Alizaliwa kwenye kambi za wakimbizi ukanda wa Gaza mwaka 1965
Aliwahi kufungwa kwenye majela ya Israel miaka ya mwanzo ya tisini
Ndie kamanda mkuu wa kikundi cha kijeshi, Qassam Brigades, cha Utawala wa Hamas wa Palestina
Anatafutwa kwa udi na uvumba na vyombo vya kijasusi na kijeshi vya Israel
Ni maarufu na hajulikani, infamous and anonymous
Akikatisha leo hii kwenye mitaa ya Wapalestina anaopigania uhai, uhuru na hazi zao si wengi watakaomtambua
Ana jicho moja na mkono mmoja, alikatwa miguu
Amenusurika kufa mara tisa
Hashobokei simu wala computer wala camera, vigumu kumdukua na kujua aliko
Moja ya kombora alilodondoshewa mwaka 2006 lilimuua mkewe Widad, binti yake wa miaka mitatu na kijana wake mchanga, Ali, yeye hakuwepo nyumbani
Kihistoria ni mkuu wa pili wa kikosi cha Qassam Brigades, majukumu aliyopokea kutoka kwa mkuu wa kwanza, Salah Shehadeh, aliyeuliwa mwaka 2002
Yeye ndio aliye dizaini mfumo wa makombora ya roketi ya Palestina na mifumo ya maandaki wanakojificha wapiganaji
Ana kura ya veto dhidi ya maamuzi ya Hamas japo ni mtiifu kwa viongozi wa kisiasa wa Hamas
Kabla ya machafuko ya Gaza Deif alikubali kusitisha mpango kabambe wa mashambulizi na utekaji wa raia na wanajeshi wa kiyahudi baada ya viongozi wa kisiasa wa Hamas kuliasa jeshi lao kufuta mpango huo
Israel wanakiri kwamba Muhammed Deif ni kamanda mzuri wa majeshi