Kulikuwa na uvumi kuwa klabu ya Simba kuachana na kocha wa klabu hiyo, Pablo Franco Martín kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu ya timu na kufungwa na Yanga katika nusu fainali la kombe la FA. Kumekuwa na taarifa kuwa Mohammed Adil Erradi, amefika Dar kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mabosi wa Simba huku akiwa ameomba ruhusa ya mapumziko katika klabu yake.
- Tunachokijua
- Taarifa hii kumetokana na moja wa wafanyakazi wa APR kutangaza kushtushwa kwa kuondoka kwa kocha huyo kimyakimya ikiaminika kuwa na mipango ya kusajiliwa na Simba.
Hata hivyo, Simba SC hawakutoa taarifa yoyote juu ya ujio wa kocha mpya kutoka Rwanda badala yake Juni 28, 2022 kupitia ukurasa wa Twitter na Instagram klabu ya Simba walitangaza kumsajli kocha mkuu, Zoran Manojlovic baada ya kumalizana na kocha wa kihispania Pablo Franco Martín na kuamua kumsajili aliyekuwa kocha raia wa Serbia Klabu ya Simba ilisema kuwa imejiridhisha juu ya ubora na uzoefu wa kocha Zoran hasa katika Soka la Afrika ambacho ndicho kigezo kikuu kilichozingatiwa katika kumuajiri.
Kabla ya kutua Simba SC, Kocha Zoran mwenye umri wa miaka 59 alikuwa anaifundisha Al Tai FC ya Saudi Arabia ambayo alijiunga nayo kutokea CR Belouizdad ya Algeria na kuiwezesha kufika robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Klabu ya Simba SC imempa malengo ya kuhakikisha anaifikisha Klabu hiyo Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) pamoja na kuurejesha Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) na Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup).