Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Watekaji watakuwa ni makaburu wanataka kumdhoofisha tajiri wa Africa!
Watekaji ni maharamia wa hapahapa kwetu. Mengine ni mbinu za kutaka watz tuamini kuwa wasiojulikana sio watz, na labda ndio maana tunaogopa uchunguzi wa nje kutuumbua. Watu wanatekwa na kuuwawa wakati wa uchaguzi, waandishi wa habari na wanaharakati pia. Ukiwa mkweli au mwenye mtazamo tofauti uko katika hatari ya kutekwa na kushambuliwa na vitisho vya kuwadhuru hata watu wa ukoo(mashangazi). Hizi ni mbinu zinatumiwa na tawala dhalimu kote duniani. Awamu hii ambayo ndio kwanza yakaribia kutimiza miaka mitatu, ndio inaongoza kwa matukio mengi zaidi tangu tupate Uhuru. Tatizo hili li 'nguoni' mwetu. Amen
 
Wanabodi,
Hii ni thread ya swali, nikipendekeza kwa kuuliza, maana siku hizi, ukiuliza kitu,, watu hawaonagi alama za kuuliza, wakadhani nimetoa statement.

Baada ya Mo kupatikana, baada ya juhudi kubwa sana za jeshi letu la polisi, baada ya ile ahadi ya motivation iliyopelekea hadi IGP kufanya press conference ya jana, hii imethibitisha kuwa kumbe Jeshi letu la polisi, linaweza, wala hatuhitaji wachunguzi wa nje. Jeshi letu la polisi sasa ndio linauwezo, au kama lilikuwa nao siku zote, then, likiamua, linaweza, ukijumlisha na ile ahadi ya motivation ya familia, bali limeweza kwa sababu, sasa ndio limeonyesha uwezo huo kwa kufanikisha Mo kupatikana akiwa mzima, salama uu salmini na bukheri wa Afya.

Sasa kwa vile familia tayari iliishatenga shilingi billion moja kwa atayefanikisha kupatikana kwa Mo, na waliofanikisha ni IGP Kamanda Sirro, na vijana wake, kwa ile Press Conference muhimu ya jana. Mimi Napendekeza hizo pesa apewe Kamanda Sirro na vijana wake, ili zitumike kuboresha jeshi letu la polisi nchini kwa kulijengea uwezo kuzuia matukio ya utekaji, kwa kuwa motivate, siku zote, mtu yoyote akitekwa au kushambuliwa na wasiojulikana, juhudi kama hizi za kumsaka MO, ikiwemo kuitisha press conference, zifanyike. Tena laiti kama tungelijua kabla namna ya kuwa motivate polisi wetu watimize wajibu wao, usikute hata Ben Saanane alipotoweka, tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana,
Aliposhambuliwa Lissu, tungejichanga tukatangaza dau, wasiojulikana wale, wangepatikana, na alipopotea Azori Gwanda, sisi media tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana, huwezi jua!, Bilioni moja jameni sii mchezo!.

Zamani tulizoea ahadi za motivation ni kwenye kutafutia kura tuu, lakini sasa, hata katika kutimiza wajibu.

Mungu Mkubwa, Pesa ndio kila kitu!, Masikini Ben Saanane, masikini Azori Gwanda
Jumamosi Njema
P.
wapewe watekaji tena! umenena!
 
Pongezi ni kwa jeshi la police Kwani kelele zake zimesaidia nini??Waliotekwa wote hakupiga kelele????? Na mbona bado hawajapatikana???? Nalipongeza kwa sababu MO amepatikana na binafsi niipongeze family ya MO kwa kutoa taarifa mapema Sana baada ya kijana wao kutekwa, yawezekana pia na hao wengine Kama taarifa zingetolewa mapema kungekuwa na nafasi kubwa ya kupatikana.mbinu ni hizi hizi kwanza zuia mipaka na Fanya upekuzi wa vyombo vyote vya usafiri majini na nchi kavu.
 
Tatizo ni script Writers, wengi kutoka Bongo Movies ndio maana hadithi za matukio imekalia kibongo movie. Yaani siku ambayo gari linalotafutwa nchi nzima lichukue dakika 15 kufika Karemjee bila ya kuonekana Taire Ndamarfali.
Au lugha moja na lafdhi ya kiafrika kusini mimi nafikiri ikiwa hujapata kukisikia kisukuma huwezi kitafautisha na kizulu. Nakwambia hata kingazija kama hukijui utasema kixhasa kwezi, ngaliwa mnono Yaani kama ile hadithi ya kifaru “Faru John”, aliejinyonga kwa vile kifaru wa kike alikuwa hamtaki si mnakumbuka alivyopotea.
Yote ni kwa sababu ya nguvu ya umma kusema hapana arudi tu, kutekana iwe mwisho. Welcome back Mo, utalosema lolote kwetu utabaki hero na victim. Iko siku ukweli utasimama.
“Pseudologia fantastica and mythomania”
Aliwezaje kuwasiliana nao kama walikua wanaongea hizo lugha za kibantu? [emoji848][emoji848]
 
Hyo hela wabaki nayo wanafamilia iwasaidie kwenda zao huko nchi za mbali wakaanze maisha mapya hii nchi haikaliki
 
FACTS
HAWAJUI KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI WALAHI
MWENYE ENZI MUNGU KAWAFUMBA MACHO NA MASIKIO NA KAWABAKISHIA MIDOMO YA KUTOLEA KINYESI WALAHI
Wacha bhana! Mungu amefungua masiko Na macho nyie wanalumumba tu?

Vilaza hamuishi
 
Ameona tz itawaka moto ,kaamuru watu wasiojulikana wamurudise salami salimini, lakini namushauri hivyo hivyo ahame tz kabisa

Inaonekana unaandika usichokijua..umejaa hisia baadala ya uhalisia
 
Gari iliyokuwa inatafutwa Tanzania nzima, ndio gari hiyo hiyo iliyomtupa Gym Khana😯..., sijui walijuaje kuwa gari iliyomtupa Gym Khana ndio gari ile ile iliyomteka mtekwaji?
Gari sio yenyewe mkuu angalia picha vizuri zile za mwanzo na za sasa.
 
Back
Top Bottom