Mohamed Salah: Sidhani kama sisi ni mwiongoni mwa timu zinazotarajiwa kushinda AFCON

Mohamed Salah: Sidhani kama sisi ni mwiongoni mwa timu zinazotarajiwa kushinda AFCON

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah amesema timu yake haipo miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kushinda Kombe la AFCON, lakini amesisitiza kuwa watapambana kwa nguvu zote ili kufika hatua za juu zaidi za mashindano hayo yanayofanika Morocco.

Salah, ambaye ni mshambuliaji wa Liverpool, alifunga bao la tatu na kuihakikishia Misri nafasi ya kufuzu robo fainali baada ya ushindi mgumu dhidi ya Benin siku ya Jumatatu.

Mechi hiyo iliisha kwa mabao 3-1 baada ya kuongezwa kwa muda wa ziada.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alisema hakuna mechi rahisi katika AFCON.

“Viwango vya timu vinakaribiana; niliwaambia wenzangu jana kuwa hakuna timu inayofungwa mabao manne au matano. (Benin) wana timu nzuri na kocha mzuri… ninafurahi kwamba hatimaye tuliweza kushinda.” Alisema Salah.
1767692997270.png
 
Hilo asahau, Morroco, Nijeria na Senegal wanaweza kunyanyua kwapa

Morocco tunaenda kubeba hii kitu, ila Algeria tusimchukulie poa.

Hao wakina senegal hawafiki popote

Kila la heri kwao Morocco 🇲🇦 au Algeria 🇩🇿
 
Mbona naona wale Ivory coast ndio watabe mno anyway nadhani Nigeria au ivory coast mmoja anachukua bila kumsahau algeria kwa mbali
1.Ivory coast
2.Nigeria
3.Senegal
4.Algeria
 
Labda yule refa aliyechezesha mechi ya Stars vs Morocco achezeshe mechi zote za Morocco zilizobaki.

Sioni kama kulikua na penati hapa sheikh, angalia vizuri kabla hajasukumwa alikua tayari amejiangusha
 
Back
Top Bottom