Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa 'Taifa Stars', Mohamed Hussein 'Mmachinga', ameiponda Taifa Stars kutokana na mfumo na mbinu zinazotumiwa na kocha Salum Mayanga.
Akizungumza na Nipashe muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Taifa Stars na Malawi Uwanja wa Uhuru juzi, Mmachinga, alisema mbinu zinazotumiwa na Mayanga hazisaidii Taifa Stars.
Mmachinga, alisema kuwa Mayanga alianzisha kikosi kwa mbinu ya kujilinda zaidi huku akitegemea mashambulizi ya kushtukiza ambayo hata hivyo hayakuwapo.
"Timu haikucheza vizuri, kocha aliaanza na mfumo ambao haukutusaidia, tulikuwa nyumbani na ni mchezo wa kirafiki, hatukupaswa kucheza vile," alisema Mmachinga.
Bila kufafanua, alisema kunatakiwa mabadiliko makubwa kwenye timu hiyo.
"Mayanga ni kocha mzuri, ila kuna kasoro ndogo ndogo zinatakiwa kufanyiwa kazi," alisema Mmachinga.
Taifa Stars ikiwa nyumbani, juzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Malawi huku Simon Msuva akiibuka shujaa kwa kuisawazishia katika kipindi cha pili.
CHANZO: Nipashe