Mohamed ' Mo ' Dewji usikubali kutoa Pesa yako kutusajilia Simba SC wachezaji hawa wabovu

ndio maana ukajihami mapema kama Mavugo ni rahisi kukabika mbona ile mechi tuliyokuwa pungufu aliwafunga bao na bado akawafungisha tela walinzi wa yanga bahati mbaya mpira ukagonga mwamba. Simba inatakiwa kutengenezwa ya sasa na ijayo siyo ya usajili kwa ajili ya leo tu
 
sasa tunaweza kuwa na kujadiliana. hapa umeandika kitu. naheshimu mtizamo wako ingawa naamini pia uliandika ukitegemea kuwa watakuja watu na mawazo tofauti na si wote watasema ... hewala au tawile.

1. laudit mavugo
huyu ni mchezaji mzuri lakini tatizo lake kubwa limekuwa ni kisaikolojia na hasa ni imani hizi za kiswahili ambazo watu wamemlisha au yeye mwenyewe kwa fikra zake. anaamini amerogwa, anaamini anahujumiwa na wenzie au mwenzie.tayari hapa ameshashindwa... angepata mtalaamu wa kisaikolojia ana akapewa mechi nyingi kucheza angekuwa mchezaji mzuri sana. na ikiwa ataenda team nyingine hapa tanzania utakuja kumwona ni mchezaji mzuri. ana kosa tu kuwa aggressive kutokana na aina ya uchezaji wake ule wa kunata na huo woga kweli anao. hapa anatakuwa kujengwa kisaikolojia. ila nakubali kwa sasa aachwe tu.

2. blagnon fredrick namkubali na nlikuwa namkubali toka mwanzo ni moja ya washambuliaji ambao nilishangaa kwa nini waliachwa na simba. alikuwa ni aina ya mshambuliaji kama john boko. yaani analazimisha kufunga hata kwa tumbo au makalio ili mradi afunge. kutokana na kuwa na nguvu kweli ukabaji wake ulikuwa mgumu. aangaliwe ana umri gani ikiwezekana arudishwe.

3. adam salamba na marcel kaheza ni wazuri.
tambwe hakuwa mchezaji mwenye nguvu sana au mkwara kwa mabeki. ni mviziaji ,ambaye unaweza kutomsikia kwa karibia dakika 20 ila ukaja msikia akiwa amefunga. hakuwa akitisha kama hao wengine akina blagnon au boko. so aina hii ya wachezaji pia ni wazuri maana wanasahaulika na hapo ndo huja kuwakumbusha mabeki kuwa wapo. salamba akipewa maelekezo ya kutulia na kuwa makini anaweza kuwa mzuri zaidi sababu nguvu anazo na umri unaruhusu.

marcel ni aina ya washambuliaji kama tambwe pia anaweza fundishwa na kupewa mazoezi ya kukaba.. but si lazima sana.. kuna washambuliaji wanaiwa goal poachers ndo alivyo huyu kijana... yeye ingekuwa ile miaka yetu tunacheza chandimu basi angekuwa ana uwezo hata wa kukaa na goal keeper wanapiga stories ila ukiipata mpira mpigie huko huko mbele..atainuka na kufunga.. huyu mnapokuwa mmezidiwa anakaa mbele standby nanyi mnamrushia mipira mirefu.kwa hiyo anafaida yake la msingi awe na pumzi na mbio basi.

ukitoa blagnon nani wengine kwa ndani na nje ya nchi wanafaa? viwango vya wachezaji wetu sometime havika constant unamkumbuka mbaraka mwaka jana? leo yupo wapi? aliweza msuva,tambwe,boko n.k kudumu kwa muda mrefu nadhani sababu ya nidhamu.

 
kama mkibahatika kuingia makundi CAF mwakani ...ni baada ya miaka 19 mweee...wakati mwingine muwe na heshima kwa Yanga
 
Usajili wa Kaheza ni sawasawa kabisa kwa simba ila kwa Salamba simba wamechemsha. Simba ilihitaji mshambuliaji mmoja tu wa ndani na mwingine mmoja wa nje/kimataifa. Kwa sababu Kichuya amesemekana anaondoka na hata asipoondoka mbadala wake ni Kaheza kwa namna mfumo wa Simba ulivyo. Kichuya huwa anacheza sana free nyuma ya Boko na Okwi jukumu hilo Kaheza anaweza lifanya vizuri japo anaweza asimfikie Kichuya. Iwapo Kichuya ataondoka ni nafasi kwa Kaheza kuchukua hilo jukumu na hata kama akibaki bado Kuchuya akiwa majeruhi au ana kadi Kaheza ataziba hiyo nafasi. Na iwapo Kichuya ataondoka ni vizuri simba ikamrudisha Ramadhani Singano japo aliondoka kwa nyodo kwani ndio mtu ninayemuona anaweza kumback up Kaheza. Kumsajili Salamba ni kupoteza pesa tu kwani Simba ilipaswa kumpandisha Kitandu kwani aina yao ya uchezaji na Salamba haina tofauti kubwa hata matumizi ya nguvu ni sawa tu. Kitandu amekosa tu nafasi lakini naamini angepata nafasi ni zaidi ya Salamba. Simba waachane sasa kushinda na Yanga na Azam kusajili badala yake wajikite kusajili wachezaji hasa wa kimataifa wawili mmoja mmaliziaji mwenye nguvu kama Boko na kiungo mshambuliaji anayejua kukaba wa kuwachangamsha Ndemla na Muzamiru ambao wanaonekana wamelala.

Na makocha wa simba nao wajitahidi kuwarekebisha Ndemla na Mohamed Hussein. Kwani kuna makosa wanyoyafanya tangu waanze kucheza ligi kuu mpaka sasa. Kama kuna watu wako nao karibu wawajulishe vinginevyo watabaki hivyo hivyo miaka yote. Nikianza na Ndemla ana mashuti makali kweli kweli yangekuwa yote yanalenga goli vizuri kila msimu asingekuwa na chini ya magoli kumi. Lakini mashuti yake yasipopaa basi yataenda nje ya goli. Katika mashuti matano moja tu ndio linalenga goli. Pia akiwa kama kiungo aache kugeukia goli kwake anapopata mpira anapaswa kugeukia goli la upinzani apeleke mashambilizi mbele hapaswi kupiga back pass hiyo ni kazi ya mabeki.

Mohamed Hussein yeye anakaba vizuri anapanda vizuri sasa hizo krosi zake ndio tatizo. Kuna aina nyingi za krosi kuna zile unapiga kwenye nafasi, kuna nyingine unamlenga fowadi wako n.k. lakini zote hizo zinamshinda. Asione aibu ajifunze namna kwasi anavyopiga krosi zake. Lakini akishindwa basi apige zile krosi shuti za kuchonganisha walau beki akichanganya anatumbukiza mpira golini kwake. lakini krosi zake za kupapasa haziisadii timu mwisho benchi litaendelea kumhusu
 
Kuna wachezaji wengine mpaka nawaonea huruma, sasa kama Salamba Simba atacheza wapi? kama sio kusugua bench pale na wenzie wakina Moh Ibrahimu, Mavugo, Husein Mohammed
 
Pesa ipo kwa mhindi ya bure yeye anasajili tu.
 
Ulichokiandika kuhusu Marcel kaheza bonaventura sio kweli huyo dogo kacheza mpira kwa misimu mitatu mfululizo bila kushuka kiwango ebu mfwatilie statistics zake ujiaminishe
 
Umenikumbusha Ramadhan Singano (Messi) jinsi alivyoondoka Simba kwenda Azam na kusababisha mvutano na malumbano mengi. Sijui yuko wapi huyu dogo.

Vv
 
kama mkibahatika kuingia makundi CAF mwakani ...ni baada ya miaka 19 mweee...wakati mwingine muwe na heshima kwa Yanga
Yanga huwa anaishia njiani tu, habebeki. Pamoja na kupangwa na wenzetu wa Rwanda na Kenya, bado yanaelekea kumshinda.

Vv
 
Wewe si mtusi nenda katoe huo ushauri kwenu rwanda kwenye team ya APR au Rayon Sport
Wewe pamoja na hao waliolike ulichokiandika akili zenu haziko sawa, msituletee ukabila hapa, Simba ina mashabiki all over East Africa, hili tatizo la ukabila na ukanda limekuwa likikua siku hadi siku humu jamvini, yaani mtu anaandika uzi mtu mzima na akili zako unaanza kumfikiria kabila lake!
 
Mpaka leo najiuliza ilikuwaje tukamwachia Blagnon tukabaki na yule Pimbi Mavugo.
 
Kwa hiyo kufunga bao mechi moja tayari unam judge mchezaji?mtoa thread ni Simba lialia wala sio Yanga ila kwa Mavugo mlilamba garasa
 

Umejitahidi sana kutoa mtazamo wako lakini bado nikujuze kitu kimoja.
1. Naamini huu ni usajili wa ndani tu ambao bila ya shaka kwa aina ya washambuliaji tuliano saizi Tanzania bila ya kuwachukua hao sijui utakwenda wapi tena kusajili!
Salamba naona kama amelalamikiwa sana na wanasimba wengi kutokana na aina a uchezaji wake lakini kwa sasa hatuna budi kumpa muda ili athibitishe kwa nini amesajiliwa.

Naamini lengo la Simba ni kutafuta mbadala wa Bocco na Okwi wanapokuwa na dharula za aina yoyote ile. Kuna kipindi Simba iliyumba kwa sababu Okwi alikuwa yupo kwao na Bocco akawa na shida kidogo. Sasa hao ndiyo vijana ambao kocha ana kazi ya kuwabadilisha ili wawe kama akina Bocco na Okwi wajao kwa sababu uwezo naamini wanao.

2. Sidhani kama Simba wameanza kufanya usaniji wa wachezaji wa nje zaidi ya tetesi za Papy Kambamba. Lakini naamini utakapofika wanaweza kukidhi kiu ya mashabiki wao japokuwa Simba hatuna historia ya mafanikio ya kusajili wachezaji wa nje wazuri.

Ukianza Pape Ndaw, Mavugo, na wengine wengi wanaishia kupiga mishahara kubwa kazi kidogo ukimtoa Okwi na Tambwe. Naona kipengele hicho wanataka kukiendea taratibu ili wakidhi haja na matamanio ya timu katika kufika malengo yao.

Namiini ukifika wakati ndiyo tunaweza kusema mengi ila mpaka sasa siyo mbaya siyo nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…