Mag3,
Unaandika huku umeghadhibika na ukiwa na hamaki hata akili haiwezi
kufikiri vyema hadi umetulia.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo ndiyo historia yake
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere iliandikwa na waandishi wengi
kabla yangu -
Kimambo, Kandoro, Barongo, Chuo Cha CCM Kivukoni na
watafiti wa nje halikadhalika.
Bahati mbaya historia hizo ilikuwa na upungufu mkubwa sana na ndipo mimi
nikaiandika historia hii kwa kutumia
Nyaraka za Sykes ambao historia yao
katika siasa za Waafrika wa Tanganyika zinaanza mwanzoni karne ya 20 na
ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kuasisi TANU na harakati dhidi ya
ukoloni wa Muingereza.
Watafiti walionitangulia mimi hakuna aliyepata fursa ya kuzisoma nyaraka hizi
wala kuwahoji wenye nyaraka hizi.
Kitabu kilipotoka mwaka wa 1998 hakika kiliwashtua wengi kwa kule kutambua
kuwa historia waliyokuwa wakiiamini kuwa ndiyo historia ya kweli ya TANU na
uhuru wa Tanganyika ilikuwa na mashimo mengi yasiyo na hesabu.
Matokeo yake kitabu kilipata review tatu kutoka mabingwa wa African History
kwenye Cambridge Journal of African History waandishi wakiwa John Iliffe,
Jonathan Glassman na James Brennan.
The East African Magazine (Nairobi) ikatoa ''serialisation'' tatu za kitabu
Business Times nao pia wakaandika '' review,'' ya kitabu hiki.
Haya nishayaeleza huko nyuma lakini nayarudia kwa kuwa somo hili kila
siku linavutia wasomaji wapya.
Kubwa katika yale yanayoshughulisha akili za wengi ni mchango wa Waislam
katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hiki ndicho kinachomuunguza
Mag3.
Kitabu kina kwenda toleo la nne Kiswahili na la tatu Kiingereza.
Mag3 historia hii si santuri inayochuja hii ni mfano wa picha ya ''Mona Lisa,'' au
ukipenda sawa na nyimbo, ''Besame Mucho.''
Kutokana na kitabu hiki nikatiwa katika mradi wa vitabu vya historia kwa mashule
chini ya Oxford University Press Nairobi na nikaandika kitabu kimoja: ''The Torch
on Kilimanjaro,'' na nikashirikishwa kwenye mradi mwingine, Dictionary of African
Biography (DAB) Oxford University Press, New York mradi chini ya Harvard.
View attachment 1119899
Hawa wote hawakuona udini ila
Mag3.
Kutokana na kusahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika nimealikwa kwingi duniani
kuzungumza pamoja na Northwestern University, Marekani wanaoongoza duniani
katika African History.
Hawa wote hawakuona udini ila
Mag3.
Mag3 anaita haya porojo na ngano na udini.
Mag3 anadhani yeye anajua kushinda hawa wote wanaonitandikia busati kwao nikae
nizungumze na wataalamu wao achilia mbali wachapaji vitabu (publishers) waliotoa
vitabu nilivyoandika.
Kuna mengine sikuyajibu kwani hayana maana na mimi siwezi kukosa adabu kuandika
matusi na kashfa.