Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama


Uwe unasoma bas kabla ya kucoment au ungetafta video ya babake alivozungumza mana uko kama umekurupuka kutoka usingizin
 

Tanzania yawakaribishaaaa mpigane kiume chema weee.....
Tanzania Tanzaniaaaaa.. nakupenda kwa moyo woteeee......
 
Ransom ndo nini Naomba kufamiswa
 
Hatimaye NYAMA tumezikuta chini, chini kabisa, tulisisitizana tuendelee kunywa mtori, nyama zipo kwa chini tu. Hakuna namna tungekosa nyama maana Mtori bila nyama, huo sio mtori ni UJI. Tujipe 'lawama' kwa kutumia muda mwingi na nguvu katika 'suala' hili!

Tumepewa simulizi kwamba mipaka yote kuna patrol, wakasisitiza kwamba hata ndani ya DSM kuna ulinzi mkubwa na mzito. Kuna 'checkpoints' baharini pia. Watekaji wamepata uhuru wa KUZUNGUKA na mateka hadi Gymkhana? Kwenye ulinzi huo? Hawakushtukiwa? Wakashuka na kuondoka? EWALAAA!

Huyu mtu ambaye alimteka MO ni kweli atakuwa anajiamini sana au akili yake imeyumba. Unamteka 'Dollar Billz Billionaire' karibu na makazi ya makamu wa Rais, yalipo makao makuu ya usalama wa taifa, unamrudisha na kumtupa karibu na IKULU, MTEKAJI anajiamini ipasavyo, au ndio 'akili ndogo' tunayosikia?

Yaani watekaji wakaona sehemu salama sana ya kwenda kumtupa Bilionea huyu ambaye ulimwengu wote unaongea habari zake ni karibu na IKULU? nafikiri Rais wetu hawezi kuwa salama kwa mantiki hiyo, maana makazi yake 'maharamia' ni rahisi kuyavamia, hata kutelekeza 'mtekwaji' na wao kutokomea wasijulikane walipo!

MTEKAJI anaetafutwa na polisi nchi nzima, habari ulimwengu wote, gari ambayo tayari imejulikana, aendeshe gari hilo, usiku, kwenye vizuizi hadi karibu na IKULU (Gymkhana) amtupe MATEKA (MO) halafu atelekeze gari yake, nafikiri Huyu MTEKAJI anajiamini sana au ana akili ndogo sana!

Hata vizuizi vya polisi vimeshindwa kutambua gari ambayo wenyewe walitupa picha? Wameshindwa kuwakamata watekaji, hadi wamemuachia mateka na kuondoka bila kujulikana. Sielewi sababu za MO kuachiliwa ni msukumo wa umma au kiasi cha Pesa kilichoahidiwa na familia?

Simu ambayo 'MO' alitumia kuwasiliana na 'nduguze' anaweza kuazima, kwa nani usiku ule (saa nane?) maeneo yale, hakuna msongamano wa watu ndio swali la msingi. 'Suspected Car' ipite 'Patrols' zote hadi Salender bridge (palipo na ulinzi mkali), waende wakaegeshe Gymkhana, wamtupe?

Kimsingi WATEKAJI hawa ni watu wakarimu sana. Wakachukua na simu wakampa bwana 'MO' awajulishe ndugu zake kwamba kaachwa Gymkhana? Huko mafichoni wakamlazimisha kula chakula hata alipokuwa anakataa, fedha wameamua kuacha wakati walikuwa wanazitaka!

'MO' ametelekezwa usiku huo, watekaji wameondoka, 'MO' akapata simu, akawapigia ndugu zake, ndugu zake 'mbio-mbio' hadi Gymkhana bila kuwajulisha polisi, wakaenda kumchukua 'MO' ambaye alitajwa kutafutwa ma polisi kwa siku 8 plus. Jambo la Kheri sana!

Au kuna njia nyingine ambayo 'MO' alitumia kuwasiliana na nduguze usiku ule? Kama haipo, walifahamu vipi ndugu yao katupwa hapo Gymkhana? Walimpata vipi mwenzao? Walifahamu vipi katupwa na kutelekezwa hapo? Alitembea mwenyewe kuelekea nyumbani kwao? Alifuatwa na polisi au nduguze?

Awali tulielezwa kwamba 'MO' katekwa na watu wenye kudhaniwa ni "wazungu" baadae tukaelezwa gari lenye umiliki wa wa kutoka "Mozambique" wanahusika, baadae usiku wa kauli ya pili 'MO' anatelekezwa, tunaelezwa 'waliomteka walikuwa wanasema kwa moja ya lugha za South Africa'. Disturbing kweli-kweli.

Jinai ambayo ABDUL NONDO alitekwa na kupatikana ndio sawa ambavyo 'MO' ametekwa na kupatikana, lakini kwa 'MO' tunaelezwa 'kapatikana' kwa Abdul 'kajiteka' MO anapelekww nyumbani, Abdul mahabusu baadae mahakamani. Abdul hadi waziri akasema "alijiteka" na kushadadia!

Watekaji hawa ni 'intellectual Kidnappers' yaani wanajua bwana 'MO' anapenda kwenda GYM wakamteka Colleseum hotel, watekaji genius wakajua 'MO' anapenda mchezo wa golf wakamrudisha 'GYMKHANA' watekaji wakarimu sana mpaka gari waliyoitumia wameiacha hapo na hata pesa hawataki tena!

Wazungu, watu kutoka nchi jirani, wasauzi; wakasafiri hadi Tanzania kupitia Mozambique, wakanunua silaha, wakatafuta chimbo, wakacheza na CCTV za Colleseum, hawakuonekana, wakamteka Eneo lenye ulinzi (siku nane) wamemerudisha Eneo lenye ulinzi, hawakutaka hata 'BUKU' wakati tunaelezwa shida ilikuwa pesa! OK! OK!

Watekaji ni mashujaa kweli-kweli. Jamaa wanasema "HODARI" maana Wamemteka karibu na makazi ya makamu wa Rais (Oysterbay) baadae wanamuachia karibu na makazi ya Rais (Gymkhana), nafikiri, naamini kuna kila sababu ya TAIFA kufanya mjadala mkubwa kuhusu 'usalama wa Raia na Mali zao'

Naamini, hawa watekaji ambao wamekuwa wakarimu ipasavyo kwa ndugu yetu 'MO' wataendelea kuwa wakarimu ipasavyo kwa ndugu zetu wengine walioteweshwa na ndugu zao hawajui kama wataaona tena. Wataturejeshea tena ndugu yetu.

Muhimu; Mohammed Guramambasi "MO" Dewji karejeshwa salama mtaani na atajumuika na familia yake, Kutekana-tekana ni uhuni wa kishamba tu! Sasa tukasikilize "MTU PESA" kutoka kwa African Stars Band (Twanga Pepeta)
 
This is good news, if is true!
Edit: Nimejiridhisha kwamba hii ni habari ya kweli. Thanks to all that worked tirelessly to get MO back home safely. Mungu ibariki Tanzania.
Unaàmbiwa hakuna aliyefanikiwa kumpata Mo ispokuwa watekaji wenuewe wameamua kumrudisha na kumtelekeza pale Gymkhana mita chache tu kutoka Ikulu.
 
Mimi naamini kuwa kila mwenye akili anajua fika ni nani alimteka Mo, nani alimteka Ben, nani alimteka Azory, nani alimpiga risasi Lisu, n.k. Wote wanamjua.

Nadhani tatizo ni kuwa hakuna uwezo wa kumfanya lolote. Mtekaji huyu, mtesaji, mwonevu na muuaji.
 
Ta
Tamko la waziri Lema limevuna duniani kote na limetetemeaha hasa
 
Ukweli sauti za akina Lema, Zito na sisi sote tuliopaza sauti mitandaoni na kwenye mazungumzo mitaani (maana karibia kila mtu alionekana kutoamini hadithi za akina Mambo ya Nyakati hizi), imesaidia sana hawa watekaji, wauaji na waonevu kumwachia binadamu mwenzetu.

Tunazidi kusisitiza, kama mtu amefanya kosa afikishwe mahakamani lakini siyo hii primitivity inayofanyika siku hizi.
Mungu ana makusudi ya kutuletea cdm
 
Ni mpumbavu anasema huu ni ujinga halafu anapoteza muda wake kutoa povu kwenye ujinga!

Povu ulilotoa linaonyesha ni jinsi gani ujinga wangu umekuchoma kihoja mpaka unaonyesha upumbavu wako!

Kama umechukia sana, go hang! Who care?
Sentensi yako ya mwisho nimeipenda sana.
 
Kuna ukakasi mwingi juu ya utekaji wa MO na cha ajabu Polisi bado wanafikiri watanzania ni wajinga kiasi kwamba hawataweza kujua Sinema ya akina Bashite na group lake ilivyochezwa vibaya na kukosewa hesabu zake.
 
Alipotea saa kumi na moja alfajiri kapatikana saa tisa usiku. Kind of strange.

Halafu alikuwa anabembelezwa kula chakula.
 
Mkuu imesaidia sana naona tunawaiga marafiki zetu wa Rwanda na Uganda
 
Kimya kitafikisha ujumbe kwa kasi sana kuliko atakayoyaongea kama atapindisha ukweli
 
Kwani unadhani karudi mwenyewe toka alikofichwa.....jeshi "limepambana" juu chini kumrudisha.

Jeshi lipi? La wapi? Yaani gari itoke huko ilipokuwa ije mpaka mjini wamtupe mtu pasipo kuonekana? hizo Sinema za kihindi kwa kizazi hiki cha Sayansi waache kuzileta Tanzania, kama wanazipenda wakatengenezee huko kolomije kwanza.
 
Wamebana wameachia, Jiwe siyo Mtu!.

Namshauri Mo asepe atulie zake huko Brunei au Kisiwa chochote cha Pasifiki ale bata miaka saba ipite kisha arudi tujenge nchi!, yeye bado kijana, kupumzika miaka saba siyo ishu!
Unauhakika na unachosema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…