Wakimpa Mkapa hii tuzo itakuwa hawa jamaa hawako makini mtu ameua watu kibao zanzibar na kunyanyasa wapinzani na democrasia isikue katika awamu yake halafu wampe?
Nawapongeza sana majaji wa huu mfuko sasa naanza amini wako makini na kazi wanayo fanya.
Papa Gee,
Na kati ya Arusha.
na Papa Gee, Arusha, - 21.10.08 @ 08:50 | #49403
Hongera morgae. Wengine wa kupewa ni Mwanawasa, kagame, mbeki. Kuffor wa Ghana. Lakini Brother Che nkapa mweke pembeni pamoja na JK, kurunzinza, kabila, kibaki, museveni, msweti II, santos, mwinyi, omar wa sudan. Mumbarak wote hawa hatufai kupewa
na Al Hasan Mwinyi, Tz, - 21.10.08 @ 08:57 | #49404
Mkapa mmemnyima Tuzo wenyewe kwa kumwandika kama fisadi
na jomba, moro, - 21.10.08 @ 09:00 | #49405
mimi nashangaa sana kwa mtu kama mkapa na huyu eyadema kufikiliwa kupewa tuzo kama hizi ni maajabu matupu. viongozi hawa ni wala rushwa wakubwa na wanaongoza kwa kuvunja haki za binadamu, kudidimiza demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari. huyu Eyadema ninamfahamu tu kwa mauhaji makubwa yaliondesha nchini kwake chini ya utawala wake. nitamwelezea zaidi Benjamini Mkapa wa Tanzania maana ndiye ninayemfamu vizuri huyu ni kiongozi mla rushwa mkubwa na siku zote ndani ya utawala alikuwa akiwazima watu wote waliokuwa wakijaribu expose rushwa mfano mzuri ni swala la GEN. ulimwengu alipojaribu ku expose ndani ya utawala alishambuliwa. Mkapa alivunja haki za binadamu kwa kutuma vijana wake Zanzibar mara baada ya uchaguzi na kuuwa watu wasiokuwa na hatia, watu wale waliuawa kwa kuamua kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa kuandamana na Mkapa aliamuru watu wale adhabu yao kuwa ni kifo. kuhusu uchumi mkapa alitekeleza sera ya uwekezaji kwa kutumia cheo chake cha urais kujiuzia kiwanda cha coal kwa bei karibu na bure na pia kuingiiza nchi katika mikataba ambayo imelitumbukiza taifa letu katika makubwa kwa tamaa yao ya kupenda rushwa na kuweka maslai ya taifa pembeni. Benjamin Mkapa kwa mtazamo wangu mimi kama mtanzania niliyeishi ndani ya utawala wa miaka 10 hafai hata kufikiriwa kutunukiwa kikombe licha ya hayo mamilioni ya dola. Benjamini mkapa angekuwa anaishi katika nchi zenye utawala wakueshimu sheria angekuwa jela kwa kutumia ofisi vibaya na kushiriki katika ulaji wa rushwa wa kupindukia.
ushauri wangu kwa vyombo hivi vya nje, please kabla hamjamfikiria kumpa mtu tuzo lolote nendeni kwenye nchi usika mkaongee na hao aliwaongoza ili kupata maoni na siyo kusoma vitabu au majarida feki wanayoandika kuhusu kukua kwa uchumi au kuleta demokrasia.
na nick, Tanzania, - 21.10.08 @ 09:44 | #49421
Mkapa haitaji hizo zawadi. alikwisha jilipa mwenyewe mara kadhaa hizo. Katika himaya ya yamafisadi kila mmoja anajilipa kadriya madaraka yake. Mo asipoteze wakati wake kuanagalia Afrika Mashariki. Huku kazi moja tu! Kukupua kila nafasi inapotokea. Huku Wizi ni halali.
na Mchora, Kibaha, - 21.10.08 @ 09:45 | #49422
Katika jukwaa la siasa Mkapa hapaswi kufikiriwa kupewa zawadi ila kufikishwa mahakamani.Mkapa ndio chanzo cha ufisadi Tanzania.Kikishika chama ambacho kinajali Watanzania lazima Mkapa na JK waende Lupango.
na OLE LETIPIPI, TANZANIA, - 21.10.08 @ 09:55 | #49426
Benjamin Mkapa ktk utawala alitumia kila nafasi aliyonayo kudidimiza demokrasia ndani ya nchi kwa kulitumia jeshi la polisi kukandamiza demekrasia na pia kutumia swala la usalama kama EXCUSE ya kuwanyima wapinzani haki yao ya kikatiba ya kukusanyana na kutoa maoni yao. Benjamini mkapa alikuwa adui mkubwa wa demokrasia .
kuhusu uhuru wavyombo vya habari ndani ya utawala wake alifungia magazeti likiwemo majira na mengineyo kwa kuandika habari ambazo akuzipenda.
aliakikisha waandishi wote ambao wanamkosoa wanachukuliwa hatua mfano mzuri ni General Ulimwengu wa RAI.
KWAHIYO BENJAMIN MKAPA HAFAI kufikiriwa kupewa TUZO yeyote ile nje na ndani ya Tanzania ambapo ametuibia pesa chungu nzima kwa kutumia makampuni ya kutoka south afrika kukusanya mapato kwa kumtumia mwanae Nicholous Mkapa.
na nick, Tanzania, - 21.10.08 @ 10:03 | #49433
Jamani hii ni Taasisi huru kama kweli tunataka maoni yetu yazingatia, basi kama una ushahidi hata wa kimazingira ukimtumuhumu rais yeyote mfano Mkapa unaweza kutuma tuhuma hizo ktk taasisi hiyo na wao huzifuatilia kwa kufanya uchunguzi kwa njia wanazozifahamu. Tukifanya hivyo tutakuwa tumetimiza wajibu wetu.
1. Kwa mfano Mkapa tunamtuhumu kwa kuviza demokrasia na pia kuua wananachi kule Pemba wasio na hatia.
2. Kujiuzia mgodi wetu wa makaa ya mawe wa kiwira kwa bei ya kutupwa
3. Mkitaba mibovu ya wawekezaji ambayo hadi leo inatutesa kiuchumi.
4. Kula pesa yetu ya kupambana na malaria aliyochangiwa na Mariah Cariah
Hizi zote ni tuhuma mimi nilizituma huko kwenye taaisis ya MO Ibrahimu huenda ndio maana hakupata hiyo tuzo
na Ron, Tz, - 21.10.08 @ 10:07 | #49436
Hebu acheni hizo bwana, tatizo Watanzania mnakariri, kuambiwa Mkapa ana kosa flani basi mnafuta mazuri yote aliyoyafanya!! huu ni unafiki wa chura..ambaye ukimwangalia kwa nyuma huonekana amekaa na ukimwangalia kwa mbele ni kama amesimama! sasa nyie haueleweki, 2005 mlivaa tshirt za ccm na kumbeba huyu bwana mdogo kikwete..leo amekuwa mzito baada ya kula misosi ya ikulu mnahaha kumtua anashindikana, acha awavunje shingo!
kama watanzania hatutakiwi kumbeza Mkapa hivi, amefanya makubwa mengi ukimlinganisha na waliomtangulia na huyu kijana aliyemfuata, hivi mnajua hata hizi barabara na majengo yote muhimu yanayomalizika sasa hivi nchini yalianzishwa katika kipindi cha Mkapa, huyu Kiwete wenu anapumulia kwenye mgongo wa huyo Mzee.
Hebu tuwe tunatoa hoja za msingi sio kufuata mkumbo bila kujua mtokapo na muendako.
After all kupata tuzo sio lazima, inawezekana alijitahidi kufanya vizuri lakini wenzie walifanya vizuri zaidi..! kwani ni ugomvi, au kawambia ameumia! jifunzeni kujenga hoja sio mnabwabwata kama bata paratatatatatata..!
na Rodney Moses, DSM,TZ, - 21.10.08 @ 10:36 | #49449
Ndugu Ron umefanya jambo la busara sana, Huyu Nyoka Cobra Mkapa anastahili kupewa zawadi ya kuwa KEKO tu na wauwaji wenzake . Namalizia kwa Kumwomba Bwana Mungu Amani iwe nawe.Shukrani
na kisisina, zimbabwe, - 21.10.08 @ 10:42 | #49453