Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Yajayo yanafraisha mkuu,, Ni kuumbuka kwa kwenda mbaliiii zaidi Unajuwa kila kitu kina mwanzo na kati then mwisho
Waswahili husema ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka, Huenda wasiojulikana wako mbioni kujianika
 
Bora ingekuwa Vitz,hilo Toyota picha yake ilikuwa mtandaoni na linatafutwa
 
IGP: waliomteka Mo walikuwa na gari la nchi jirani ila hakulitaja,ila wataalamu wa kufuatilia lile gari walisema ni la Msumbiji
Mkuu, number plate za Msumbiji haziko hivyo ....!!
 
Tumezoea kumuona Humphrey Polepole akiitisha press conference kufafanua jambo hata kwa issue ndogo ndogo tu, lkn tangu Mohammed Dewji atekwe takribani siku kumi, si Polepole wala Bashiru wala Mwenyekiti wa chama aliyejitokeza kuzungumzia tukio hili.

Tulitegemea CCM kama chama kongwe ionyeshe mfano kwa vyama vingine jinsi ya kuwa karibu na wanachama wake pindi wanapopata matatizo lkn imekuwa ndivyo sivyo.

Leo mtaenda kumwambia nini Dewji, mtaiambia nini familia yake na mtawaambia nini wanachama wenu na watanzania kwa ujumla.

Mmekosea, mtaonyesha ukomavu wa kisiasa kama chama kikikiri kuwa kimekosea, kukiri kosa siyo unyonge bali ni ujasiri.
 
Gari iliyompeleka nchi jirani imemrudisha kupitia boda ile ile na namba zile zile. Na huenda uhamiaji wamehakiki pasport zao na wakazigonga kuingia
[emoji16] [emoji16] [emoji16] hili linawezekana tu TZ ya vi-wonder.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ina maana unajifanya hujui Mo alitekwa na nani?
Really? Seriously?
 
Hawezi kuja kwani hata yeye mwenyewe alikuwa ameandaliwa cha kutueleza kabla ya kumuachia MO. Hata yale maelezo ktk simu ya MO sio yeye mwenyewe bali walitwit kwa niaba yake. NI AIBU KWA JESHI LA POLISI NA NI AIBU KWA SERIKALI NA NI AIBU KWA NCHI YETU. Mimi ningemshauri Jiwe aachane kabisa na mtoto pendwa kwani tutakuja kuyashuhudia mengi na makubwa zaidi ya haya.
 
Ndugu wanabodi,
Ukiiangalia press ya IGP kisha ukaangalia majigambo ya Mambosasa akinesha gari iliyotajwa na IGP kuwa imepatikana na MO akiwa salama kabisa lazima utagundua kuwa kuna picha imechezwa hapa
Lakini yote kwa yote tumshukuru Mungu MO kapatikana salama
Aksante.
 
kwa mtazamo wangu swala hili litaisha kama la Roma mkatoliki. mo mwenyewe atakavyotoa majibu mtashangaa. subirini..
 
Duh hawa watekaji kiboko wanaroho ngumu sana ...wakamrudisha na gari ile ile mpaka gymkana?!
 
Tunataka majibu, hamuwezi kuliweka taifa kwenye tension kubwa namna hii halafu hili jambo likaisha kirahisi hivi
 
Acha utoto Mkubwa, mbona hata Mimi mwana Yanga nilihuzunika na sasa nimefurahi kupatikana kwake? Mamipira yako yasikutoe akili,pale ilikuwa ni ishu ya afya na uhai Wa mtu ndugu. Tajiri Mkubwa kama huyu hata bila simba na Yanga angestua watu na kumbuka aliwahi kuwa MP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…