Mohamed Said na Historia ya TANU

Mohamed Said na Historia ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Mohamed Said na uvurugaji wa historia ya nchi yetu

Na Prudence Karugendo

''Nimevumilia sana mpaka imefikia mahali naona niandike kuhusu uvurugaji wa makusudi wa historia ya nchi yetu unaofanywa na mtu mmoja anayejiita kijana wa mjini, hasa Dar es salaam, Mohamed Said!''

Hii ni sentensi ya utanguliza katika barua yake aliyoniandikia na kuisambaza kwa wasomaji
wengi kwa barua pepe.

Jibu langu kwake nimeliweka pamoja na barua hii yake.
Soma utetezi wangu hapo chini:
 
Attachments

JIBU LA BWANA KARUGENDO

Hiyo hapo juu ni barua aliyoniandikia Bwana Karugendo akinilaumu kwa kuandika kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.’’Padri amenishtumu kwa ‘’kuvuruga,’’ historia ya nchi yetu. Bwana Karugendo hajapatapo kusema kweli kama alivyosema maneno hayo. Kweli kitabu hiki kimevuruga historia ya nchi yetu. Kitabu hiki kilipochapwa London mwaka wa 1998 na kikaanza kusomwa palipita kishindo. Nini kilisababisha kishindo hiki? Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ilikuwa imekwishaandikwa na ikifahamika. Lakini historia zote hizo zilikuwa na kasoro moja kubwa sana. Historia hizi zilikuwa hazitaji jina la ukoo wa Sykes. Hawa akina Sykes wana umuhimu gani katika historia ya Tanganyika? Sasa hapa itakubidi usafiri urudi nyuma wakati Tanganyika inatawaliwa na Wajerumani. Kamanda Herman Von Wissman alikwenda Msumbiji kutafuta askari mamluki kuja Tanganyika kusaidia jeshi la Wajerumani waliokuwa wanapigana na wananchi wa Tanganyika. Pangani wakipambana na Abushiri bin Salim na Iringa wakipambana na Chief Mkwawa. Hivi ndivyo babu yake Abdulwahid Sykes, Sykes Mbuwane alivyoingia Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1800 na Kleist akazaliwa Pangani mwaka wa 1894. Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 aliandika maisha yake na huu mswada ukaja kujumuishwa katika kitabu alichohariri John Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichochapwa mwaka wa 1973 kutokana na Seminar Paper ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliyoandika mjukuu wake, Aisha ‘’Daisy,’’ Sykes mwaka wa 1968 (A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
 
Umesomeka mkuu.
Icebreaker,
Hawa hapo chini ni akina mama waliomsindikiza Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere
Uwanja wa Ndege safari yake ya kwanza UNO mwaka wa 1955.

TATU BINT MZEE.JPG

Kulia: Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed na wa kwanza kushoto ni Bi. Chiku bint Said Kikusa (Mama Sakina).

Haya majina Bwana Karugendo yanamkera hapendi kuyasoma katika historia niliyoandika.
Padri masikini ya Mungu hajui kuwa hawa shangazi zangu ndiyo walikuwa mashoga wa
Mama Maria Nyerere katika siku zile ngumu za kupigania uhuru Mama Maria akiendesha
duka la mafuta ya taa Mtaa wa Livingstone na Mchikichi si mbali na nyumbani kwa Bi. Chiku
Kikusa.

Masikini ya Mungu Bwana Karugendo hajui kuwa hawa akina mama ndiyo walioipa nguvu TANU kwa
mahudhurio ya mikutano na nyimbo zao za lelemama zilizohamasisha wengi kujiunga na
TANU na kumuunga mkono Mwalimu Nyerere.

Historia hii yeye anasema Mohamed Said anapotosha.
Angependa ibaki historia ambazo wazalendo hawa hawakutajwa.

Aisha Daisy Sykes binti yake Abdul Sykes anakumbuka nyakati hizi yeye akiwa mtoto
mdogo na anaandika:

''...nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na
shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika
mikutano yao ya TANU.

Nakumbuka vizuri sana jinsi baba alikvyokuwa karibu sana na Mwalimu Sakina na ndugu yake
Mwalimu Fatna (wote hawa watoto wa Mama Sakina), na jinsi alivyowaleta ndugu hawa karibu
na Mama Maria na hawa wakamjulisha Mama Maria Nyerere kwa mama yao na mashoga zake
Bi Hawa Maftaha, Bibi Titi Mohamed na Bi Tatu binti Mzee.''
 
Hii mambo haiwezi kuisha kila mtu anataka ajulikane kuwa alichangia ktk Uhuru wa Tanganyika. Nimeona MS na Karugendo wote mkitaja ndugu zenu wa damu au wenye nasaba na nyinyi ktk ukombozi wa kisiasa waTanganyika. Mimi pia nina babu zangu walishiriki wakitokea pande za kaskazini, walipigana na mjerumani na baadae ktk ukoloni. Je sasa nianze Ku force their recognition ktk vitabu vya historia vya nchi yetu kuwa viwaandike babu zangu hawa? Hasha! Kwa upande wangu nikiona Uhuru najua si tokeo la nguvu za mtu mmoja ila ni mkusanyiko wa watu na matukio mengi yaliyotendwa kwa imani moja ya kumuondoa mvamizi na mkoloni. Ila hili la kutaka ulazima wa kutambulika kwa familia fulani kama ndiyo iliyoleta Uhuru peke yake si jambo jema. Wengine tuishie kuwatambua tu formerly bila migongano itakayoleta kutoelewana tukajikuta hata hao waliopigana kwa ajili yetu watusikitikie kwa tuyafanyayo kwa kutanguliza koo au jamaa zetu mbele na si utaifa
 
JIBU LA PADRI KARUGENDO

Hiyo hapo juu ni barua aliyoniandikia Padri akinilaumu kwa kuandika kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.’’Padri amenishtumu kwa ‘’kuvuruga,’’ historia ya nchi yetu. Padri hajapatapo kusema kweli kama alivyosema maneno hayo. Kweli kitabu hiki kimevuruga historia ya nchi yetu. Kitabu hiki kilipochapwa London mwaka wa 1998 na kikaanza kusomwa palipita kishindo. Nini kilisababisha kishindo hiki? Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ilikuwa imekwishaandikwa na ikifahamika. Lakini historia zote hizo zilikuwa na kasoro moja kubwa sana. Historia hizi zilikuwa hazitaji jina la ukoo wa Sykes. Hawa akina Sykes wana umuhimu gani katika historia ya Tanganyika? Sasa hapa itakubidi usafiri urudi nyuma wakati Tanganyika inatawaliwa na Wajerumani. Kamanda Herman Von Wissman alikwenda Msumbiji kutafuta askari mamluki kuja Tanganyika kusaidia jeshi la Wajerumani waliokuwa wanapigana na wananchi wa Tanganyika. Pangani wakipambana na Abushiri bin Salim na Iringa wakipambana na Chief Mkwawa. Hivi ndivyo babu yake Abdulwahid Sykes, Sykes Mbuwane alivyoingia Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1800 na Kleist akazaliwa Pangani mwaka wa 1894. Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 aliandika maisha yake na huu mswada ukaja kujumuishwa katika kitabu alichohariri John Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichochapwa mwaka wa 1973 kutokana na Seminar Paper ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliyoandika mjukuu wake, Aisha ‘’Daisy,’’ Sykes mwaka wa 1968 (A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
Nafikiri Padre Privatus Karugendo hausikina uzi huu, maana kama nimesoma vizuri jibu limetolewa na Bwana Prudence Karugendo. Padre Privatus Karugendo na Bwana Prudence Karugendo ni watu wawili tafauti japo ni mtu na kakaye.
 
mzee wangu Mohamed Said heshima yako,
unaweza ukawa sahihi kwenye zako hili kwakuwa mimi si mjuvi wa haya mambo siwezi kubisha.
- point yangu nimeona kasoro ktk majina ya unaemjibu ambaye ni PRUDENCE KARUGENDO Kwako Ww Umempa Nyadhifa Ya UPADRI Ambayo Hajawahi Kuwa Nayo!
- Labda Tuseme Ulitaka Kumaanisha PADRI PRIVATUS KARUGENDO Ambaye Ni Kaka Yake? Ambaye Pia Alishaacha Upadri Huo Ingawa Bado Anatambulika Kama Padri.
 
Remote,
Usiwe na wasiwasi sote sisi hapa ni wanafunzi tunajifunza zungumza
bila hofu.

Nashukuru kwa kunifahamisha ninayemjibu ni Prudence Karugendo.
Nafanya nafanya masahihisho.
 
Nafikiri Padre Privatus Karugendo hausikina uzi huu, maana kama nimesoma vizuri jibu limetolewa na Bwana Prudence Karugendo. Padre Privatus Karugendo na Bwana Prudence Karugendo ni watu wawili tafauti japo ni mtu na kakaye.
Bullet.
Nimefahamishwa kuhusu hawa ndugu wawili na narekebisha.
Nakushukuru kwa kunisahihisha.
 
Hii mambo haiwezi kuisha kila mtu anataka ajulikane kuwa alichangia ktk Uhuru wa Tanganyika. Nimeona MS na Karugendo wote mkitaja ndugu zenu wa damu au wenye nasaba na nyinyi ktk ukombozi wa kisiasa waTanganyika. Mimi pia nina babu zangu walishiriki wakitokea pande za kaskazini, walipigana na mjerumani na baadae ktk ukoloni. Je sasa nianze Ku force their recognition ktk vitabu vya historia vya nchi yetu kuwa viwaandike babu zangu hawa? Hasha! Kwa upande wangu nikiona Uhuru najua si tokeo la nguvu za mtu mmoja ila ni mkusanyiko wa watu na matukio mengi yaliyotendwa kwa imani moja ya kumuondoa mvamizi na mkoloni. Ila hili la kutaka ulazima wa kutambulika kwa familia fulani kama ndiyo iliyoleta Uhuru peke yake si jambo jema. Wengine tuishie kuwatambua tu formerly bila migongano itakayoleta kutoelewana tukajikuta hata hao waliopigana kwa ajili yetu watusikitikie kwa tuyafanyayo kwa kutanguliza koo au jamaa zetu mbele na si utaifa
James,
Ikiwa ipo historia itakuwapo historia na utaweza kuandika kitu cha kusomeka.
Hakuna tatizo katika hili wala hakuna ubaya wowote.

Huna historia huwezi kuandika kitu kisichokuwapo.
 
Alichoongea James Comey hapo juu kina usahihi. Hapa naona kama kuna udini unatakiwa kujadiliwa sana. Tungeishia hapa. Baba angu Mohameid Said umekuwa ukikosolewa sana kwenye maandiko yako. Hongera hukati tamaa, lakini nafikiri usipende kujibu mijadala inayoonekana kama ina udini
Nyasirori,
Hainipi shida kujibu chochote yote hayo ni sehemu ya matatizo ya historia
ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Niko hapa kueleza ukweli ninaoujua kuhusu historia ya TANU ili watu wajue
nini walifanya waliotutangulia na tuwaidhike na tujifunze.
 
Bullet,
Amin kwa sote.
Huna lolote la kusema katika majibu niliyompa Bwana Karugendo?
Hakuna jipya ambalo wewe hukuwa unaliijua?
Nilinunua kitabu chako kinachoelezea yote hayo, Pia aliyoyaandika Bwana Karugendo kweli mengine yalikuwa mapya kwangu,ila tunafundishwa kwamba elimu ni bahari, haina mwisho. Andiko lako limeniongezea kitu,hali kadharika andiko la Bwana Karugendo.
Mfano sikujua kwamba Dr.Kyaruzi hakuwamo kwenye kamati ya kwanza ya TANU
 
Nafikiri Padre Privatus Karugendo hausikina uzi huu, maana kama nimesoma vizuri jibu limetolewa na Bwana Prudence Karugendo. Padre Privatus Karugendo na Bwana Prudence Karugendo ni watu wawili tafauti japo ni mtu na kakaye.
Uko sawa hawa ni watu wawili tofauti ingawa ni ndugu.
 
JIBU LA BWANA KARUGENDO

Hiyo hapo juu ni barua aliyoniandikia Bwana Karugendo akinilaumu kwa kuandika kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.’’Padri amenishtumu kwa ‘’kuvuruga,’’ historia ya nchi yetu. Bwana Karugendo hajapatapo kusema kweli kama alivyosema maneno hayo. Kweli kitabu hiki kimevuruga historia ya nchi yetu. Kitabu hiki kilipochapwa London mwaka wa 1998 na kikaanza kusomwa palipita kishindo. Nini kilisababisha kishindo hiki? Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ilikuwa imekwishaandikwa na ikifahamika. Lakini historia zote hizo zilikuwa na kasoro moja kubwa sana. Historia hizi zilikuwa hazitaji jina la ukoo wa Sykes. Hawa akina Sykes wana umuhimu gani katika historia ya Tanganyika? Sasa hapa itakubidi usafiri urudi nyuma wakati Tanganyika inatawaliwa na Wajerumani. Kamanda Herman Von Wissman alikwenda Msumbiji kutafuta askari mamluki kuja Tanganyika kusaidia jeshi la Wajerumani waliokuwa wanapigana na wananchi wa Tanganyika. Pangani wakipambana na Abushiri bin Salim na Iringa wakipambana na Chief Mkwawa. Hivi ndivyo babu yake Abdulwahid Sykes, Sykes Mbuwane alivyoingia Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1800 na Kleist akazaliwa Pangani mwaka wa 1894. Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 aliandika maisha yake na huu mswada ukaja kujumuishwa katika kitabu alichohariri John Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichochapwa mwaka wa 1973 kutokana na Seminar Paper ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliyoandika mjukuu wake, Aisha ‘’Daisy,’’ Sykes mwaka wa 1968 (A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
Mkuu Maalim Mohamed Said, asante kwa hii.

P.
 
Back
Top Bottom