Mohamed Issa: Kwenye hili la utekaji sio serikali pekee ya kunyooshewa kidole hata hao wapinzani wanaweza kutekana

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Akizungumza na BBC mchambuzi wa mambo ya kisiasa ndugu Mohamed Issa amesema kuinyooshea Serikali pekee kwenye mambo ya kupotea na kutekwa kwa watu sio sawa kwani hata vyama vya upinzani huwa vinafanya hayo matukio kama matokeo ya kutofautiana wao kwa wao.

My take
Hivi inawezekana kweli kwa Tanzania yetu chama cha upinzani kikafanya mauaji kama Yale ya Kibao!? Ukizingatia mheshimiwa Rais alijisifu kwamba intelejensia ya Tanzania ni kubwa sana.
 
Sheilkh Mohamed Issa amesema hivyo au unamsingizia?
 
BBC waache kuhoji watu waliokunywa vilevi.Udini umemjaa hadi kwenye kope bila hata kujali uhai wa watu.
 
Wakati tukiwa Chadema tulikuwa tunatekana ili kupata ruhuma ,Dk Slaa

USSR
Wana jitahidi kuhamisha magoli.
Sawa kauliwa na chadema tuseme.
Kabla ya kuuliwa inaonekana alikiwa anafuatiliwa kwa simu.wekeni mawasiliano yake ya mwisho
 
Wakati tukiwa Chadema tulikuwa tunatekana ili kupata ruhuma ,Dk Slaa

USSR
kibao alitekwa kwenye maeneo gani?
chadema wangemtaka kumuua kibao wasingesubiri apande kwenye gari wakamshushe wakati ni mtu wao.
 

Punguani huyo Mohamed Issa......Hivi unadhani wapinzani wangekuwa wanateka ingechukua hata dakika 5 bila kukamatwa? Wapinzani wapo clean lakini kila siku wanapelekwa mahakamani kwa kesi za kubumba.
 
Hapo ndipo uchunguzi huru unahitajika kubaini wahalifu. Isiwe serikali, vyombo vya usalama au vyama vya siasa.
 
Uchambuzi wa kijinga kabisa. Hata hawezi kukumbuka ni nani anao wajibu wa kuchunguza na kubaini hao wapinzani wanao teka watu.
Akili za hawa watu zimelala kabisa.
 
Unapo anzakuona watu wa aina ya huyu mzee wanapigania chama, hapo ni lazima uanze kuwa na mashaka makubwa juu ya usalama wa chama hicho.
Inaonekana CCM tayari imetekwa, imebaki tu watu kukana hali hiyo kwa mazoea tu na woga wa kuto onekana wao ndio wenye matatizo.
Lakini uozo kamwe hauwezi kujificha milele, ni swala la muda tu kila kitu kitajifunua wazi.
 
Tunapouingizia uhai wa watu itikadi na U-Chama ni dhahiri kuna mahali tunaelekea..!
 
Ingekuwa wapinzani wanatekana basi utekaji ungeshaisha siku nyingi
 
Sisis wananchi hatuhitaji ngojera na kutupiana lawama kila upande, tunachohitajii wahusika watafutwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria, bila ya kujali ni nani altenda huo unyama. Huyo mchambuzi uchwara aliyeenda kuropoka BBC alikuwa na fitina zake binafsi na anavutwa zaidi na kutetea wale wanaotoka katika upande wake ( " upande wake kwa kuwa ni mwenzetu")
 
Ndicho na Rais amefanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…