Hapa watu wanabishana kama wako MAHAKAMANI. Mushi, nafikiri jamaa wanachokiongelea kinaonekana. Ila wee bado washikilia neno UZALENDO HALISI. Ondoa basi hiyo HALISI na bakiza uzalendo na habari ziendelee.
Hakuna kipimo cha Uzalendo. Karibu wote hapa tu-MAFISADI ila sema tu hatuna uwezo. Ndiyo maana dawa pekee ni kuweka sheria kali na ukaguzi wa mara kwa mara. Kiongozi akiwa anafanya kazi bila kuwa na MIIKO, basi atakuwa Dikteta, Fisadi, nk nk. Na hiyo miiko lazima ziwepo idara zinahakikisha miiko inaheshimika. Tatizo, hizo idara kwa Tanzania ziliuwawa, zikazikwa (azimio la Arusha, UWT nk), na hapo ndipo PEPO ya Mafisadi ikaanza. Hakuna mtu asiyetaka faida kama Mfanyabiashara. Mhindi ni binadamu wa kawaida kama sisi anayetaka na tuseme hata zaidi yetu sisi kupata faida. Kama wenyewe tunamfunulia, kwa nini asile? Kama tungelikuwa WAZALENDO kweli, basi Wahindi, Wazungu nk nchi hii wasingelipata kitu. Serikali tumejaa sisi, UWT ni sisi, POLISI ni sisi, Wizara zote ni sisi, kwenye migodi ni sisi, BoT ni sisi, bandarini ni sisi, TRA ni sisi sasa kama Mhindi ana-FISADI, mwenye makosa ni MHINDI au Sisi MIPINGO?? Kusema Wahindi ni MAFISADI kwanza ni kujidhalilisha. Ni sawa na kusema "Mitanzania haina akili". Imelala fofofo. Anakuja Mhindi/Mzungu na dola 1, baada ya miaka 5 anaondoka na dola milioni moja.
TUKOME kuwaita WAHINDI Mafisadi. Mafisadi ni SISI MIPINGO na ULAFI wetu. Hawa jamaa ni WATAFUTAJI tu. Ifike wakati tuanze kubeba misalaba yetu wenyewe. Mara ohh, Mwanamke, mara ohh, Wahindi, mara ohh Wazungu. Ningelikuwa RAIS, ningeliwafungulia Wahindi na kuwaomba Msamaha. Ila akina Yona, Mkapa, Mramba, Mary, Mahalu, Mboma nk hawa ndiyo wakushika na ku**&&^%$$$$$. Hapo sasa usubiri kama utaona kuna MHINDI au Mzungu anakuja KUFISADI Tanzania. Ua Mizizi na si matawi.
Narudia tena, WATANZANIA TUANZE KUBEBA MISALABA YETU WENYEWE.