Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Icebreaker,Umesomeka mkuu.
Nafikiri Padre Privatus Karugendo hausikina uzi huu, maana kama nimesoma vizuri jibu limetolewa na Bwana Prudence Karugendo. Padre Privatus Karugendo na Bwana Prudence Karugendo ni watu wawili tafauti japo ni mtu na kakaye.JIBU LA PADRI KARUGENDO
Hiyo hapo juu ni barua aliyoniandikia Padri akinilaumu kwa kuandika kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.’’Padri amenishtumu kwa ‘’kuvuruga,’’ historia ya nchi yetu. Padri hajapatapo kusema kweli kama alivyosema maneno hayo. Kweli kitabu hiki kimevuruga historia ya nchi yetu. Kitabu hiki kilipochapwa London mwaka wa 1998 na kikaanza kusomwa palipita kishindo. Nini kilisababisha kishindo hiki? Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ilikuwa imekwishaandikwa na ikifahamika. Lakini historia zote hizo zilikuwa na kasoro moja kubwa sana. Historia hizi zilikuwa hazitaji jina la ukoo wa Sykes. Hawa akina Sykes wana umuhimu gani katika historia ya Tanganyika? Sasa hapa itakubidi usafiri urudi nyuma wakati Tanganyika inatawaliwa na Wajerumani. Kamanda Herman Von Wissman alikwenda Msumbiji kutafuta askari mamluki kuja Tanganyika kusaidia jeshi la Wajerumani waliokuwa wanapigana na wananchi wa Tanganyika. Pangani wakipambana na Abushiri bin Salim na Iringa wakipambana na Chief Mkwawa. Hivi ndivyo babu yake Abdulwahid Sykes, Sykes Mbuwane alivyoingia Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1800 na Kleist akazaliwa Pangani mwaka wa 1894. Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 aliandika maisha yake na huu mswada ukaja kujumuishwa katika kitabu alichohariri John Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichochapwa mwaka wa 1973 kutokana na Seminar Paper ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliyoandika mjukuu wake, Aisha ‘’Daisy,’’ Sykes mwaka wa 1968 (A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
Remote,mzee wangu Mohamed Said heshima yako,
unaweza ukawa sahihi kwenye zako hili kwakuwa mimi si mjuvi wa haya mambo siwezi kubisha.
- point yangu nimeona kasoro ktk majina ya unaemjibu ambaye ni PRUDENCE KARUGENDO Kwako Ww Umempa Nyadhifa Ya UPADRI Ambayo Hajawahi Kuwa Nayo!
- Labda Tuseme Ulitaka Kumaanisha PADRI PRIVATUS KARUGENDO Ambaye Ni Kaka Yake? Ambaye Pia Alishaacha Upadri Huo Ingawa Bado Anatambulika Kama Padri.
Bullet.Nafikiri Padre Privatus Karugendo hausikina uzi huu, maana kama nimesoma vizuri jibu limetolewa na Bwana Prudence Karugendo. Padre Privatus Karugendo na Bwana Prudence Karugendo ni watu wawili tafauti japo ni mtu na kakaye.
James,Hii mambo haiwezi kuisha kila mtu anataka ajulikane kuwa alichangia ktk Uhuru wa Tanganyika. Nimeona MS na Karugendo wote mkitaja ndugu zenu wa damu au wenye nasaba na nyinyi ktk ukombozi wa kisiasa waTanganyika. Mimi pia nina babu zangu walishiriki wakitokea pande za kaskazini, walipigana na mjerumani na baadae ktk ukoloni. Je sasa nianze Ku force their recognition ktk vitabu vya historia vya nchi yetu kuwa viwaandike babu zangu hawa? Hasha! Kwa upande wangu nikiona Uhuru najua si tokeo la nguvu za mtu mmoja ila ni mkusanyiko wa watu na matukio mengi yaliyotendwa kwa imani moja ya kumuondoa mvamizi na mkoloni. Ila hili la kutaka ulazima wa kutambulika kwa familia fulani kama ndiyo iliyoleta Uhuru peke yake si jambo jema. Wengine tuishie kuwatambua tu formerly bila migongano itakayoleta kutoelewana tukajikuta hata hao waliopigana kwa ajili yetu watusikitikie kwa tuyafanyayo kwa kutanguliza koo au jamaa zetu mbele na si utaifa
Nyasirori,Alichoongea James Comey hapo juu kina usahihi. Hapa naona kama kuna udini unatakiwa kujadiliwa sana. Tungeishia hapa. Baba angu Mohameid Said umekuwa ukikosolewa sana kwenye maandiko yako. Hongera hukati tamaa, lakini nafikiri usipende kujibu mijadala inayoonekana kama ina udini
Asante kwa masahihisho. Mungu akubariki sana.Bullet.
Nimefahamishwa kuhusu hawa ndugu wawili na narekebisha.
Nakushukuru kwa kunisahihisha.
Asante kwa masahihisho. Mungu akubariki sana.
Bullet,Asante kwa masahihisho. Mungu akubariki sana.
Nilinunua kitabu chako kinachoelezea yote hayo, Pia aliyoyaandika Bwana Karugendo kweli mengine yalikuwa mapya kwangu,ila tunafundishwa kwamba elimu ni bahari, haina mwisho. Andiko lako limeniongezea kitu,hali kadharika andiko la Bwana Karugendo.Bullet,
Amin kwa sote.
Huna lolote la kusema katika majibu niliyompa Bwana Karugendo?
Hakuna jipya ambalo wewe hukuwa unaliijua?
Uko sawa hawa ni watu wawili tofauti ingawa ni ndugu.Nafikiri Padre Privatus Karugendo hausikina uzi huu, maana kama nimesoma vizuri jibu limetolewa na Bwana Prudence Karugendo. Padre Privatus Karugendo na Bwana Prudence Karugendo ni watu wawili tafauti japo ni mtu na kakaye.
Bali...Uko sawa hawa ni watu wawili tofauti ingawa ni ndugu.
Mkuu Maalim Mohamed Said, asante kwa hii.JIBU LA BWANA KARUGENDO
Hiyo hapo juu ni barua aliyoniandikia Bwana Karugendo akinilaumu kwa kuandika kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.’’Padri amenishtumu kwa ‘’kuvuruga,’’ historia ya nchi yetu. Bwana Karugendo hajapatapo kusema kweli kama alivyosema maneno hayo. Kweli kitabu hiki kimevuruga historia ya nchi yetu. Kitabu hiki kilipochapwa London mwaka wa 1998 na kikaanza kusomwa palipita kishindo. Nini kilisababisha kishindo hiki? Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ilikuwa imekwishaandikwa na ikifahamika. Lakini historia zote hizo zilikuwa na kasoro moja kubwa sana. Historia hizi zilikuwa hazitaji jina la ukoo wa Sykes. Hawa akina Sykes wana umuhimu gani katika historia ya Tanganyika? Sasa hapa itakubidi usafiri urudi nyuma wakati Tanganyika inatawaliwa na Wajerumani. Kamanda Herman Von Wissman alikwenda Msumbiji kutafuta askari mamluki kuja Tanganyika kusaidia jeshi la Wajerumani waliokuwa wanapigana na wananchi wa Tanganyika. Pangani wakipambana na Abushiri bin Salim na Iringa wakipambana na Chief Mkwawa. Hivi ndivyo babu yake Abdulwahid Sykes, Sykes Mbuwane alivyoingia Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1800 na Kleist akazaliwa Pangani mwaka wa 1894. Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 aliandika maisha yake na huu mswada ukaja kujumuishwa katika kitabu alichohariri John Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichochapwa mwaka wa 1973 kutokana na Seminar Paper ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliyoandika mjukuu wake, Aisha ‘’Daisy,’’ Sykes mwaka wa 1968 (A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).