Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Status
Not open for further replies.

Mwanamume kuolewa na mwanamume mwenzake unaona ndiyo maendeleo huko Ulaya?
 
pkuhusu bunge mwaka 2000 baada ya waislam wengi kushinda kura za maoni ubunge,mchakato ukarudiwa kwa hoja zisizo na mashiko,makada wa msalaba walifurahi na kutamba kwamba tumewafyeka waislam,hebu tupe takwimu za dini bungeni
They say numbers don't lie, Maalim Mohammed Said, can lie on an anything else but not in numbers. Bunge la JMT lina jumla ya Wabunge, 441, kati yao, wabunge wakuchaguliwa kutoka majmboni ni 364 na Viti maalum 87, na 10 ni wakuteuliwa na rais.

Wabunge wote wa Zanzibar ni Waislamu, ndani ya Bunge la JMT, kuna wabunge 50 wa majimbo kutoka Zanzibar, na wabunge 20 wa viti maalum. Jumla 70.

Hapa bara kuna wabunge wa Muslim dominated areas hawajawahi kuwa Wakristu, rough estimates ni majimbo 50, Ukijumlisha na 30 wa viti maalum bara tuna raugh estimates ya 170/441 ambayo ni zaidi ya 40%, akitokea mtu akawalisha urongo kuwa Bunge la JMT lina Wakatoliki 76% na Waislamu just 6%!, this pure nonsense!, and this person must be mad!. Na kukitokea Waislamu wakuamini urongo huu, they seriously need their heads be examined!.
P
 

Same old fake stories, same pomposity...
different thread, different day.
 
Oxx,
Ninaposema TANU kilikuwa chama cha Waislam maana yangu ni
kuwa jihudi kubwa ya kuanzisha chama hicho ilitokana na Waislam.

Inahitaji uijue historia ya TANU kuelewa hili,

Uislam wakati wa kupigania uhuru ndiyo itikadi iliytumika kupambana
na dhulma za ukoloni.

Uislam ukatumika kuwaunganisha wananchi wote dhidi ya ukoloni na
mkakati huu ulifanikiwa sana.
Oxx,
Historia hii inawatisha wengi kusema kuwa TANU ilianzishwa kutokana na juhudi
kubwa ya Waislam.

Ukiisoma historia ya TANU ile historia ya kweli si historia ya Chuo Cha Kivukoni
utashangaa na bila shaka utajiuliza kuwa kwa nini historia hii ni tofauti na hii
inayofundishwa na ndiyo iliyo rasmi.

Mwaka wa 1953 miezi michache kabla ya uchaguzi wa TAA Abdul Sykes alikwenda
Nansio wa Hamza Mwapachu akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul
Islamiyya fi Tanganyika.

Ulifanyika mkutano Abdul akitaka kupata kauli ya mwisho ya Mwapachu kuwa ampishe
Nyerere kwenye nafasi ya urais wa TAA na uchaguzi wa TAA wa 1954 waunde TANU
na kudai uhuru wa Tanganyika.

Mwapachu akamwambia Abdul kuwa amsaidie Nyerere kuchukua uongozi wa TAA kwani
kama Abdul atasimama na Nyerere kwa nia ya Abdul kushinda uchaguzi ule, Nyerere
asingeweza kumshinda Abdul katika hali ya siasa za Dar es Salaam ile ya 1950s.

Wote kati ya wale wazalendo watatu walikuwa wanajua kuwa Nyerere alifaa Zaidi kuongoza
harakati za uhuru kuliko Abdul.

Lakini kubwa ambalo Hamza Mwapachu alilosema kumwambia Abdul ni kuwa yeye kama
Muislam ataongoza TANU kudai uhuru, itaonekana ni harakati zingine za Waislam baada
ya vita vya Maji Maji kutaka kusababisha machafuko.

TANU ikiwa na kiongozi Mkristo hii litaonekama ni harakati za wananchi wote wa Tanganyika
kudai uhuru wao.

Uchaguzi ule uliofanyika tarehe 17 Aprili 1953 katika Ukumbi wa Arnautoglo ndiyo uliomtia
Nyerere katika uongozi wa TAA 1953 lakini alishinda kwa kura chache sana.

Kufuatia uchaguzi huu hawa wafuatao ndiyo wakawa viongozi wa TAA mwaka wa 1953:

J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary;
Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer na
Ally K. Sykes akiwa Assistant Treasurer. Wajumbe wengine Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa
Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo
na Patrick Aoko.
[1]


Oxx,
Umewahi kuisoma popote historia hii?
Au ulikuwa unaijua kabla ya mimi kukueleza hapa?

[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
 
Same old fake stories, same pomposity...
different thread, different day.
Nanren,
Ikiwa hizo ndizo fikra zako sawa hakuna neno ila mimi nitawaeleza wasomaji kile
nikijuacho katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
 
Watu badala ya kujadili hoja iliyopo mezani mnawajadili akshababu,is,boko haram na nk . hii mada hamjaielewa mmekurupuka.
 
Umejazwa ujinga na ukakujaa. Uislam ni salama kabisa.
Unaposema ni salama wewe unaishi dunia gani?! Hivi unaona vitu ambavyo ISIS wamefanya huko mashariki ya kati, Vipi kuhusu Alshabaab, Boko Haramu, Al qaeda na wengineo?! Usalama ni kukata watu vichwa kama vile kuchinja kuku! Kujitoa muhanga! N.k. Hakuna usalama wowote.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…