Mohamed Issa "Banka" akaribia kutua Simba SC

Kasapwenda

New Member
Joined
Oct 5, 2017
Posts
2
Reaction score
1

Baada ya Yanga kuchelewa mahasimu wao Simba wameibuka kwa mbele na kupeleka ofanono kwa Mtibwa Sugar kwa ajili ya kiungo Mohamed Issa 'Banka'

Kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Mohamed Issa 'Banka' yupo mbioni kukamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Simba, ambayo imeonyesha kwenda resi kwa ajili ya kumsajili katika kipindi hiki dirisha dogo.

Meneja wa mchezaji huyo Jamali Kisongo, ameisema kuwa, amekuwa akikutana mara kwa mara na viongozi wa klabu ya Simba, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na timu hiyo kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa amekuwa gumzo nchini.

"Simba wapo kwenye wakati mzuri kumchukua kwasababu wamekuja na tumezungumza nao zaidi ya mara mbili na ukweli mambo yanakwenda vizuri kama wakiendelea hivi wanaweza kumchukua Banka," amesema Kisongo.

Kiongozi huyo amesema awali Yanga walikuwa wakimtaka mchezaji huyo lakini wamekuwa kimya tofauti na wenzao Simba ambao licha ya kuongea kupitia vyombo vya habari lakini wameonyesha kwa vitendo kama kweli wanamuhitaji mchezaji huyo kwa kukutana naye yeye kama Meneja wa mchezaji.

Mohamed Issa 'Bank' amekuwa kwenye kiwango bora hivisasa kutokana na kazi nzuri anayoifanya kwenye klabu yake ya Azam FC na timu ya taifa ya Zanzibar ambayo inashiriki michuano ya kombe la Chalenji huko nchini Kenya.
 
Mi bado naona yule mfungaji wao anaitwa mohammed juma ni mzuri na sisikii kutakiwa na timu kubwa. Alitufunga bao la pili na akahojiwa na kusema kuwa anahamu ya kuchezea stars ila huwa haitwi na hivyo ndo salvam hiyo
 
Timu itawashinda viongozi,, dawa yenu BAKORA TU,, mnaacha kusagili strikers mnakimbilia mchezaji kisa YANGA wanamtaka,,, UPUUZI WA KIWANGO cha lami... ni bora kubaki na MAVUGO
 
Aisee we mwandende una mawazo kama yangu. yaani hawa viongozi wa simba hovyo kabisa. yaani wamesajili huyo mchezaji kwa kuwa yanga wanamtaka basi hakuna lingine. shida ya simba sasa hivi sio viungo, kipa wala beki shida ya simba ni washambuliaji wawili wa kati wa kumpa changamoto Boko basi. hata huyo kwasi wangemsajili mwakani wamwache mwanjale amalizie msimu kwani bado ni mmojawapo wa mabeki bora wa kati kwenye VPL. hao viongozi wangemsajili yule mshambuliaji khamis suleiman ningewaelewa au yule mtoto wa kenya kwenye challenge anaitwa Ochieng.
 
Back
Top Bottom