Mohamed Mwameja hatomsahau Al-Haj Muhidini Ndolanga

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
Ukipata nafasi ya kuzungumzia masuala la ya soka la tanzania na aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba na Taifa stars, Mohamed Mwameja, ni lazma akusimulie kisa hiki.
Miaka ya tisini enzi hizo Muhidini Ndongala akiwa ni Mwenyekiti wa chama cha soka cha tanzania(FAT).
Taifa Stars ilikuwa katika michuano ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika, ikawa imebakiza mechi moja ya ugenini ambayo Taifa stars ilihitaji droo tu na timu ya taifa ya Bukinafaso ili ifuzu kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika.
Inasemekana Ndolanga alipokea hongo, mpaka siku ya mechi inakaribia, Mwenyekiti huyo akatoa comment kwamba FAT haina pesa ya kuigharamia timu hivyo timu ikajitoa na kuiachia Bukinafaso ifuzu kiulainii.
 
Sasa Mwameja anahusika vipi? Mwameja aligombana na hicho kibabu sijui ilikua issue gani kibabu kikamwambia hatakaa achezee Taifa Stars labda kibabu kiondoke FAT enzi hizo. Yale yale ya Maximo na Kaseja. Hilo la hongo kwa kibabu wala simo.
 
Ndiba - Kwani na Mwameja alistahili kupata mgao au ni vipi? Au hii mechi ingemtoa vipi Mwameja?
 
Mkuu habari **** ina utata kidogo taifa Stars haikuwahi kuhitaji droo ifuzu mara zote tunakuwa wa mwisho au wa pili kutoka mwisho. Mwameja alikosana na Ndolanga baada kufungisha kizembe bao la faulu dhidi ya Misri.
 
Siwezi kukukatalia kama hii habari ina utata kwani siwezi kumwamini Mwameja (ambaye alinipa habari hii)
Pia nakumbuka vizuri kwmba miaka hiyo Taifa stars ilikuwa 'kichwa cha mwendazimu'
 
Ndiba - Kwani na Mwameja alistahili kupata mgao au ni vipi? Au hii mechi ingemtoa vipi Mwameja?
Kwa mujibu wa Mwameja, anasema yeye alikuwa kizalendo zaidi hivyo kufuzu kwa stars kungeipaisha Taifa kisoka.
 
Hapo kama angeongelea ukiritimba wa FAT,hapo ningemwelewa!!! Ila ndolanga na Mwameja ni hoja mbili toufauti
 
U
Mkuu habari **** ina utata kidogo taifa Stars haikuwahi kuhitaji droo ifuzu mara zote tunakuwa wa mwisho au wa pili kutoka mwisho. Mwameja alikosana na Ndolanga baada kufungisha kizembe bao la faulu dhidi ya Misri.
Ugomvi wa Mwameja na Ndolanga unatokana na Ndolanga kumfanyia fitna Mwameja wakati amepata dili la kwenda kuchezea Reading ya Uingereza. Na FAT ilikua na fitna sana those days ndo maana wachezajo wetu walishindwa kwenda kucheza nje
 
Ulichokiandika ndio ninachokifahamu mimi, ingawa sijui kwanini ndolanga alimnyima vibali
 
Ulichokiandika ndio ninachokifahamu mimi, ingawa sijui kwanini ndolanga alimnyima vibali
Kwa mujibu wa Mwameja mwenyewe anasema dili la kwenda Reading alipewa na Mzee Jomo Sono sasa yeye akamwambia Jomo Sono kwamba hawezi kwenda ulaya wakati hajui familia ataiachaje, Mzee Jomo Sono akamhaidi kumpa hela ambazo alizituma kupitia Account ya FAT, kwa uhuni wao wakishirikiana na mmoja wa viongozi wa simba wakasema Simba ilikua inadaiwa na FAT na ile hela wamekata juu kwa juu. Sababu ya kunyimwa kibali ni wazee walikua wanataka 10% kabla ya kutoa kibali
 
U

Ugomvi wa Mwameja na Ndolanga unatokana na Ndolanga kumfanyia fitna Mwameja wakati amepata dili la kwenda kuchezea Reading ya Uingereza. Na FAT ilikua na fitna sana those days ndo maana wachezajo wetu walishindwa kwenda kucheza nje

Hiki ulichoandika ndio ukweli wenyewe.. nakumbuka kuna mechi moja mwameja aligoma kumpa mkono ndolanga wakati wa kusalimiana!.. gazeti la sanifu likamchora na kumuita MUHIDINI DOO LANGU!!.. inawezekana akawa rais wa chama cha soka aliechukiwa kuliko wote nchini
 
Huyu mzee Alhadji pamoja na ndugu yake Aden Ismaill Rage pamoja na wazamini wa Simba na Yanga walichangia kwa kiasi kikubwa kufelisha maisha ya wachezaji wa zamani
 
Mwaka gani stars ilikuwa inahitaji draw tu ili ifuzu afrika!?...halafu eti fat wakadai hawana hela za kwenda kwenye mchezo na Burkina Faso so tukawaacha waende!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…