Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mkuu hakiki mawazo yako. Huwezi kuchukua 1b ama kwa shs au dola cash bank bila mamlaka zote kujua. Hivi unadhani hakuna alert ilikuwa kwenye mabenk?
Fikiri zaidi kidooogo.
 
Endelea kunengua tu tunakutazameni mtamaliza viunu aina zote awamu hii. Mate yatawakauka maana hoja za maana hamna mmebakiwa na haja pekee. Eti makada mbona hamkuguswa na tukio la kutekwa Mo? Kwanini baada ya Zitto na Lema kuwatikisa Mo kaonekana vina uhusiano gani?
 
Hili gari ndio hao wanaosemekana watekaji walitaka kulichoma moto na wakaanzia kuunguza siti .uongo uliojee
 
Mmejidhalilisha wenyewe kwa ushamba wenu na Kick huwa haiendelei, Polisi na Tanzania imevuka nguo siku zote badala ya kutafuta mtu nyie ni kulumbana na wanasiasa mpaka mtu karudi mwenyewe babu yako misuti alisema wametekwa 75 kabla ya MO hii si aibu kwamba kila mtu arudi mwenyewe.

Kaeni kimya kuficha upumbavu wenu jana Siro alisema hajui yuko wapi na kama mzima vipi leo apongezwe.
 
Watu wawili au kumi hawawezi kudanganya UMMA wa watu Million 40 Kwa wakati mmoja

Mkuu, ni ngumu sana kumdanganya mtu mzima mmoja tu mwenye akili timamu, hata kwa siku 5 mfululizo, iweje iwe rahisi kuwadanganya waTz Million 40+. Wanaoratibu haya mambo siamini kama hawalijui hili ninachokiona ni kiburi tu kwamba hata wakijua ni "Sisi" watatufanya nini zaidi ya kelele tu.
 
wapenda amani walipiga kelele mtanzania mwenzetu arudi..
haikujalisha alikuwa chama gani...
amerudi tumefurahi..
mbona unajishuku jombaa
ila ni wazi awamu ya tano imezalisha magaidi zaidi..
*magaidi hao wamefanya matukio mengi ya utekaji na watu kutishiwa ama kupigwa risasi..
halafu pombe huwa haongeagi..
ila la shilawadu atalitolea mapovu
 
Wanaona hakuna tunaloweza kufanya
 
Nawaza tu katika stori nilizosikia kuhusu maiko jaksoni na akina eminem n.k

"gari ile ile ilomteka ndo ilompakia tena"
Hakufungwa kitu usoni ?

Kama hakufungwa ina maana aliwaona watekaji kwa macho?

Kama hakuwaona,vipi alione gari kwamba ndo lile lile kisha asiwaone watekaji?


Nimemuona Mo dewji sijuiiiiiiiiiiiiii
 
Nahumu:3.1
Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki.
Nahumu:3.2
Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka;
Nahumu:3.5
Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.
Nahumu:3.6
Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau.
 
Wanasema Aliwaona ila hakuweza kuwatambua walikua wamevalia mask mkuu
 
Ni utani ambao unaweza onekana wa kipumbavu, lakini hata mimi nilipomuona nikamfananisha na mo sallah. Tunashukuru amerudi salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…