Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Status
Not open for further replies.

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145


Kwanza napenda ifahamike kuwa dhumuni la kuipandisha clip hii hapa ni kumpinga huyo anaejiita "Sungura Media" aliyeipandisha clip hii youtube na kuandika kuwa eti ni "video ya siri". Haya mafundisho ya historia ya Alama Mohamed Said siyo siri, yapo mtandaoni, yapo kwenye tovuti yake na yameshajadiliwa sana hapa JF.

Mfahamu Alama Mohamed Said:

Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe 25 Februarikatika mwaka wa 1952 huko Gerezani jijini Dar es Salaam - ambapo ndiko kulikokuwa na asili ya upinzani dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini Tanganyika katika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways. Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa Nyerere kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere. Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika Chuo Kikuu cha Wales huko mjini [[Cardiff, Uingereza na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).


Utafiti juu ya historia ya uhuru wa TangayikaEdit

Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi. Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa. Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).


Tazama piaEdit



Viungo vya Nje

Chanzo: https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Mohamed_Said

cc: Mohamed Said
 
Kama Nyerere aliua Uislam kweli Tanzania
Basi aliona mbali sana

Maana nikiona demand wanazotaka Waislam huku Tz Bara halafu ukilinganisha na wanachowafanyia wasio Waislam kule Zanzibar, utaona kabisa hawa watu wakiwa na nguvu sana lazima amani ya nchi itatetereka tu au watajaribu ku Islamize nchi nzima

Waislam mtaona kama nina chuki na nyie ila huu ni ukweli unaouma mtanisamehe

Mfano, India na Pakistan zilikuwa nchi moja chini ya utawala wa Mwingereza, ila kutokana na demand za Waislam na vurugu zao ikabidi waigawe iwe nchi Mbili, Waislam wakaenda Pakistan, Wahindu wakabaki India

Pakistan leo hii wote tunajua ni nchi ya aina gani
 
muafi, Una historia mbadala wa iliyoletwa hapo? Umeusikiliza mkanda?

Hilo la "mafala" Kwa upande wangu hujakosea, mimi ni falah.

"Fala" ni neno linalotokana na neno la Kiarabu "falah" likimaanisha "peasant" Kwa Kiswahili "mkulima mdogo" au "mshamba". Karibu kwetu shamba.

Kwa upande wa Alama Mohamed Said nimekuwekea ukurasa wa wikipedia unaomuelezea, sidhani kama ana "qualify" kuwa fala.
 
Kuwa chini ya hawa wenye imani hiyo ni kukataa amani, kama huamini basi unauliwa na si vinginevyo.

Wenyeji wa ulaya wameingiliwa ustaarabu wao amani yao, na hayo maendeleo ya ulaya yanavurugwa muda si mrefu.

Historia si vibaya kuijua lkn swala la kuua udini lilikuwa la msingi mno, tusingekuwa taifa moja leo. Nyerere alifanikiwa vizuri.
 
Kuwa chini ya hawa wenye imani hiyo ni kukataa amani, kama huamini basi unauliwa na si vinginevyo.
Wenyeji wa ulaya wameingiliwa ustaarabu wao amani yao, na hayo maendeleo ya ulaya yanavurugwa muda si mrefu.
Historia si vibaya kuijua lkn swala la kuua udini lilikuwa la msingi mno, tusingekuwa taifa moja leo. Nyerere alifanikiwa vizuri.
Mada ni TANU, unaweza Kumpinga njoo upinge, mada iko wazi. Tuletee historia mbadala.
 
Nyerere alibebwa na Waislam kufika alipofika kisha akawageuka Bibi Titi Mohammed alimfunga kifungo cha maisha kwa kupingana nae baada kumuona ameageuka.

Jina la Bibi Titi likaondoshwa katika historia ya wanaharakati walio dai UHURU wa Tangannyika.

Mwinyi kwa kuujua ukweli ndio aliekuja kumwachia huru na angalau akapewa jina la Mtaa mmoja kama kumbukumbu ya juhudi yake.

Takadiri (ambae mchonga akampachika jina la MTAKADINI)
Vilevile ni mfano mwengine wa wahanga hawa wapo wengi.
 
Sheikh Said Abdallah
Mkuu Dada yangu, nikuzimiaye, Faiza Foxy, kwanza asante kutuletea hii clip ya Redio Kheri, yenye maurongo wa Mzee wetu na member mwenzetu Maalim Mohamned Said, maana bila wewe kuileta humu, akina sisi, tusingejua jinsi mnavyodanganyana humo na kufanya uchochezi kwenye hizo redio zenu za dini!.

Kwa kuanzia tuu, kuanzia headline ya bandiko hili ni urongo, Tanu hakijawahi kuwa ni chama cha Kiislamu, kuanzia kuasisiwa kwake, hakuna Muislamu yoyote aliwahi kuasisi chama chochote cha kupigania uhuru wa Tanganyika, Tanu ilitokana na TAA, ambayo ilitokana na AA. Muasisi wa AA ni Mkristo Cecil Kalaghe, muasisi wa TAA ni Mkristo Dr. Kyaruzi, na muasisi wa Tanu ni Mkristo Mwl. Julius Kambarage Nyerere, tangu AA, TAA hadi TANU, hakuna wakati wowote vyama hivi viliwahi kuwa vya dini fulani, ila kitu ambacho ni kweli, Tanu ilimuwa na members wengi Waislamu kuliko Wakristu, ila nguvu ya chama chochote ni logistical support, mfadhili mkuu wa Tanu ni Mkristo tajiri Mzee John Rupia, na sio wale masikini wa Gerezani japo pia tusiudharau mchango wao wa senti 5 ya samaki, senti 10,senti 20 ya mbuni, thumuni ya sungura, na shilingi ya mwenge, enzi hizo, noti ni ya shilingi 5, 10,20, 50 na noti kubwa ilikuwa Sh.100 ya masai.

Nimeisikiliza yote nikakuta ...Du...!, mnapigwa kamba kweli kweli na Mzee wetu huyu...
huu ni muendelezo wa ule ule urongo wa siku zote wa uchochezi wa udini, kusingizia kitu cha urongo marehemu kina karma kali sana!.

Japo namheshimu sana Maalim Mohammed Said, kitu pekee mimi ninachotofautiana nae ni matumizi ya takwimu za urongo ili kupush forward agenda zake ovu za uchochezi wa udini.

Kwenye mahojiano hayo, ameongopa kuwa 76% ya wabunge wa Bunge la JMT, ni Wakatoliki,18% madhehebu mengine ya Kikristu yaliyobakia, halafu Waislamu ni just 6%!. Huu ni urongo wa kiwango cha lami mchana kweupe. Mtu huhitaji kufanya sensa ya Wabunge Waislamu kujua huu ni urongo, bila hata sensa, Wabunge wote kutoka Zanzibar ni Waislamu ambao kabla hujawajumlisha wabunge Waislamu wa bara, hao Wanzibar tuu wenyewe wanafanya theluthi moja ya Wabunge wote!. Huu ni urongo!.

Hata kwa kutumia tuu just ordinary common sense, inakuja kweli akilini, 76% ya wabunge wakawa ni Wakatoliki?!,this doesnt make sense to me, this is non sense, just bull shit!.
(ashakum for this)

Ukiwa na asilimia 99% ya ukweli, na just 1% ya urongo, huo urongo una nullify ukweli wote wa hoja zake kuzifanya null and void ab initio.

P.
 
Kama hayo ndiyo yalikuwa malengo ya Waislamu wa kabla ya Uhuru basi Nyerere alishauriwa Veena Sana na kanisa katoliki. Yaani Waislamu walitaka waingize mfumo Islam na kuifanya nchi iwe typical Muslim state. Khaa. Huu ulikuwa ni mpango wa Mungu
 
Kama Nyerere aliua Uislam kweli Tanzania
Basi aliona mbali sana

Maana nikiona demand wanazotaka Waislam huku Tz Bara halafu ukilinganisha na wanachowafanyia wasio Waislam kule Zanzibar, utaona kabisa hawa watu wakiwa na nguvu sana lazima amani ya nchi itatetereka tu

Huu ni ukweli unaouma na Waislam mtanisamehe
Umeandika UKWELI MTUPU.

Nyerere alifanya la maana sana.


Wallah Wabillah.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom