MoEVT, NACTE, HESLB na UDOM tunaomba ufafanuzi

MoEVT, NACTE, HESLB na UDOM tunaomba ufafanuzi

nyakahanga

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Posts
240
Reaction score
65
Heshima wakuu.

Ni matumaini yangu kuwa hapa ndani kuna watu wanaohusika na vitengo ama taasisi nilizozitaja katika Subject ya post hii.

Mnamo tarehe 14/9/2014, tovuti ya NACTE ilitoa majina yasiyopungua 4000 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ngazi ya stashahada ya juu ya ualimu (kwa masomo ya sayansi na hisabati) katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa taarifa za uhakika ni kwamba majina hayo yanajumuisha waombaji walioomba moja kwa moja kupitia chuo kikuu cha Dodoma na wale waliotuma maombi yao kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi (MoEVT).

Mkanganyiko uliojitokeza ni kwamba, katika tangazo la wizara ya elimu juu ya mafunzo haya la tarehe lilibainisha kuwa waombaji wote watakaochaguliwa watapewa ufadhili na serikali (?wizara) ili kuwawezesha katika mafunzo hayo yaani kwa njia ya ruzuku (kwa wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne) na mkopo kwa wale waliopata ufaulu wa daraja la pili na la tatu.

Tangazo liko hapa (tangazo la pili la kuhusu diploma) TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

Sambamba na hilo, bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) nao walifungua dirisha la maombi ya mkopo kwa wanafunzi wa aina hiyo ya mafunzo (wale watakaochaguliwa UDOM) kwa mwaka wa masomo 2014/2015, dirisha lililofunguliwa mwezi agost mwanzoni na kufungwa tarehe 10 September mwaka huu.

Tangazo liko hapa GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF LOANS TO STUDENTS ADMITTED TO PURSUE DIPLOMAS IN SCIENCE/MATHEMATICS WITH EDUCATION UNDER SPECIAL PROGRAMME FOR 2014/2015 ACADEMIC YEAR.

Hoja yangu ya msingi ambayo nazitaka taasisi tajwa hapo juu zilete majibu hasa MoEVT na HESLB ni;

Je tangazo la kuomba mkopo wa mafunzo hayo lililotolewa na HESLB linawahusu wanafunzi (waombaji) wote waliochaguliwa na mafunzo hayo katika chuo kikuu cha Dodoma (wale walioomba moja kwa moja kupitia chuo na walioomba kupitia wizara ya elimu)? Au liliwahusu walioomba kupitia chuo pekee?

Mashiko ya hoja yangu ni kwamba, mbona majina ya walochaguliwa na mafunzo hayo yametolewa tarehe 14 September, siku nne baada ya deadline? Je hao walioomba kupitia wizara wangejuaje kuwa watachaguliwa UDOM hivyo waombe mkopo kabla ya selection?

Na je kuna mpango gani wa kuwasaidia vijana hawa ambao hawajaomba mkopo kupitia HESLB ( naamini sio wote wataweza maisha ya chuo kikuu cha dodoma bila mkopo hata wakiweza kulipa ada ya kozi zao). Naomba wahusika wapite huku watoe majibu juu ya hili.

Karibuni kwa maoni.

Imeandikwa na Matthew Wejja, Mtanzania wa kawaida.
 
Ninalolijua mm ni kwamba waandaaji wa hii mifumo yote ambayo hatuna budi kuifuata wametutangulia kwenda shule.

Nikiwa na maana kwamba walijua huo mkanganyiko uliokupata na kuzusha maswali mengi yasiyo na majibu vichwani mwa wengi hasa wahusika.

Jambo la msingi ni kusubili ni nini watakifatisha baada ya hicho kilicho kukanganya.
 
Jamani mie nilijaribu kulifuatilia hili kwa taasisi husika na majibu niliyopewa ni kama hivi.

1. waombaji walitakiwa kufanya maombi ya mkopo kabla ya dirisha kufungwa lkn kwa sababu wengi hawakuwa wakijua hili hawakuomba so walioomba ni watu wachache tu.

2. kutokana na sababu ya kwanza nacte wakaamua kutoa majina ya walio chaguliwa ili wajijue wafanye mchakato wa kuomba.

3. kwa sababu muda ulishapita na walioomba ni wachache wameahidi kufungua tena kuanzia wiki ijayo kuwaruhusu wale ambao hawakuomba wafanye hivyo.

So tuzubiri tuone litakapofunguliwa tuchangamke kabla halijafungwa tena.
 
Heshima wakuu,
Ni matumaini yangu kuwa hapa ndani kuna watu wanaohusika na vitengo ama taasisi nilizozitaja katika Subject ya post hii.
Mnamo tarehe 14/9/2014, tovuti ya NACTE ilitoa majina yasiyopungua 4000 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ngazi ya stashahada ya juu ya ualimu (kwa masomo ya sayansi na hisabati) katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa taarifa za uhakika ni kwamba majina hayo yanajumuisha waombaji walioomba moja kwa moja kupitia chuo kikuu cha Dodoma na wale waliotuma maombi yao kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi (MoEVT).
Mkanganyiko uliojitokeza ni kwamba, katika tangazo la wizara ya elimu juu ya mafunzo haya la tarehe lilibainisha kuwa waombaji wote watakaochaguliwa watapewa ufadhili na serikali (?wizara) ili kuwawezesha katika mafunzo hayo yaani kwa njia ya ruzuku (kwa wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne) na mkopo kwa wale waliopata ufaulu wa daraja la pili na la tatu. Tangazo liko hapa (tangazo la pili la kuhusu diploma) TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
Sambamba na hilo, bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) nao walifungua dirisha la maombi ya mkopo kwa wanafunzi wa aina hiyo ya mafunzo (wale watakaochaguliwa UDOM) kwa mwaka wa masomo 2014/2015, dirisha lililofunguliwa mwezi agost mwanzoni na kufungwa tarehe 10 September mwaka huu. Tangazo liko hapa GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF LOANS TO STUDENTS ADMITTED TO PURSUE DIPLOMAS IN SCIENCE/MATHEMATICS WITH EDUCATION UNDER SPECIAL PROGRAMME FOR 2014/2015 ACADEMIC YEAR

Hoja yangu ya msingi ambayo nazitaka taasisi tajwa hapo juu zilete majibu hasa MoEVT na HESLB ni; Je tangazo la kuomba mkopo wa mafunzo hayo lililotolewa na HESLB linawahusu wanafunzi (waombaji) wote waliochaguliwa na mafunzo hayo katika chuo kikuu cha Dodoma (wale walioomba moja kwa moja kupitia chuo na walioomba kupitia wizara ya elimu)? Au liliwahusu walioomba kupitia chuo pekee?
Mashiko ya hoja yangu ni kwamba, mbona majina ya walochaguliwa na mafunzo hayo yametolewa tarehe 14 September, siku nne baada ya deadline? Je hao walioomba kupitia wizara wangejuaje kuwa watachaguliwa UDOM hivyo waombe mkopo kabla ya selection? Na je kuna mpango gani wa kuwasaidia vijana hawa ambao hawajaomba mkopo kupitia HESLB ( naamini sio wote wataweza maisha ya chuo kikuu cha dodoma bila mkopo hata wakiweza kulipa ada ya kozi zao). Naomba wahusika wapite huku watoe majibu juu ya hili.
Karibuni kwa maoni.

Imeandikwa na Matthew Wejja, Mtanzania wa kawaida.

Kwanza nikurekebishe kidogo, wanaoenda UDOM siyo advanced diploma, bali ni diploma ya kawaida na waliochaguliwa ni wale wa form four tu.

Wale walioomba kupitia wizara ya elimu kwa form four wote wamepangwa dipoloma ya elimu ya awali na msingi na wale form sx wamepangwa advanced diploma katika vyuo vya ualimu vya serikali.

Hao waliopangwa UDOM waliomba kupitia nacte na chuoni moja kwa moja, na pia walipewa taarifa mapema kwamba waombe mkopo.

Hivyo kuchelewa kuomba kwa kusubiri majina yatoke ni uzembe wao au wengine kutopata taarifa kwa kuwa ni jambo jipya. Ni sawa tu na tcu ukiomba na mkopo unaomba pamoja bila kusubiri kama utapata chuo.

Pamoja na hilo kwa hawa watawekewa utaratibu wao kupitia chuo wa kuwawezesha kupata mikopo ili waweze kumudu masomo yao.

Ondoa shaka ndugu.
 
Kwanza nikurekebishe kidogo, wanaoenda UDOM siyo advanced diploma, bali ni diploma ya kawaida na waliochaguliwa ni wale wa form four tu. Wale walioomba kupitia wizara ya elimu kwa form four wote wamepangwa dipoloma ya elimu ya awali na msingi na wale form sx wamepangwa advanced diploma katika vyuo vya ualimu vya serikali.
Hao waliopangwa UDOM waliomba kupitia nacte na chuoni moja kwa moja, na pia walipewa taarifa mapema kwamba waombe mkopo. Hivyo kuchelewa kuomba kwa kusubiri majina yatoke ni uzembe wao au wengine kutopata taarifa kwa kuwa ni jambo jipya. Ni sawa tu na tcu ukiomba na mkopo unaomba pamoja bila kusubiri kama utapata chuo.
Pamoja na hilo kwa hawa watawekewa utaratibu wao kupitia chuo wa kuwawezesha kupata mikopo ili waweze kumudu masomo yao. Ondoa shaka ndugu.

Asante kwa marekebisho mkuu,
Naomba pia nikurekebishe kuwa wapo wengi tu walioandika barua zao za maombi kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na siyo kupitia NACTE na wamechaguliwa University of Dodoma (nadhani sababu ni ufaulu wao mzuri wa masomo ya sayansi).

Tangazo la wizara ya elimu juu ya mafunzo haya lilibainisha vyuo vitano maalumu kwa mafunzo hayo, majina yalitoka NACTE na wengi walipangwa katika vyuo hivyo ambavyo ni Butimba, Korogwe, n.k.. Kumbe kuna wengine wengi wenye sifa ktk kundi hilo walibaki na ndio waliounganishwa moja kwa moja UDOM kutoka wizara ya Elimu.

Hao ndio wanaolalamika kuwa hawakuwa na taarifa kama watachaguliwa UDOM na kulikuwa na issue ya kuomba mkopo.
 
Kwanza nikurekebishe kidogo, wanaoenda UDOM siyo advanced diploma, bali ni diploma ya kawaida na waliochaguliwa ni wale wa form four tu. Wale walioomba kupitia wizara ya elimu kwa form four wote wamepangwa dipoloma ya elimu ya awali na msingi na wale form sx wamepangwa advanced diploma katika vyuo vya ualimu vya serikali.
Hao waliopangwa UDOM waliomba kupitia nacte na chuoni moja kwa moja, na pia walipewa taarifa mapema kwamba waombe mkopo. Hivyo kuchelewa kuomba kwa kusubiri majina yatoke ni uzembe wao au wengine kutopata taarifa kwa kuwa ni jambo jipya. Ni sawa tu na tcu ukiomba na mkopo unaomba pamoja bila kusubiri kama utapata chuo.
Pamoja na hilo kwa hawa watawekewa utaratibu wao kupitia chuo wa kuwawezesha kupata mikopo ili waweze kumudu masomo yao. Ondoa shaka ndugu.

lupeke pole sana:mimi nimhitimu wq kidato cha nne 2013 na nilituma maombi yng kwa katibu mkuu wizarani na nimechaguliwa UDOM sis katika tangazo lao hawakutwambia tuombe mkopo wala kutuelekeza kwa faida pia wamechukua ht form six waliotumia vyeti vyao vya form IV .jaribu kuwa kwanza unafuatilia kabla ya kuongea
 
Mbona unacomplain? Hapa ni kueleweshana, na si kubishana, mabishano yapo jukwaa la siasa. Nimekuambia UDOM wote ni form four tu.

Kama alimaliza form six na ameomba kwa cheti cha form four, utamhesabu mi form six, na mpaka utumie cheti cha form four wakati wewe ni form six maana yake ni form six aliyefeli.

Pia nikuambie tu kwamba dirisha litafunguliwa tena kwani hata wanaoenda advanced diploma watapewa mikopo na mpaka sasa hawajapewa fursa ya kuomba.
Kwa diploma hakuna atakayekosa mkopo.
 
nimeupenda mjadala huu ila ni busara watu wa HESLB wakaja na jibu la moja kwa moja na sio siasa zaidi kwa mfano;

Eti vyuo vitaweka utaratibu wa kupatiwa mikopo ili waweze kumudu masomo yao:swali;utaanza lini?utaratibu gani?utaratibu huo utashughulikia suala hilo kwa muda gani?

Na hiyo mikopo itatoka wapi?INAUMASANA kuona wasomi nao wanageuka wanasiasa.
 
muda wa kuapply mkopo kwa special diploma in science and math ulishatolewa ambao ni wiki mbili tu za maombi kuanzia 29/9/014.

Wadau pia nimeona extension ya muda wa kuwasili kutoka {18/10 kwenda 8/11}-2014.
 
mnaikashfu heslb wakat imefanya mapinduz? ln ulwahi kuskia diploma na chet wanashare keki ya taifa?

halaf ni ushamba wenu wa mambo ya net coz taarfa za kutma maombi heslb zilizagaa every kona. ila msjal mtafikiriwa tena kaen chonjo
 
Back
Top Bottom