Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Kaminywa kama alivyominywa Roma!Familia yake tu ndio watajua undani wa kutekwa kwake!Sisi wengine tuliopiga kelele tutabaki solemba kama sakata la Roma!
 
Haswaaaaaaa

Hata mimi nimejiuliza hili swali.
Vipi wamwachie kurejea nyumbani bila ya kumshikilia ili atoe maelezo yake rasmi kwa mamlaka ya dola ili kusaidia kupatikana kwa hao maharamia???
Hili jambo lina ukakasi sana, sijajua polisi wetu wanafanyaje kazi; nadhani kama polisi wangekuwa serious na kuwapata watekaji kama wanavyojinasibu basi starting point ilikuwa ni kuanza na option hiyo.

Ila kama hiki hakitafanyika basi Zitto apewe credit zake (na familia impe billion 1 yake).
 
Itakuwa alikuwa mitaa hiyo hiyo ya Jirani
 
Kitendo cha huyu jamaa(MO) Kutumia neno 'Nashukuru mamlaka husika na Polisi kuhakikisha NARUDI salama' Na sio 'NAPATIKANA salama' n ujumbe mkubwa sana kwa anayeelewa tofauti ya neno 'KURUDI na KUPATIKANA'
 
Kinachofurahisha kuhusu Hawa watekaji ni kwamba wanaacha same mark ukiangalia wote waliotekwa Huwa hawawezi kuja eleza ni nini kilitokea hivo tunaunganisha dot tu na kujua ni wale wale nalitegemea hilo kwa mo pia
 
Mipaka ilifungwa na ulinzi ulikuwa wa Kutosha.
 
Waache uhuni Wa kishamba watueleze ukweli.
 
Anayekulinda wewe na mali yako hata ukaweza kila mara kuandika humu JF ni nani? Au anayewalinda hao Mabwana zako, ambao kila kukicha hukimbilia kwenye vyombo vya habari kuilaumu Serikali, kama hufanyavyo humu JF, wakiwa huru na salama, ni nani?
Ni Muumba wake pamoja na Kodi anayolipa!
 
Watu wasiojulikana
Walianza Kumteka Ben sa 8
Wakafwata kwa Tundu Lisuu
Wakaja kwa Roma
Wakaja kwa waandishi wa habari
Watu wasioujulikana wakendelea na hatakati zao
Mara paaaap wakamfwata Mo
Marapaaaaap watu wasiojulikana wakamrudisha Mo na gari lile walilomtekea tena wakimuacha sehemu nyeti usiki ambayo kwa usiku ile sehemu huwezi hata kupita kizembe maana kuna mamwela wa hatari l.
Watu wasiojulikana kwanini mnaendelea kutusumbua akili za watanzania.
Watu wasiojulikana kwanini mnaumiza vichwa vyetu.
Watu wasiojulikana mtuache wajameniiiii
 
Kuna mengi sana ya kujiuliza licha ya kupatikana kwake, alkuwa eneo gani kwa hapa Dar? Alkuwa na akinani hao watekaji? Je hao watekaji bado wapo nchini au wameishatoroka?? Je walioenda kumtupa huko Gymkhana walijiamini nini wakati polisi usiku huwa wanapiga patrol? Hawakuogopa movement za watu, coz in Dar people move 24/7 ?? Je baada kutupwa huko alifikaje nyumbani kwake bila kwenda polisi kutoa taarifa au kuomba msaada? ?

Tukijibiwa hayo maswali, tutaacha kuishuku taasisi flani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…