Mohamed Dewji amemshukuru Rais Samia kwenye Jambo Gani? Aliyeelewa atuambie

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Katika Hotuba yake aliyoitoa Kwenye kilele cha Simba Day, Bwana MO, Ameanza na kumshukuru Rais Samia, kwamba anamshukuru sana Rais Samia, tena kwa kurudia rusia mara kadhaa, hii ilikuwa kabla ya Rais kupiga simu.

Ni wazi kabisa kwamba , Kushukuru ni jambo Jema sana, Binadamu yeyote asiye na shukrani huyo ni sawa na mtu mfu.

Lakini ni vema shukrani hizo ziwe kwa sababu fulani, sasa unaposema tu kwamba Unamshukuru Rais Samia bila hata kusema Unamshukuru kwa jambo gani ni lazima tukushangae, na wakati mwingine tutadhani labda Unamshukuru kwa hii Pumzi tunayoipata, maana huwezi kumshukuru Binadamu hivihivi tu.

Labda kama kuna aliyesikia Rais anashukuriwa kwenye nini basi Atuambie
 
Sababu hajatekwa
Hawa watu sijui wanawezaje kuwachota akili watanzania. Alipotekwa watu walipiga kelele nchi yote. Sasa hivi watu wanatekwa yeye kama mwathirika wa utekaji hata kulaani kwa kinafiki tu hafanyi, badala yake anakusanya ma-nyumbu uwanja wa taifa na kumshukuru utawala unaoteka raia. Hawa watu siyo kabisa.
 
Ukikaa chini ukafikiria akili za mtanzania lazima uhisi ni binadamu ambae hajakamilika.
 
Huyu jamaa Mimi pia nimemshangaa sana.
 
Mama kamwambia asivunjike Moyo, aendelee kuweka Pesa Simba....!

Yeye Kwa kipindi chake atafanya wepesi ili mpango wa Mabadiriko Simba uweze kukamilika Kwa haraka...!

Yani nyie kusoma hamjui hata Picha hamuoni.
 
Huyu no kiongozi da mbumbumbu,dakika 45 hawajaoiga on target hats moja
 
Bado anaweweseka hakuwahi fikiria kulala na bwana akiwa yeye ni tajiri no 1 Africa na Rais anawapa hela watakazo za uchaguzii......
Kakutana mwamba zaidj hela zaoe kamla kiboga au ?
 
Huenda pungufu ya kodi.
CCM kwa scratch my back i'll scratch yours ndio wenyewe.
 
Mradi yeye kashukuru na Rais Samia anafahamu kwanini kapewa shukran, tosha kabisa. Si lazima tujuwe mtu anatowa shukran za nini.

Tuwache umbea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…