliwa watapewa ufadhili na serikali (?wizara) ili kuwawezesha katika mafunzo hayo yaani kwa njia ya ruzuku (kwa wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne) na mkopo kwa wale waliopata ufaulu wa daraja la pili na la tatu.
Tangazo liko hapa (tangazo la pili la kuhusu diploma) TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
Sambamba na hilo, bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) nao walifungua dirisha la maombi ya mkopo kwa wanafunzi wa aina hiyo ya mafunzo (wale watakaochaguliwa UDOM) kwa mwaka wa masomo 2014/2015, dirisha lililofunguliwa mwezi agost mwanzoni na kufungwa tarehe 10 September mwaka huu.
Tangazo liko hapa GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF LOANS TO STUDENTS ADMITTED TO PURSUE DIPLOMAS IN SCIENCE/MATHEMATICS WITH EDUCATION UNDER SPECIAL PROGRAMME FOR 2014/2015 ACADEMIC YEAR.
Hoja yangu ya msingi ambayo nazitaka taasisi tajwa hapo juu zilete majibu hasa MoEVT na HESLB ni;
Je tangazo la kuomba mkopo wa mafunzo hayo lililotolewa na HESLB linawahusu wanafunzi (waombaji) wote waliochaguliwa na mafunzo hayo katika chuo kikuu cha Dodoma (wale walioomba moja kwa moja kupitia chuo na walioomba kupitia wizara ya elimu)? Au liliwahusu walioomba kupitia chuo pekee?
Mashiko ya hoja yangu ni kwamba, mbona majina ya walochaguliwa na mafunzo hayo yametolewa tarehe 14 September, siku nne baada ya deadline? Je hao walioomba kupitia wizara wangejuaje kuwa watachaguliwa UDOM hivyo waombe mkopo kabla ya selection?
Na je kuna mpango gani wa kuwasaidia vijana hawa ambao hawajaomba mkopo kupitia HESLB ( naamini sio wote wataweza maisha ya chuo kikuu cha dodoma bila mkopo hata wakiweza kulipa ada ya kozi zao). Naomba wahusika wapite huku watoe majibu juu ya hili.
Karibuni kwa maoni.
Imeandikwa na Matthew Wejja, Mtanzania wa kawaida.