Nilikuwa sijawahi kulisikia na sikujua hilo eneo(Gymkhana) lilipo.Inanipa ukakasi kwa eneo ambalo wameenda kumtupa... lile eneo lina ulinzi sana mida ya usiku...
Mkuu nimekasirika sana. Jiwe anataka watanzania waishi kama wako shimoni! Wamemkamata Mo wakamuweka pale makumbusho huku wakiwaacha wenzio kwenye taharukiMbona Mungu ametupa uwezo wote ila hatutaki kuutumia?
Pole sana ila umeonyesha hauna ubinadamu, nilichojifunza kwako kumbe humu JF tunaweza kuwa tunajadiliana na watekaji wenyewe na wasiojulikana wenyewe.Ila Muhindi ndo Mungu wenu?
Mkuu paskali umeona clip ya hiyo gari iliyotelekezwa?yani full comedy gari ya jana tuliyoonyeshwa na igp na hii ni tofauti,ile ya jana inabeba spare tyre kwenye mlango wa nyuma.hii haina hata chuma ya kubeba spare tyre kwahiyo comedy za jiwe za chattle kabisa yani full upumbavu.Wanabodi,
Hii ni thread ya swali, nikipendekeza kwa kuuliza, maana siku hizi, ukiuliza kitu,, watu hawaonagi alama za kuuliza, wakadhani nimetoa statement.
Baada ya Mo kupatikana, baada ya juhudi kubwa sana za jeshi letu la polisi, baada ya ile ahadi ya motivation iliyopelekea hadi IGP kufanya press conference ya jana, hii imethibitisha kuwa kumbe Jeshi letu la polisi, linaweza, wala hatuhitaji wachunguzi wa nje. Jeshi letu la polisi sasa ndio linauwezo, au kama lilikuwa nao siku zote, then, likiamua, linaweza, ukijumlisha na ile ahadi ya motivation ya familia, bali limeweza kwa sababu, sasa ndio limeonyesha uwezo huo kwa kufanikisha Mo kupatikana akiwa mzima, salama uu salmini na bukheri wa Afya.
Sasa kwa vile familia tayari iliishatenga shilingi billion moja kwa atayefanikisha kupatikana kwa Mo, na waliofanikisha ni IGP Kamanda Sirro, na vijana wake, kwa ile Press Conference muhimu ya jana. Mimi Napendekeza hizo pesa apewe Kamanda Sirro na vijana wake, ili zitumike kuboresha jeshi letu la polisi nchini kwa kulijengea uwezo kuzuia matukio ya utekaji, kwa kuwa motivate, siku zote, mtu yoyote akitekwa au kushambuliwa na wasiojulikana, juhudi kama hizi za kumsaka MO, ikiwemo kuitisha press conference, zifanyike. Tena laiti kama tungelijua kabla namna ya kuwa motivate polisi wetu watimize wajibu wao, usikute hata Ben Saanane alipotoweka, tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana,
Aliposhambuliwa Lissu, tungejichanga tukatangaza dau, wasiojulikana wale, wangepatikana, na alipopotea Azori Gwanda, sisi media tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana, huwezi jua!, Bilioni moja jameni sii mchezo!.
Zamani tulizoea ahadi za motivation ni kwenye kutafutia kura tuu, lakini sasa, hata katika kutimiza wajibu.
Mungu Mkubwa, Pesa ndio kila kitu!, Masikini Ben Saanane, masikini Azori Gwanda
Jumamosi Njema
P.
Hapo kwenye gari mkuu haukuelewa vzr story!! Gari ilivuka mpaka kuingia Tanzania tarehe 1/septemba/2018 na sio ilivuka mpaka kutoka. NA INGEWEZEKANA VIPI ITOKE WAKATI TAARIFA ZA AWALI TU NI KUFUNGA MIPAKA?? TOYOTA SURF INGERUHUSIWA VIPI KUVUKA?????Hebu subir hapo hapo alipiga simu! Kwa hiyo walimpa na simu apige au alipata simu kwa msamaria mwema? Sasa huyo aliyempa simu ndo ana claim hiyo Billion au? Pia hilo gari lilimtokea walisema lishavuka mpaka! Tena leo tunaliona! Hawa wanatuona mazwazwa kabisa, haya tuleteeni hiyo cctv shootage maana jana mzee wa sisitiv alijaribu kuficha pic la gari lkn bado watu wakamzidi akili! Na ndo maana hawakusema rangi ya gari wala habari ya noah hawataki tusikie!
All in all nina furaha tajir karudi sasa kifuatacho ni kuwa zakaria tuu maana washa turuhusu kumiliki silaha.
Hahahaha ushamba wa jiwe utamcost siku moja
Cover story hapa itakuwa ni nini ? Maana hata mtoto mdogo anajua Mo alichukuliwa na kina nani .
Halafu watu wa aina hii ndio wakakae meza Moja na kina Prof Thontorn wa Barrick tutegemee kulipwa na Accasia matrilioni ??
Tutakesha tukisiburia hilo
Hebu nusahihishe pinky?Hivi umesoma ulichokiandika?
Sisi wananchi hatuna sera..tuna haki na wajibu..sera zinazosimamiwa na serikali ni za ccm..Serikali ni mwajiriwa wa wananchi ukibisha na hilo utakuwa umeshinda.
Pongezi ni kwa wote waliolipigia kelele swala hili mpaka Mo kupatikana.Pongezi ni kwa jeshi la police Kwani kelele zake zimesaidia nini??Waliotekwa wote hakupiga kelele????? Na mbona bado hawajapatikana???? Nalipongeza kwa sababu MO amepatikana na binafsi niipongeze family ya MO kwa kutoa taarifa mapema Sana baada ya kijana wao kutekwa, yawezekana pia na hao wengine Kama taarifa zingetolewa mapema kungekuwa na nafasi kubwa ya kupatikana.mbinu ni hizi hizi kwanza zuia mipaka na Fanya upekuzi wa vyombo vyote vya usafiri majini na nchi kavu.
Hawezi kuleta mizoga ya jiwe na ya mungu wa darisalamaKama Sirro angeleta mizoga ya watekaji hao tungesema kazi imefanyika kwa hio bakhresa ajifungie kabatini kwa sababu wale makaburu wakizimaliza za,Mo Energy wanakujapizipitia za Azam energy
Kama kuna Ransom ilitolewa kuna haja gani ya kupongezana ilhaili watekaji wacko huru wanagida vinnywaji